Waziri Mkuu Asitisha Vibali Vya Uvunaji Mbao


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesitisha utoaji wa vibali vya uvunaji wa mbao kutoka katika mashamba nane ya miti ya kupandwa yanayosimamiwa na Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii inamiliki mashamba ya miti ya kupandwa 18, na kati ya hayo uvunaji umekuwa ukifanyika katika mashamba nane ambayo ni
Sao Hill (Mufindi),
Buhindi (Sengerema),
Meru/Usa (Arumeru),
West Kilimanjaro (Hai),
Shume (Lushoto),
North Kilimanjaro (Rombo),
Kiwira (Rungwe) na
Kawetire (Mbeya Vijijini).
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Julai 8, 2016) na kufafanua kwamba usitishaji huo unalenga kutathmini taratibu, kanuni na vigezo sahihi vinavyotakiwa kutumika katika kugawa malighafi kutoka kwenye mashamba hayo.

Amesema wadau wote wa viwanda vinavyojikita katika malighafi ya misitu na hususan wamiliki wa viwanda vya kupasua mbao wanashauriwa kuwa watulivu wakati utaratibu huu ukifanyiwa mapitio na umma utatangaziwa rasmi pindi uboreshaji huo utakapokamilika.

NAFASI TANO ZA KAZI BOFYA HAPA

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa July 08, 2016 bofya hapa




1 maoni:

Mpango wa Madawati itakuwaje sasa?

Reply

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top