RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 49 & 50 (Mwisho)


Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA


ILIPOISHIA
“Tumekupata”
Alipokea jibu mmoja kutoka, makao makuu. Wakaendelea kujibu mashambulizi ya watu hao ambao wamewavamia na hawakujua niwatu wangapi. Hali katika eneo la mto ikazidi kuwa mbaya zaidi milio ya bunduki, ilizidi kurindima kila kona.
“Helcoptar…..!!!”
Anna alishangaa baada ya kuona helcoptar zipatazo sita za jeshi la marekani zikifika katika eneo hilo, huku wajeshi wengi wakishuka kwenye helcoptar hizo zilizopo hewani, kwa kutumia kamba ndefu hadi chini.
‘Tunakufa leo’
Halima alijisemea kimoyo moyo huku akiendelea kuftyatua risasi nyingi kuelekea walipo wanajeshi hao.


ENDELEA
“Sister nguvu yetu imesha anza kuwa ndogo tunafanyaje”
Jamaa mmoja alizungumza huku akibadili magazine ya mwisho katika bunduki yake na endapo risasi zitakwisha kwenye magazine hiyo, basi hatokuwa na msaada wowote.
“Endelea kupambana hatuwezi kurudi nyuma”

Fetty alizungumza huku akizendelea kufyatua risasi kuelekea walipo wanajeshi hao
“Fetty eheee omba msaada kwa mkuu, lasivyo tutakufa humu”
Halima alilalamika kama kawaida yake, Fetty kutazama idadi ya wanajeshi wanao shuka kwenye helecoptar hizo kubwa za kijeshi, ikambidi awasilianen na bwana Rusev.
“Muheshimiwa wanajeshi wa Marekani wametuvamia”
“Endeleni kupambana”
“Sawa muheshimiwa ila tunahitaji msaada wa vijana wengine”

“Msaada….. Masaada wa nini pambaneni”
Majibu ya bwana Rusev, yakamtia hasira Fetty aliye jibanza kwenye mti huku akisikilizia jinsi risasi hizo zinavyo zidi kupigwa kwenye sehemu walipo.
“Muheshimiwa nakuheshimu, ila narudia tena nahitaji msaada wako”
“Kama hamjampata Agnes basi, hakuna cha msaada wowote kutoka kwangu”
Mawasiliano yakakatwa, Fetry akabaki aking’ata meno yake kwa hasira. Kumbukumbu ya tukio hili likamrudisha miaka ya nyuma, jinsi siku wanajeshi wa Tanzania walivyo vamia kwenye kambi yao, na kuwashambulia sana kisha wakaingia mikononi mwao wanajeshi hao, hapo ndipo ulipo kuwa mwisho wa maisha yao ya furaha na amani na wakajikuta wakiwa wanaishi kama wakimbizi na kukubali kufanya kazi na watu ambao ni magaidi wa kidunia, ili mradi waweze kuendelea kuishi kwenye maisha haya.

Fetty akiwa katika mawazo hayo, akamshuhudia kijana mmoja wa bwana Rusev akianguka chini, baada ya kupigwa risasi ya kichwa, akiwa anashangaa tukio hilo, kijana mwengine akajitokea kwa hasira kwenye mti alio kuwa amejificha huku akiwa na bastola mbili mkononi mwake, akifyatua risasi zisizo na idadi, ila alicho weza kukutana nacho, ni mvua ya risasi zizizo toka kwenye jeshi lilio wazidi nguvu.
“Fetty amesemaje”
Halima alizungumza huku machozi yakimlenga lenga.
“Mmmmmm…….”
“Amesemaje mkuuuuuu…..”
“Hana msaada na sisi, tupambane kama kufa tufe ila si kukamatwa”

“Mungu weeeee, nini sasa hichi”
Halima alizungumza huku machozi yakimwagika, akachomo magazine kwenye bunduki yake na kukuta ikiwa na risasi chache, akajipapasa hana tena magazine. Akageuza kichwa sehemu alipo Anna, akamkuta akiendelea kufyatua risasi pasipo kuangalia wezake wapo katika hali gani. Vijana wawili wa bwana Rusev walio bakia, wanazidi kuyapigania maisha yao kwani ni heri kufa kuliko kukamatwa na jeshi hilo.
“Nakupenda Anna, Fetty”
Halima alizungumza kwa sauti ya unyonge, akairudishia Magazine yake kwenye bunduki, akapiga goti mmoja chini, akawatazama jinsi wanajeshi wa wanavyo zivurumisha risasi katika eneo walipo.
“One one one bullet”(Mtu mmoja, risasi moja)
Halima alizungumza huku akiendelea kufyatatua risasi kwa kila aliye weza kumuona kwa wakati huo. Ila zilipo fika risasi kumi na mbili, bunduki yake ikagoma kutoa risasi, ikiashiria kwamba hakuna risasi nyingine ndani ya bunduki hiyo aina ya AK47, zinazo tumika sana nchini Russia.
***
Asubuhi na mapema, raisi Praygod akakurupuka kitandani, akaka kitako huku akionekana kuwa na wasiwasi mwingi sana. Rahabu taratibu akajinyanyua na kumtazama jinsi anavyo tokwa na jasho jingi mwilini.
“Una tatizo gani mume wangu?”
“Naota mandoto mabaya mabaya tu”
“Ohoo pole mume wangu”

Rahab alizungumza huku akimkumbatia raisi Praygod, taratibu akaanza kumpapasa kifuani mwake, hisia za mapenzi zikaanza kuusisimua mwili wa raisi Praygod, taratibu akajikuta akianza kumnyonya mke wake mdomo, baada ya muda wakajikuta wakizama kwenye dimbwi zito la kupena haki ya wanandoa.
Baada ya kumaliza wakaingia bafuni kuoga, Rahab akamuandalia mume wake nguo za kuvaa kwenye kikao anacho kwenda kukifanya na wakuu wote wa kitengo cha usalama wa taifa.
“Leo nitapendeza sana mke wangu”
“Kwa nini?”
“Umenichagulia nguo wewe”
“Ahaaa si kawaida”
“Sawa ila utapendeza sana, siku zote nimezoea kujichagulia nguo mwenyewe”

