Kampuni ya mabasi ya City Boy iliyoua Watu 30 yafungiwa



Siku moja baada ya kutokea ajali ya mabasi iliyosababisha vifo vya watu 30 na majeruhi kadhaa, Kampuni ya mabasi ya City Boy imefungiwa kufanya biashara
hiyo kwa muda usiojulikana.


Ajali hiyo ilitokea eneo la Maweni, Manyoni, mkoani Singida baada ya mabasi ya kampuni hiyo, moja likitokea Dar es Salaam na lingine likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam kugongana.


Msemaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), David Mziray amesema leo kuwa kampuni hiyo ina miliki mabasi 12 na yote yamefungiwa kufanya safari yoyote kuanzia leo.


“Mabasi hayo yamefungiwa kuanzia leo kwa muda usiojulikana, ukaguzi wa mabasi yao utaanza kufanyika kupitia jeshi la polisi,” amesema Mziray.
 HABARI KUU LEO BOFYA HAPA 
















Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA



















Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top