Yanga yapata pigo jingine tena Deus Kiseke apata ajali ya pikipiki

Kuelekea katika mchezo wa kombe la shirikisho  Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana, Timu ya Yanga imeendelea kupata majanga kwa baadhi ya wachezaji wake tegemeo baada ya winga, Deus Kiseke, Kupata ajali ya pikipiki
jana eneo la Ubungo akiwa anaelekea kwenye mazoezi uwanja wa BokoVetarani, Jijini Dar es salaam.
Tukio hilo lilitokea saa 9:15 asubuhi, wakati mchezaji huyo akitokea nyumbani kwake Kigogo, hivyo kufanya wachezaji watano majeruhiwa timu hiyo wengine wakiwa ni Geofrey Mwashiuya, Juma Mahadhi, Malimi Busungu na Haji Mwinyi.
Hali hii inaonyesha hali mbaya Jangwani imetua, Kwani mbali na majeruhi hao Mshambuliaji Mzimbambwe, Donald Ngoma, anasumbuliwa na malariahuku Obrey Chirwa na Nadir Harub Cannavaro wakiomba rihusa baada ya kupata matatizo ya kifamilia.
Akithibitisha hayo Daktari wa timu hiyo, Edward Bavu, alisema hali ya winga huyo inaendelea vizuri baada ya kupata matibabu kwa michubuko aliyopata katika mwili wake."Kaseke anaungana na wachezaji wengine majeruhi, Mwashiuya na mwinyi bado wanasumbuliwa na maumivu ya goti wakati jana Mahadhi alijitonesha jeraha alilopata katika mchezo wa TP Mazembe uliochezwa June 28, 2016 jijini Dar es salaam" alisema Bavu.....Kocha Mkuu wa Yanga asema bado Yanga iko vizuri bofya hapa

















Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top