“Ila si una wafanyakazi wenye jukumu hili?”
“Ndio ila mke wangu upo kwa nini nichaguliwe na mfanyakazi”
“Hapa utakuwa poa sana”
Rahab alizungumza baada ya kumfunga tai raisi Praygod, akampiga busu la mdomoni
“Twende tukapate kifungua kinywa pamoja”
Wakatoka na kwenda kwenye sebla yao, ambapo wakakuta chakula tayari kimesha andaliwa na kukaguliwa na daktari maalumu anaye weza kukagua chakula cha raisi kabla hajakila. Wakapata chakula baada ya kumaliza akaomba kuweza kuitiwa wafanyakazi wote wa ikulu, ikawa kama alivyo agiza.
“Nimewaita hapa kutokana nahitaji kuwatambulisha mama yenu, so mukimuona huko nje misije mukamdharau.”
“Muheshimuni kama munavyo niheshimu mimi, mpendeni kama munavyo nipenda mimi. Nisinge penda mtu yoyote kuweza kuona mtu ana….ana anaa mkosea adabu”
“Mumenielewa”

Ndio muheshimiwa”
Baada ya utambulisho huo, raisi Praygod akawaamuru wafanyakazi wake kuweza kuondoka, akabaki na mke wake. Akamtuma mmoja wa walinzi wake kwenda kumuita Samson kwenye chumba chake. Samson akafika katika sehemu walipo.
“Umeamkaje muheshimiwa”
Samson alisalimia kwa heshima
“Salama tu kaa”
“Madam Rahab je wewe umeakaje?”
“Nipo salama”
Kwa nguvu aliyo weza kumuwekea Samson. Rahab anamamlaka makubwa ya kuweza kumuamrisha Samson, akafanya kile alicho weza kumuambia.
“Jiandaeni kwani nitawahitaji kwenye kikao baada ya muda fulani hivi”
“Baby kwa nini sisi?”
“Nahitaji tusaidiane katika kuirudisha heshima ya nchi, pia kesho tutakwenda kwenye misiba ya wanajeshi wali fariki walipo kuwa wakimsafirisha makamu wa raisi”
“Kwani hawakuzikwa?”

“Ndio, hawajazikwa, nimeagiza kwamba iwe siku ya maombolezi kwani pia wale wananchi walio poteza maisha uwanja wataifa inabdidi kuzikwa kesho”
“Sawa”
Raisi Praygod akawaaga, akaongozana na walinzi wake wawili hadi chumba cha mkutano.
“Hivi umempataje pataje raisi?”
Samson alizungumza huku akiachia tabasamu pana usoni mwake
“Ni story ndefu sana, tangu tuachane pale kwenye ndege basi ikawa ndio siku ya mimi kuweza kuonana na raisi Pray”
“Ahaaa maisha haya bwana, adui yako amekuwa mume wako”
“Usiongee kwa sauti kubwa, tusije kuhisiwa vibaya. Ila kusema kweli ninampenda mume wangu”
Samson hakuwa na chakuzungumza zaidi ya kuanza kupata kifungua kinywa, Rahab akaondoka na kuelekea chumbani kwao kujiandaa na kikao ambacho mume wake alimuhitaji kuweza kufika.
***
“Kila mmoja ninaamini ameyaona yaliyo jitokeza.”
“Nchi imepata fedheha mbele ya wageni, walio huzuria msiba ulio kuwa wangu pamoja na wahanga wengine. Kiongozi mkubwa wa nchi kuweza kufanya mambo ambayo yangefanywa na wagaidi ameweza kuyafanya yeye.”
“Inaonekana ni jinsi gani, kitengo chenu, kilivyo jisahau kwa asiliimia nyingi tuu kwani hadi inafikia hatua ya matukio ya ajabu kama kushambuliwa kwa wanajeshi na makamu wa raisi kutoroshwa, yote ni uzembe na inavyo onekana anamiliki kundi kubwa la vijana anao weza kuwatumia katika kuleta machafuko kwenye nchi hii.”

Raisi Praygod alizungumza kwa saut iliyo jaa msisitizo mkubwa huku akiwatazama viongozi hao wapatao kumi na mbili walio izunguka meza kubwa katika eneo hilo.
“Yote yaliyo weza kujitokeza, hayaweze kubadilika, ila tunaweza kuyafanya wananchi wakaweza kutuamini na kuishi kwa amani. Kwani inavyo onekana hali ya amni imekuwa tata kwa wananchi.”
“Hivyo basi, nitahakikisha kwamba tunafanya kazi, iliyo wafanya kila mmoja wenu kuwa katika kitengo alicho kuwepo. Hata mimi mwenyewe nitahakikisha kwamba ninafanya kazi zote zakijeshi kama ni kuua basi tuue yule anaye stahili kuuliwa.”
“Sinto kuwa na msamaha kwa mtu ambaye ukimpa nafasi moja, anakuua wewe. Kuanzia sasa nahitaji kusikia ni wapi alipo makamu wa raisi wangu, yeye na kundi lake tuweze kuwatia nguvuni kwa pamoja. Nakaribisha maoni”

Raisi Praygod akazima maiki yake aliyo kuwa akitumia kuzungumzia. Kiongozi mmoja akanyoosha kidole na raisi Praygod akampa nafasi ya kuzungumza
“Muheshimiwa, kwanza tuombe radhi ya yale yaliyo jitokeza. Pili tumeweza kupata sehemu ambayo makamu wako amejificha na kundi lake”
“Ni hapa ndani ya nchi?”
Raisi Praygod alizungumza huku akimtumbulia macho kiongozi huyo.
“Hapana si ndani ya nchi hii, ila yupo nchini Kenya, na taarifa hizi tulizipata kwa wana usalama wa nchi ya Kenya”
“Eheee mu..mu muu mumejipangaje?”
“Tulimesha andaa taskforce kuweza kuvamia katika sehemu hiyo, huku tukishirikiana na interpol”
“Fanyeni mawasiliano na raisi wa Kenya sasa hivi nizungumze naye”
***
“Kwa nini memenisaidia?”
Agnes aliuliza swali baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa akiwa na Jackline pamoja na Monk
“Kwani inatubidi kurudi nchini kwetu kuimarisha ulinzi na si kuendelea kutumika katika vikosi vya ajabu”
“Umejuaje kama ni vikosi vya ajabu na umenifamu fahamu vipi mimi?”
Agnes aliendelea kumuuliza maswali Jackline ili kuweza kumfahamu vizuri
“Kipindi nyinyi munakuja kwenye ngome ya bwana Rusev, mimi nilikuwa ni miongoni mwa walinzi wake wakaribu. Wiki moja baada ya nyinyi kufika pale mimi nilipewa kazi ya kwenda kumuangamiza raisi wa Korea kaskazini.”

