TANZANIA PRISONS YAMSAINI SAMATTA NA WENGINE WAWILI



KOCHA wa Tanzania Prisons, Salum Mayanga amemsaini golikipa Andrew Ntala kuwa mrithi wa Beno Kakolanya aliyetimkia Yanga SC baada ya kuwa na msimu mzuri. Timu hiyo ya Mbeya iliyomaliza nafasi

ya nne msimu uliopita imewasaini pia wachezaji wawili wa nafasi ya kiungo, Kazungu Nchinjayi kutoka Majimaji FC na Mohammed Samatta kutoka JKT Mgambo iliyoteremka daraja msimu uliopita.

“Ni kweli nimesaini mkataba wa mwaka mmoja katika timu ya Tanzania Prisons siku ya Jumatano ya Idd nikiwa na Samatta na Ntala,” anasema Kazungu anayecheza namba 4 na 6.
Credit:Dauda
Breaking News : Orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri na Majiji walioteuliwa leo na Rais Magufuli bofya hapa

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top