Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA ahojiwa na Jeshi la Polisi Dar



Patric Ole Sosopi (kushoto mwenye gwanda).

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Taifa(BAVICHA), Patric Ole Sosopi jana alihojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa tuhuma ya kutoa
lugha chafu inayotishia uvunjifu wa amani.

Patric Ole Sosopi (mwenye gwanda).

Sosopi alifika kituoni hapo saa 4.10 asubuhi huku ameambatana na wakili wake Frederick Kikwelo huku wakisindikizwa na wafuasi watano wa chama hicho.

Akizungumzia suala hilo baada ya kutoka polisi mwanasheria wake alisema mwenyemkiti huyo alihojiwa kwa nusu saa na alipewa dhamana na jeshi la polisi huku wakiendelea na upelelezi wao ambapo ukikamilika watakabidhi kwa mwendesha mashtaka kwa ajili ya kupitia ushahidi.

Sosopi alisema baada ya kuhojiwa alielezwa na jeshi la polisi kuwa arudi Julai 18 mwaka huu lakini hawajampa sababu ya msingi ya kurudi siku hiyo.

“Polisi hawajanipa sababu ya msingi ya kurudi Julai 18 mwaka huu,”alisema Sosopi. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu alichohojiwa Sosopi, alisema hana taarifa hizo hivyo atafuatiulia.
Breaking News : Orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri na Majiji walioteuliwa leo na Rais Magufuli bofya hapa

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top