“Ilikuwa ni kazi ngumu sana kwangu, hii ni kutokana na umahiri wa ulinzi wa kiongozi huyo. Ila nilijaribu kufanya ninacho weza, nikiwa katika sura ya bandia, iliyo nifanya nionekane kama mjapan.”
“Nilizidiwa kwa mashambulizi ya walinzi wa kiongozi huyo. Nilipo jaribu kuomba msaada kwa kiongozi bwana Rusev aliniambia………”
Jackline akashusha pumzi kubwa kisha akaendelea kuzungumza
“Akaniambia niendelee kupambana tu kwani ni kazi ninayo takiwa kuikamilisha mimi mwenyewe.”
“Niijitahidi sana, nikafanikiwa kuwakimbia pasipo kuweza kunikamata, ila niliweza kupata majeraha kadhaa ya risasi mgongoni mwangu”

“Nilikwenda kwenye temple moja ambapo ndipo nilipo kutana na Monk”
“Temple ni nini?”
“Ni nyumba ya ibada, ni sawa na kama kanisa au msikiti”
“Mzee huyu aliweza kunileta huku, aliweza kunitunza kama mwanae, ila aliweza kunitafutia waalimu walio weza kunifundishi ujuzi mkubwa wa kupambana, kuanzia kung fu, kareti, judo, krobariotik, ninja”
“Kwahiyo nimefuzu katika hayo yote, lengo langu kubwa ni kuweza kwenda kuhakikisha siku ninamuondoa dunia bwana Rusev yeye na kundi lake kwani hana msaada wowote kwa sisi waafrika, anawajali sana wa russia wezake”
Hapo kidogo Agnes akaanza kufunguka akili yake, swali alilo anza kujiuliza ni kwa nini alitumwa yeye, na kwa nini alipaswa kwenda kuua viongozi wakubwa kama hao. Swali kama hilo halikuwa na jibu kichwani mwa Agnes.

“Ila hili ni ombi, sinto hitaji kukulazimisha. Kama unahitaji kuwa nawi unaweza kuungana nami na tukarudi Tanzania na ukafanya yaliyo mema kujisafisha jina lako. Ila kama hauto hitaji basi unaweza kurudi kwa Russev na kuendelea kuishi chini ya bahari pasipo kuelelewa dunia inakwendaje”
Jackline alizungumza na kutuka nje ya nyumba hiyo. Agnes akabaki akitazamana na Monk huyo ambaye muda wote yupo kimya. Agnes akanyanyuka na kutoka nje.
“Nahitaji mafunzo”
Agnes alizungumza akimtaza Jacklin usoni mwake
“Je utakuwa tayari kurudi Tanzania?”
“Nipo tayari kurudi Tanzania”
“Basi mazoezi tunaanza sasa”
Jackline alizungumza, akamtisha Agnes kama anarusha ngumi, Agnes akakwepa, kidogo ila akastukia akipigwa teke la kifua lililo muangusha chini.
“Umakini ni muhimu sana”
Jackline alizungumza huku akimpa mkono Agnes na kumnyanyua kutoka chini alipo angukia
***
Hadi kuna pambazuka hapakuwa na msaada wowote kutoka kwa bwana Rusev. Fetty na wezake wakajikuta hali ya mashambulizi ya wanajeshi yakiwazidi na kujikuta wakikata tamaa kabisa. Kijana mmoja wa bwaa Rusev baada ya kuona hali imekuwa ngumu kwa upande wao. Akajichoma kisu cha tumbo na kujiua, jambo lililo zidi kuwachanganya Fetty na wezake.

Wa pili baada ya kuona mwenzake amekufa, akachomoa risasi moja aliyo ihifadhi mfukoni, akaiweka kwenye magazine ya bastola yek iliyo isha risasi, akairudisha magazine kwenye bastola yake, kisha akajipiga risasi ya kichwa na kufa hapo hapo.
Wakabaki Fetty, Anna na Halima wakishangaa tukio hilo, hawakuwa na risasi kwenye bunduki zao, na kila walivyo chungulia wakawaona askari wakizidi kusogea katika eneo walipo


SHE IS MY WIFE(50)

Hapakuwa na aliye weza kumsemesha mwenzake, kwani hali ya hatari tayari kila mmoaja aliweza kuiona. Wingi wa wanajeshi uliwafanya ujasiri wa kuweza kutoroka katika eneo hilo upotee.
“Haya ndio malipo yetu”
Halima alizungumza huku akimwagikwa na machozi mengi, kwani hakuamini kama leo hii anaweza kukamatwa tena, kwenye nchi ya ugenini. Fetty akawatazama wezake, jinsi walivyo wanyonge, taratibu akasimama kisha taratibu akajitokeza kwenye mti alio kuwa amejificha, bunduki za wanajeshi baadhi zikaelekea kwake, akiashiria kwamba yupo tayari kwa kufa
***
Mawasiliano ya kitelejensia yakaweza kufanyika kati ya majasusi wa Kitanzania na Kenya. Vikosi vikaandaliwa kwa ushirikiano mkubwa kwenda kufanya uvamizi kwenye hotel ya makamu wa raisi aliye kuwa msaliti kwenye nchi yake. Kwa usiri wa hali ya juu vikosi hivyo vikaweza kujongea kwenye hotel hiyo, ila chakushangaza ukimya mwingi wa hotel hiyo uliwafanya hata majasusi hao kuweza kushangaa kwani hawakujua ni kwanini eneo hilo lipo kimya kiasi kwamba wasiwasi uliweza kuwaingia.

