MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kupungua kwa mizigo bandarini kumeathiri si Tanzania pekee bali dunia nzima na kwamba kubanwa kwa mianya ya wizi kumesababisha kuongezeka kwa
mapato kutoka Sh bil 458 Aprili mwaka huu kufikia Sh bil 517.
Aidha, TRA imesema itaanza uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipakodi (TIN) kutokana na kuwepo watu wenye namba mbili na wasiohakiki watalazimika kudaiwa kodi na TRA.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari jana, Kamishna wa TRA, Alphayo Kidata alisema upungufu huo wa mizigo bandarini umezikumba pia bandari za Beira, Msumbiji, Mombasa, Kenya na kwingineko na kusababisha mapato kupungua.
“Lakini sisi pamoja na upungufu wa mizigo bandarini makusanyo yanazidi kuongezeka kutokana na kuzibwa mianya ya kukwepa kodi, hivyo napenda kuwapongeza wafanyakazi wote wa mamlaka na kusema kwa sasa hakuna mtu anayeweza kukwepa kodi na wale waliozoea wakae katika njia kuu,” alisema Kidata.
Kidata alisema wananchi wanatakiwa kuwaunga mkono kwani sasa kodi inaonekana katika kufanya shughuli za serikali kama kuboresha miundombinu pamoja na kutoa elimu bure.
Alisema TRA imefikia na kuvuka lengo la makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2015/16 kwa kukusanya Sh trilioni 13.8 sawa na asilimia 100.04 ya lengo la kukusanya Sh trilioni 13.4 iliyokuwa imepangwa na serikali.
Kidata alisema katika kipindi cha Juni mwaka huu, TRA imekusanya Sh trilioni 1.4 sawa na asilimia 107.83 ya lengo la kukuzanya Sh trilioni 1.3 ambapo makusanyo ya mwaka wa fedha 2015/16 ni sawa na ongezeko la asilimia 23.70 la makusanyo ya mwaka 2014/15.
Akizungumzia mashine za kielektroniki za EFDs, Kidata alisema walipoanza utoaji mashine hizo zilikuwa 5,703 na mpaka sasa mashine 1,700 zimegawiwa kwa watumiaji na wataanza kupita duka hadi duka kuhakiki matumizi ya mashine hizo.
Kamishna wa mapato ya ndani, Elijah Mwandumbya, alisema mwaka huu wa fedha wamejipanga kuhakikisha wanaondoa changamoto kwa mtu mmoja kuwa na TIN zaidi ya moja hivyo watafanya uhakiki.
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
News alert:Orodha ya Majina ya Makatibu Tawala wa Wilaya walioteuliwa jana Bofya hapa
Video:Leo sikukuu ya Eid mtazame na sikiliza ujumbe wa Mufti Abubakary Zuberi alioutoa jana akithibitisha kuandama kwa mwezi pia sikiliza ratiba kamili ya leo ya Sikukuu ya Eid
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatano July 06, 2016 Sikukuu ya EID
MKE MPYA WA KING MSWATI 2016 Bofya hapa
News alert:Mtuhumiwa wa Ujambazi Maduka ya Pesa, Mauaji Msikitini Awatoroka Polisi aliwatorokaje bofya hapa
AJALI: Masihara ya madereva yasababisha vifo na majeruhi wengi Singida Bofya hapa
Lowassa alijikuta akisimamishwa na wanachi waishio mpakani mwa Kenya na Tanzania Bofya hapa
LOWASSA APIGIWA SALUTI NA WANAJESHI LEO JUMAPILI JULY 03, 2016 Bofya hapa

Video:Chadema kuzuia Mkutano wa CCM wa kuchagua mwenyekiti wa chama Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa
Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA