Mourinho amkejeli tena Arsene Wenger



Mourinho
Mkufunzi Jose Mourinho amesema kuwa yuko tayari kuchukua jukumu la kuifunza Manchester United, lakini akaonekana pia kumkejeli meneja
wa Arsenal Arsene Wenger.

Amesema ''niko mahala nitakapo''.

Raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 aliongezea: ''Nadhani ni kazi ambayo kila mtu anahitaji na sio wengi ambao huipata na mimi nimeipata''.

Alipoulizwa iwapo ana chochote cha kujionyesha baada ya kufutwa kazi akiwa Chelsea, alijibu, akionekana kumrejelea Wenger: ''Kuna mameneja ambao hawajashinda mataji kwa kipindi cha miaka 10 iliopita. Wengine bado kabisa. Mara yangu ya mwisho kushinda taji ni mwaka uliopita''.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea anachukua mahala pake Louis Van Gaal,ambaye alifutwa kazi baada ya United kushinda kombe la FA mnamo mwezi Mei.

Mourinho anasema kuwa anachukizwa kuona kwamba United haitashiriki katika mechi za kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao lakini akasisiiza kuwa yuko Old Trafford kushinda mataji. Arsene Wenger

Nataka kila kitu,alisema.Nataka kushinda mechi,nataka kucheza vizuri sitaki kufungwa magoli.nataka mashabiki kutuunga mkono.

''Ni kweli hatuwezi kupata kila kitu, lakini tunataka''.
Breaking News:Kesho Sikukuu ya EID Bofya hapa 
  
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA


















Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top