Wakiwa katika eneo hili, wakaanza kustukia kuona baadhi ya majengo yakianza kulipuka kwa mabomo yaliyo tengwa ndani. Ikawabidi wote kutawanyika ili kuyaokoa maisha yao. Hoteli nzima iliweza kuporommoka kwa mabomu, na kubaki vipande vipande vya kuta ndogo ndogo na chakavu, jambo lililo zidi kuwachanganya majasusi hao
Taarifa za kulipuka kwa hoteli hiyo, zikawafikia maraisi wote wawili wa Tanzania pamoja na Kenye. Raisi Praygod akabaki akiwa amechanganyikiwa asipate kujua ni nini anaweza kuzungumza kwani adui yake hadi sasa hivi hajulikani ni wapi alipo na nilini anaweza kufanya shambulizi litakalo itingisha nchi.

“Hajulikani alipo!!?”
Rahab aliuliza kwa msahangao mkubwa baada ya kupewa taarifa hiyo
“Ndio na hoteli nzima imelipuka”
“Kuna mtu kati ya watu nahisi anaweza kumwaga siri za mipango yenu ambayo munaweza kuipanga”
“Sasa atakuwa ni nani?”
“Kati ya viongozi hao hao wa usalama wa Taifa, ulio panga nao huo mkakati”
Raisi Praygod akajitupa kitandani akionekana kujichokea kisawa sawa, kila alilo lifikiria akaona halina jibu halisi.
“Naomba hiyo kazi uniachie mimi mume wangu”
“Kazi gani?”
“Yakumtafuta adui yako nina imani nitampata nikishirikiana na Samsoan”

“Ila kumbuka wewe ni MKE WANGU, mke wa raisi, sasa utaifanya vipi hiyo kazi”
“Nakuomba unipatie nina imani nitaweza kuifanikisha na wewe utafurahi”
“Ila utaingia matatizoni tena mke wangu, unadhani nitakuwa katika hali gani?”
“Usijali mke wako, tambua mimi ndio nilikulinda kwa uwezo wangu wote hadi leo umefikia hapa”
Raisi Praygod akamtazama mke wake kisha akampa mkono na kumvutia kitandani, akamlaza vizuri kifuani kwake
“Rahab kumbuka ninakupenda sana, tena sana. Sinto hitaji kukupoteza nina imani unalitambua hilo”
Raisi Praygod alizungumza kwa sauti ya unyonge, iliyo jaaa uchungu ndani yake.
“Ndio baby ila amini kwamba ninaweza kuifanya kazi hiyo”
“Sawa”

“Nitakupa vijna wa kukusaidia?”
“Hapana nahitaji kuifanya nikiwa na Samson, ila vijana wawe tayari sisi tukiimaliza kazi hiyo”
Raisi Praygod akashusha pumzi, kisha akamtazama Rahab usoni, taratibu akaendelea kuutadhimini uzuri wa Rahab. Kwa mbali machozi yakanza kumlenga lenga.
“Mbona hivyo baby?”
“Niahidi utaishi mke wangu na huto kufa?”
“Nakuahidi nitarudi, na nitaendelea kuilinda heshima yako pamoja na nchi yangu”

Raisi Praygod akamkumbatia mke wake kwa nguvu, taratibu Rahab akaanzisha uchokozi wa kuupeleka mkono wake katika maficho ya tango la raisi, taratibu Raisi Praygod akanza kutoa miguno ya kimahaba, iliyo zidi kumsisimua Rahab na kumfanya aongeze kasi kubwa katika kulichua tango hilo. Rahab akahakikisha anampa memewe penzi ambalo hakuwahi kulipata tangu wakutane, raisi Praygod, alijikuta akitukana kila aina aina ya tusi kwa jinsi alivyo zidi kuupata utamu wa mke wake kipenzi Rahab.
Baada ya mtanange mkubwa, taratibu Rahab akajilaza kifuani mwa raisi huku akihema taratibu, pumzi nzito iliyo pitapita kifuani mwa raisi Praygod.
“Nakupenda sana mke wangu”
“Nakupenda pia baby”
***
Agnes akazidi kufanya mazoezi kwa juhudi zake zote, huku kila mara akilini mwake akiwakumbuka marafiki zake alio waacha kwenye ngome ya bwana Rusev.
‘Fetty, Anna, Halima ninawapenda sana’
Agnes alizungumza huku akiendelea akupokea mafunzo makali kutoka kwa Jaquline, aliye amua kumfundisha vilivyo Agnes.
“Mbona roho ina niuma hivi?”
Agnes alimuuliza Jaquline, baada ya kumaliza kufanya mazoezi hayo, kwa siku ya kwanza
“Kuna tatizo baya limetokea”
“Tatizo…..!! Tatizo gani?”
“Hata mimi siwezi kufahamu ila ni tatizo ambalo litakuwa ni pigo kubwa sana kwako”
“Mmmmmm…..!!”

“Yaaa huwa ndivyo tunavyo weza kuamini. Na ukipitia katika mafunzo ya unija utaweza kukutana na hisia hizo.”
“Siku zote huwa hisia katika maisha ya binadamu ndio kitu kikubwa sana, kwani zinaweza kukufanya wewe kuepuka kwa jambo baya au kuingia katika jambo baya”
“Sasa nitawezaje kujua mafunzo hayo”
“Juhudu zako katika mazoezi ndizo zitakazo kufanya wewe kuweza kukutana na mafunzo mengine mapya”
“Yatachukua muda gani?”
“Sio muda gani, ila juhudu zako ndizo zitakuwezesha kuwahi au kuchelewa kufanya mazoezi”
Jaquline akaondoka na kumuacha Agnes akiwa anatafakari ni kitu gani ambacho anaweza kukifanya ili kujihimarisha katika mazoezi hayo. Akaitazama njia waliyo pita jana usiku kuingilia kijijini hapo, ambapo kuna nyumba nyingi zilizo tengenezwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi.
“Mungu ibariki Tanzania”
Agnes alijikuta akiyatamka maneno hayo pasipo kudhamiria, taratibu akaingia ndani ya nyumba hiyo.
***
Baada ya siri kuweza kuvuja ya kuweza kuvamiwa katika hoteli yake. Makamu wa raisi, pamoja na vijana wake wapatao kumi na mbili, wakatega mabumu kwenye hoteli nzima. Pasipo kujali ni hasara gani anayo weza kuipata kwenye hoteli hiyo, anayo ishi peke yake na vijana wake tu. Walipo maliza zoezi hilo, wakashuka chini ya ardhi kwenye njia zinazo weza kuwapeleka moja kwa moja hadi nchi ya Somalia, ambapo wanaweza kupotelea katika nchi za uarabuni pasipo kuweza kukamatwa na kuweza kuhukumiwa kifo.

