Tupo vizuri- Kocha Mkuu wa Yanga Pluijm


 
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amesema maandalizi yao kuelekea mchezo wao wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Madeama ya Ghana yanaendelea vizuri na kwamba kikosi chake kitafanya
maajabu kwa kufika fainali za michuano hiyo.

Yanga ipo kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo ambapo imepoteza mechi mbili za mwanzo dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria na TP Mazembe ya Congo DR.

Akizungumza na gazeti hili jana, Pluijm alisema kitu cha kufurahisha ni kurejea kwa baadhi ya wachezaji wake walioukosa mchezo uliopita wa Mazembe ambao ni Simon Msuva, Oscar Joashua na mshambuliaji wake Amissi Tambwe.

“Maandalizi yetu yanakwenda vizuri na wachezaji wana ari kubwa wakiniahidi ushindi muda tulioupata kutoka mchezo wetu wa mwisho umetusaidia sana hata wachezaji wetu walio majeruhi wamepona na Obrey Chirwa naye amezidi kupata muda wa kuzoeana na wenzake kiuchezaji kitu ambacho ni faida kwetu,” alisema Pluijm.

Yanga inatarajia kucheza na Madeama Julai 15 kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Wawakilishi hao wanashika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi A ikiwa haina pointi baada ya kupoteza michezo yake miwili.

Pluijm alisema matokeo hayo hayajawakatisha tamaa kwani bado wana uwezo mkubwa wa kushinda mechi zao nne zilizobaki na kutinga nusu fainali na baadaye kucheza fainali kitu ambacho anajua kitawashangaza wengi.

“Najua watu wengi wametutoa kwenye mashindano baada ya kuanza vibaya lakini niwaambie nina imani kubwa na timu yangu na kuwa uwezekano mkubwa wa kuwashangaza watu mwaka huu kwa Yanga kucheza fainali ya michuano hiyo kwa sababu tuna timu bora iliyokamilika,” alisema Pluijm.

Kocha huyo raia wa Uholanzi alisema, mikakati yao kwa sasa ni kuhakikisha hawapotezi hata mchezo mmoja kati ya minne iliyosalia lengo ni kupata pointi 12, au tisa kitu ambacho kinawezekana kutokana na utayari waliokuwa nao wachezaji wake.

 HABARI KUU LEO BOFYA HAPA 
















Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA


















Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top