Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha



Baada ya Bunge la Tanzania kupitisha marekebisho ya sheria ya kodi ya ongezeko la thamani ‘VAT’ ya mwaka 2014 kuanzia July 01 2016 kwenye huduma za kifedha kwa kurekebisha kifungu cha 13 cha jedwali la
msamaha wa kodi.


Mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji kuhusu marekebisho hayo ya sheria.

Leo July 01 2016 Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA’, Alphayo Kidata amezungumza na waandishi wa habari na kusema kuna taarifa ambazo si za kweli zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa VAT itatozwa kwanye amana ya mwenye fedha kwenye benki. Hii siyo kweli, ukweli ni kuwa kiasi cha VAT kitakachotozwa ni asilimia 18 ya kiasi cha gharama ya huduma iliyotolewa na benki au taasisi yoyote ya fedha.


Kidata ameeleza mfano huu; Ada ya huduma ya benki ambayo mteja ametozwa ni sh 1000 kodi ya ongezeko la thamani itakayotozwa kwenye kiasi hiki ni sh 152.50 tu na benki kubaki na sh 847.50 kiwango hicho cha sh 152.50 ndicho kitakachorejeshwa serikalini na benki au taasisi ya fedha baada ya kupunguza kodi ya ongezeko la thamani iliyolipwa kwenye manunuzi ambayo yamefanywa na benki au taasisi ya fedha husika.


TRA imezitaka benki na taasisi za fedha zilizoamua kwa makusudi kutoa taarifa zisizosahihi kwa umma kuacha mara moja vinginevyo hatua kali zitachukuliwa.

Aidha imeziagiza benki na taasisi zinazohusika kurekebisha mara moja taarifa walizokwishazisambaza ili zibebe maudhui sahihi ya marekebisho ya sheria hii.


 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top