“Wataisoma namba”
Makamu wa raisi alizungumza huku akicheka kwa dharau. Wakaendelea kutembea kwenye njia hizo zilizopo ardhini huku vijana wake wakiendelea kuimarisha ulinzi mkali kila wanapo pita. Matochi makubwa waliyo yabeba yaliweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kuendelea na safari yao hiyo, waliyo weza kukusanya vinywaji na vyakula vya kutusho.
“Yale mabumu uliyatega kwa muda gani?”
Alimuuliza kijana wake mmoja mtaalamu wa maswala ya kutega mabomu na kutegua.
“Niliyatega kwa dakika arobaini na tano”
“Ahaaa safi, kwa umbali huu tulio kwenda hata yakilipuka si hayata weza kutudhuru?”
“Ndio muheshimiwa”
“Basi tutafute sehemu tupumzikeni kwa maana nimechoka sana”

“Ila muheshimiwa kwa usalama inabidi tusonge mbele kwani hatuta weza kujua mabomu hayo kwa pammoja yanaweza kutudhuru sisi, kumbuka tupo chini ya ardhi”
“Sawa”
Wakazidi kusonga mbele huku makamu wa raisi akionekana kuchoka sana, mwili mkubwa wenye kitambi kikubwa, ulizidi kumuelemea na kujikuta akihema kama bata mzinga
“Hembu fanyeni mpango muwasiliane na general Godwin”
Alitoa amri huku akiendelea kuhema na kutembea mwendo wa kivivu vivu, gafla tetemeko la ardhi likaanza kutikisa sehemu walipo, makamu wa raisi akajikuta akistuka sana na kuhofia usalama wake.

“Nini hicho?”
“Mabomu ndio yanaiporomosha hoteli”
“Ohaaa”
Baada ya dakika moja tetemeko hilo kilatulia. Hapo makamu wa raisi hakuwa na hata muda wa kupoteza zaidi ya kuwaamrisha vijana wake waweze kusonga mbele.
“Mzee simu ipo hewani”
Kijana wake akampatia simu, akaichukua na kuiweka sikioni mwake
“Ndio ndugu yangu Godwin”
“Mipango naona imefeli?”
“Ndio kaka, yaani hapa nahitaji vijana wako wanisaidie bwana”
“Usijali mutapokelewa na madam”
“Madam, madam gani tena huyo?”

“Utamuona tu mukikutana mimi nipo mbali na Somalia”
“Sawa muheshimiwa”
Makamu wa raisi akakata simu na kuendelea kutembea, huku akiwa na mawazo mengi ni kwanini jaribio la kuchukua madaraka limeweza kushindwa
‘Nitajipanga tena, lazima niichukue Tanzania’
Alijisemea kimoyo moyo. Akawaamrisha vijana wake waweze kupumzika, ili wajipatie chakula na hata kama kuna uwezekano waweze kulala, kwani kwa jinsi saa yake ya mkononi inavyo muonyesha, wametembea zaidi ya masaa kumi na tatu na muda huo ni wakati wa usiku, japo ndani ya njia hizo kuna giza lisilo weza kuonyesha kwamba muda huu ni mchana au usiku.
***
Rahab hakuwa na muda wakupoteza, akaingia bafuni akaoga kuondoa uchuvu. Kisha akamuomba muwe wake kuweza kumfungulia kwenye chumba ambacho kuna silahan na vitu mbalimbali vya raisi anavyo weza kuvitumia pale panapo jitokeza tatizo la uvamizi wa kivita.
Rahab akachukua mavazi meusi ambayo siku zote ananamini, kwa mavazi kama hayo basi kazi yake huwa ni nzuri, akachukua bastola sita pamoja na magazine zakutosha zilizo jaa risasi.
“Nipo tayari”
Alimuambia raisi Praygod Makuya, aliye baki akimtazama tu, mke wake jinsi alivyo weza kujiandaa

“Kuna kitu umesahau?”
“Nini hicho?”
“Saa ya mkononi”
Raisi Praygod akamkabidhi Rahab saa moja, nyeusi inayo onekana kutengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu
“Saa hiyo, imefungwa, mitambu maalumu kwa kupitia satelait tutaweza kukuona kila unapo kwenda”
“Sawa mume wangu”
Rahab akamkumbatia Raisi Praygod na kumbusu mdomoni. Wakatoka chumbani kwao na kwenda katika chumba, walipo wakuta vijana wawili wa raisi pamoja na Samson wakiwa tayari wamesha jiandaa kwa kazi ya kwenda kumtafuta makamu wa raisi na kuweza kumkamata.
“Ninaimani watanzania wanatamani kuweza kuisikia taarifa ya kukamatwa kwa msaliti wao. Ninawapa baraka zote katika kazi hii munayo kwenda kuifanya”
“Asante muheshimiwa”
Vijana hao waliweza kuzungumza na kumpa heshima raisi Praygod, aliye achia tabasamu pana kidogo akionekana kufurahishwa na vijana hao ambao wamejitolea maisha yao kuweza kulitete taifa lao.

“Si kila kitu kipo tayari?”
Rahab aliuliza, huku akimtazama mume wake machoni?”
“Ndio mutaondoka na helcoptar hadi Kenya, kwenye hoteli ilipo kuwa na mutapokelewa na makamanda nilio waagiza kuwapokea nao bado wapo kwenye oparesheni hiyo”
“Sawa”
Wakatoka hadi kwenye kiwanja kidogo cha helcoptar, wakaingia kwenye moja ya helcoptar inayo kwenda kwa kasi. Safari ikaanza huhu raisi pamoja na walinzi wengine wakiwapungia mkono vijana wao.
“Sasa hivi ni saa nane usiku, hadi saa moja asubuhi oparesheni iwe imekwisha”
“Sawa madam”
Kwa mwendo kasi wa helcoptar hiyo, wakafika Kenye majira ya saa tisa usiku, wakashushwa katika eneo la hoteli ambapo ulinzi wa majasusi wa nchi mbili kati ya Tanzania na Kenye bado unaendelea.
“Mimi ninaitwa kamanda Lawi Okoye”
Kamanda mmoja wa kike alijitambulisha baada ya kuwapokea kutoka katika helcoptar hiyo iliyo waleta
“Mimi ni Mrs President”
“Karibuni”

Samson akabaki akiwa anashangaa, kwani majengo yote ya sehemu hiyo yameanguka chini na nikuta baadhi zimesimama.
“Sasa hapa atakuwa amepona mtu kweli?”
Samson alimuuliza Rahab huku wakiendelea kutembea kuelekea kwenye moja ya kibanda alipo mkuu wa kikosi hicho.
“Ngoja utaona tu”
Tatatibu Rahab, akachuchumaa, mkono wake wa kulia akauweka chini na kugusa ardhi, kwa uwezo na nguvu ya hisia zake, aliweza kugundua kwamba maadui zao wamepita chini ya ardhi na kwamuda huo wapo mbali sana na hapo walipo.
“No tunapoteza muda”
Rahab alinyanyuka haraka, akaanza kukimbia kuelekea porini huku vijana wake wakiwa nyuma wakiwafwata, hadi kamanda Lawi Okoye aliweza kuunga msafara huo.

“Munakwenda wapi hamuja onana na mkuu?”
Kamanda Lawi Okoye aliuliza huku akikimbia
“Hei miss hii ni kazi isiyo kuhusu, ningekuomba uweze kurudi na kuendelea kuimarisha ulinzi katika lile eneo”
Rahab alizungumza huku akimtazama kamanda Lawi Okoye kwa macho makali sana hadi yeye mwenyewe, akamuelewa Rahab pasipo kuuliza swali jengine. Rahab na vijana wake watatu wakendelea kusonga mbele
“Huku”
Rahab alizidi kuwaongoza vijana wake, kwa kufwata usawa wa sehemu ambapo njia hizo zilizopo ardhini zinaweza kupita. Kasi ya Samson na Rahab, ikazidi kuwatesa vijana wa raisi Praygod wanao onekana kuchoka sana kwa kukimbia.
“Wamechoka wale?”
Samson alizungumza baada ya kugeuka nyuma na kukuta vijana hao wamewaacha mbali sana
“Twende mbele, achana nao”
Rahab akazidi kuongeza kasi zaidi hadi vijana hao wakapotezana nao. Wakafika kwenye moja yam lima Rahab akasimama huku akihema sana. Akaitazama saa yake ya mkononi inaonyesha ni saa kumi na moja kasoro alfajiri.
“Hawa washenzi watakuwa wamelekea wapi?”
“Kwa nini?”
“Nimepoteza hisia ya kujua ni wapi walipo kwenda”
“Sasa tutafanyaje?”
“Ngoja”
***
Anna na Halima, wakamshuhudia Fetty akinyoosha mikono yake juu, ikiashiria kwamba amejisalimisha mikononi mwa wanajeshi hao, walio kuwa wanapambana nao usiku kucha. Machozi mengi ya uchungu yakazidi kumwagika Halima. Kwani hakuwa tayari kufa, naye taratibu akajitokeza huku akiwa ameinyoosha mikono yake juu. Anna naye hakuwa na jinsi akafanya kama walivyo weza kufanya wezake.
Ikatolewa amri na mkuu wa vikosi hivyo mabinti hao waweze kukamatwa. Fetty na wezake hawakuwa na ujanja zaidi ya kupiga magoti chini, na kujisalimisha. Wanajeshi wakawazingiza, wakiwa na silaha zenye uwezo mkubwa. Kila mmoja akavishwa pingu imara mikononi na miguuni wakafungwa cheni ngumu sana.

“Kumbe ni wasichana, washenzi sana”
Asakri huyo aliuzungumza huku akimtazama Fetty usuni aliye weza kufumba macho yake akionyesha kububujikwa na machozi ndani kwa ndani. Wakaichunguza miili ya magaidi wengine, wakawakuta wakiwa tayari wamesha poteza maisha. Ulinzi mkali ukaimarishwa hadi helcoptar sita zilivyo weza kufika katika eneo hilo, huku hecoptar moja ikiwa imebeba waandhishi wa habari wa vituo vikubwa viwili vya habari duniani BBC na CNN.
Tukio la wasichana watatu magaidi kukamatwa, likatawala vyombo vingi vya habari duniani, kila wenye vituo vya tv, waliweza kujiunga moja kwa moja na vituo hivyo viwili na kuonyesha hali inavyo weza kundelea katika msitu huo.
Bwana Rusev na watu wake wakashuhudia jinsi Fetty na wezake jinsi wanavyo ingizwa kwenye helcoptar hizo za jeshi.
“Muheshimiwa sasa ni kwanini hukuhitaji tuwapatie msaad……………”
Kabla ya kijana huyo hajamaliza sentensi yake, akapigwa risasi mbili za kifua na bwana Rusev anaye onekana kushikwa na hasira kali sana

“Huo ndio msaada ulio wapatia”
Bwana Rusev alizungumza kwa hasira, hadi vijana wengine waliomo ndani ya chumba hicho ya mawasiliano wakakaa kimya
“Munashangaa nini? Endeleeni na kazi iliyo waweka hapa na toeni hii takataka ya huyu mshenzi mbele ya macho yangu”
Bwana Rusev aliendelea kufoka, vijana wake wanao muogopa kila mmoja akaendelea na kazi yake huku baadhi wakiutoa mwili wa kijana huyo.
Moja kwa moja Fetty na wezake wakapelekwa kwenye kambi ya jeshi ya Marekani iliyopo Russia kwa ajili ya mahojino maalumu.

Wakaingizwa kwenye moja ya chumba, ambacho kimejaa kila aina ya silaha za mateso, wakavuliwa nguo zote na kubaki kama walivyo zaliwa, huku kazi hiyo ikifanywa na majasusi wa kike wakirussia na marekani.
Wakafungwa miguu juu, vichwa chini. Wakamwagiwa mafuta yanayo teleza kwenye miili yao. Kisha majasisi hao watatu walio kabidhiwa kazi hiyo, kila mmoja akakamata fimbo aina ya mkia wa taa na kukaa tayari kwa kuanza kuwapa mateso Fetty na wezake ili waweze kuzungumza ni nani aliye watuma.

Fimbo hizo zenuye miba miba mikali, kila ilivyo tua kwenye miili yao, kila mmoja alikia kwa uwezo wake, fimbo hizo ziliweza kutoka na nyma kila walipo chapwa. Halima, alioenekana kulia kupita wezake wote, ila hakuwa yayari kuweza kuzungumza kitu cha ania yoyote. Mateso yakazidi kuongezwa, huku vyuma vya moto vikibandikwa mara kadhaa kwenye miili yao, kila walipo ulizwa swali na kuto kujibu, vilizidi kuwapa machungu. Fetty kwenye mawazo yake, mara kwa mara aliweza kumfikiria bwana Rusev, kimoyo moyo akajiapisha kumuua kingozi huyo aliye wageuka kwa mkono wake yeye mwenyewe.
Anna, alikaa kama bubu, machozi yakimtiririka, akiamini kukaa kimya kwake hakuto muingiza matatizoni.
‘Bora waniue kuliko kusema’
Alijisemea kimoyo huku akiyasikilizia maumivu ya pasi, ya moto iliyo bandikwa mgongoni mwake na kumfanya ayakaze meno yake.
***
Makamu wa raisi akaendelea kusonga mbele na watu wake, baada ya kujipumzisha kwa lisaa zima, kwa jinsi ramani waliyo nayo inavyo waonyesha, wakafika kwenye moja ya sehemu walipo kuta mgawanyiko wa njia nne.
“Hii inakwenda Somalia”
Msoma ramani aliweza kuwaonyesha ni wapi kwa kwenda nao bila kipingamizi waafwata. Saa ya makamu wa raisi inamuonyesha ni saa kumi na moja na robo, asubuhi, msoma ramani amewaahidi kama watatembea kwa mwendo huyo huo, hadi saa moja kamili asubuhi watatokea kwenye fukwe za bahari na hapo ndipo wataweza kukutana na mtu waliye ahidiwa kuwapokea.

Wakazidi kusonga mbele, jinsi masaa yalivyo zidi kwenda ndivyo kwa mbali walivyo weza kuuona mwanga ulio ingia kwenye nyia hizo.
“Pale ndipo kwakutokea?”
Makamu wa raisi aliuliza kwa furaha sana
“Ndio?”
“Twendeni twendeni”
Makamu wa raisi akazidi kuongeza mwendo hadi vijana wake wakafurahi, kwani anaoenekana kuwa na hamu kubwa sana ya kuweza kutoka kwenye sehemu hiyo.
“Yaani nawaambia siku nikija kuitia Tanzania mikononi mwangu, basi nyinyi nyote nitawapa vyeo vikubwa”
“Sawa mkuu”
“Ndio lazima nifanye hivyo”
Makamu wa raisi alizungumza huku akihema kama bata mzinga, aliye kimbia kwa umbali mrefu sana. Wakafika kwenye sehemu ya kutoke, wakakuta ngazi ndefu kwenda juu. Kijana mmoja akapanda hadi juu, akafungua mfuniko wa chuma uli funika katika eneo hilo, akachungulia nje, akakuta hakuna mtu katika eneo hilo ambalo kidogo lipo mlimani na bahari inaonekana kwa chini kidogo. Akatoka akiwa na bunduki yake, akawaamrisha wengine kuweza kutoka kwani eneo walilopo ni salama kabisa.
***
Rahab akasimama katika eneo hilo zaidi ya nusu saa, akijaribu kuvuta hisia ni wapi walipo watu wao wanao watafuta. Katika eno alipo simama Rahab kwa chini ndipo zilipo njia nne zilizo gawanyika. Akaweka tena mkono wake chini, alipo simama akatazama mbele na kuona mlima mmoja mrefu, wenye majabali makubwa ambao wanapaswa kuuweza kuupanda.
“Twende tukaupande mlima ule”
“Sawa madam”
Wakaendelea kukimbia hadi wakaufikia mlima, taratibu wakaanza kuupanda mlima huo ulio nyoka mithili ya namba moja. Haikuwa kazi rahisi kwao ila wakajikaza hivyo hivyo kuhakikisha kwamba wanapanda mlima huo kwa juhudi zao zote. Ili wagharimu zaidi ya lisaa na nusu kuweza kufika kileleni mwa mlima huo. Hapo ndio wakaweza kuiona bahari kwa chuni.
“Watakuwa maeneo haya”
Rahab alizungumza huku akiangaza angaza macho yake kila kona, kwa bahati nzuri kwa mbali kidogo anaona mtu akichomoza kichwa chake, kwa haraka wakajibanza kwenye moja ya jabali na kumtazama mtu huyo ni nini atakacho kifanya.

“Bingo”
Rahab alizungumza mara baada ya kumuona mtu huyo akioka huku akiwa na bunduki, wakaanza kutoka mmoja baada ya mwengine hadi wakafikia kumi, wa kumi na moja wakamuona makamu wa raisi waliye kuwa wakimtafuta, wakamshuhudia jinsi anavyo cheke cheka na kufurahia kuuona mwanga wa juu. Wakatoka vijana wengine wawili na kuifanya idadi yao kuwa kumi na mbili. Vijana hao wanaendelea kuimarisha ulizni katika eneo hilo huku wakionekana kama kuna kitu wanacho kisubiria.
“Wanafanyaje?”
Samson aliuliza
“Nahisi kuna kikundi kingine kina kuja kuwachukua si unaona zile boti mbili zinazo kuja kwa kasi katika eneo hili?”
“Si tuwavamie?”
“Ngoja tutazame, mchezo”
Boti mbili hizo za kisasa zilizo tokea kwenye moja ya meli kubwa ya kifahari, zikajongea hadi karibu na nchi kavu. Wakashuka vijana wengine nane, huku mmoja wao akiwa mwanamke aliye valia mavazi meusi pamoja na miwani. Makamu wa raisi akaanza kushuka taratibu na vijana wake, huku wakiendelea kuimarisha ulinzi katika eneo. Wakakutana kati kati na kiongozi ambaye aliweza kuagizwa na Mzee Godwin.
“Karibu sana muheshimiwa, jina langu ninaitwa Madam Merry”

“Ohoo asante sana binti”
Makamu wa raisi alizungumza kwa furaha kubwa, huku akimpa mkono Madam Merry. Kabla hata hawajazungumza chochote, vijana wa makamu wa raisi mmoja baada ya mwengine waakanza kuanguka chini huku wakilia kwa maumivu makali ya risasi zinazo waftwa kama mvua. Vijana wa Madam Merry walipo ona hali imebadilika gafla, wakamchukua kiongozi wao kwa haraka na kurudi naye kwenye boti zao, wakaondoka katika eneo hilo kwa kasi ya ajabu sana.
Makamu wa raisi akazidi kuchanganyikiwa kwani vijana wake walizidi kuteketea kwa risasi zinazo fyatuliwa na Samson pamoja na Rahab. Ambao wanazidi kuwafwata katika eneo walipo.

Ndani ya dakika mbili vijana wote kumi na mbili wa makamu wa raisi wamelala chini, akabaki makamu wa raisi peke yake huku akitetemeka mwili mzima, hadi haja ndogo ikaanza kumwagika.
“Samson mjomba wangu…….”
Makamu wa raisi alizunguza kwa kiwewe huku akimtazama Samson anaye mfwata taratibu sehemu alipo simama
“Aha….. aahaa Samson mjombaaa. Naa naaa naaa kuu kuuu kuaaa”
Makamu wa Raisi alizidi kutetemeka, ila Samson hakuweza kumuonyeshea sura ya furaha. Alicho kifanya Samson ni kumtandika teke moja ya miguu, lililo mrusha juu kiashi na kuanguka chini. Makamu wa raisi alishindwa kujizuida kumwaga machozi, hii ni baada ya kuulalia mkono wake wa kulia vibaya na kuuvunja.
“Usimuue”
Rahab alimzuia Samson asimuue makamu wa raisi, kwani sheria itafwata mkondo wake. Rahab akaiminya batani moja ya saa yake ya mkononi ambayo kwa iliweza kumuonyesha sura ya mume wake.

“Hei baby”
Rahab alizungumza kumstua mume wake anaye onekana kumtumbulia macho kama haamini
“Mke wangu”
“Nimefanikiwa mume wangu, muhalifu tupo naye hapa”
Rahab akaigeuza saa yake, na kuielekezea katika sehemu alipo lala makamu wa raisi, akiwa chini ya ulinzi mkali wa Samson. Watu wote waliopo ndani ya chumba cha mawasilino waliweza kushangilia kwa kazi aliyo ifanya mke wa raisi. Wakawasiliana na majasusi waliopo Kenye, haraka wakaomba ruhussa kuweza kuingia nchini Somalia kumchukua mfungwa wao. Serikali ya Somalia haikuwa na hiyana wakaziruhu helcoptar hizi kuweza kuingia nchini mwao.
Wakafika katika eneo walipo Rahab, wakawachukua wote watatu, huku miili ya marehemu ikibebwa na helcoptar nyingine ya jeshi.

Kukamatwa kwa makamu wa raisi vituo vya televishion, TBC, ITV, STAR TV, CHANEL TEN na kadhalika vikishirikiano na vituo vya redio, vikaonyesha jinsi makamu wa raisi akikabidhiwa na vijana wawili Samson na Rahab, kwa jeshi la polisi pamoja na jeshi la kujenga taifa. Kwa ajili ya kumpeleka katika ngazi za mbele za sheria.
Kwenye mitandao ya kijamii, facebook, twitter, whatsapp, immo, tovuti pamoja na blog za watu mbali mbali ikiwemo www.storizaeddy.blogspot.com ziliweza kuweka vipande vya video pamoja na picha zikimuonyesha makamu wa raisi akiwa mikononi mwa wanajeshi pamoja na askari. Heshima kwa vijana wawili Samson pamoja na mke wa Raisi Praygod, ziliendelea kutolewa na watu mbalimbali serikalini. Huku Rahab akionekana ni shujaa aliye weza kumkamata gaidi ambaye angeachiliwa angeweza kuleta madhara makubwa hapo baadaye.
Raisi Pragod akamtangaza Rahab rasmi kwenye vyombo vya habari kwamba ni mke wake halali, akaadisia historia fupi walipo kutana hadi wakaona. Kila mtanzania aliweza kufurahishwa na mahusiano hayo ambayo watu wengi waliyaita ni zali la mentali.
***
Mwaka mzima ukakatiza Fetty na wezake wakiendelea kusota kwenye gereza kubwa la Guantemana, gereza linalo sifika kukusanya idadi kubwa ya wahalifu walio weza kufanya matukio makubwa sana duniani. Hukumu ya wao kupelekwa Gwantemana kuhukumiwa kifongo cha maisha, nikutokana na wao kutoweza kuzungumza kitu cha aina yoyote kwa serikali ya Marekani.
“Hatuwezi kufia humu ni lazima tutoroke”
Fetty aliwaambia wezake, wakiwa katika meza ya kulia chakula
“Tutatorokaje?”
“Musijali ninayo mipango”
Fetty alizungumza huku akiachia tabasamu pana usoni mwake na kuwafanya Anna na Halima kumkodolea macho
***
“Jack inabidi nirudi Tanzania na wezangu”
“Kina nani?”
“Fetty, Anna na Halima”
Agnes alizungumza mara baada ya kufuzu mafunzo ya uninja, na kukamilika na kuwa mpiganaji hatari sana
“Utawezaje kuwatoa Gwantemana”
“Usijali nina mpango madhubuti”
Agnes alizungumza huku akilichomoa panga lake mngoni na kulishika kikamilifu akiashiria amekamilia kwenda kuifanya kazi hiyo iliyo hatari kupindukia katika maisha yake.


MWISHO
 
 
 
 

  RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 43 & 44 bofya hapa RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 41 & 42 bofya hapa 

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 39 & 40 bofya hapa

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 35 & 36 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 33 & 34 bofya hapa


RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 29 & 30 bofya hapa
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 27 & 28 bofya hapa 


RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 15 & 16 bofya hapa 

  RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 13 & 14 bofa hapa

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 11 & 12 bofya hapa 
RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 9 & 10 bofya hapa

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top