Tetesi za soka Ulaya- leo Jumapili


Manchester United wamewaambia Juventus kuwa wako tayari kulipa pauni milioni 100 kumsajili

Manchester United wamewaambia Juventus kuwa wako tayari kulipa pauni milioni 100 kumsajili kiungo kutoka Ufaransa Paul Pogba, 23, na watampa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki (Mail on Sunday).

Arsenal watampa mkataba mpya Arsene Wenger kwa matumaini ya kumshawishi asiondoke baada ya tetesi kuzagaa kuwa chama cha soka cha England, FA, kinamnyatia (Observer).

Meneja mpya wa Manchester City, Pep Guardiola anataka kumsajili mshambuliaji kutoka Uruguay anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, 29, anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 85, pamoja na kiungo Mjerumani anayechezea Real Madrid, Toni Kroos, 26, ambaye kipengele chake cha uhamisho kina thamani ya pauni milioni 63 (Sunday Mirror).

Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain wamekubali kumsajili kiungo kutoka Poland anayechezea Sevilla Gregorz Krychowiak, 26, kwa pauni milioni 22 (Marca). Pep Guardiola anataka kumsajili mshambuliaji kutoka Uruguay anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, 29

Liverpool watapambana na Everton katika kumsajili kiungo kutoka Ubelgiji Axel Witsel, 27, anayecheza soka Zenith St Petersburg nchini Urusi (Sunday Mirror).

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal, Robin van Persie, 32, huenda akarejea katika ligi kuu ya England baada ya klabu yake ya sasa Fernabahce ya Uturuki kuwaambia West Ham na Crystal Palace kuwa wanaweza kumsajili (Sun on Sunday).

Chelsea wamefanikiwa juhudi za kumsajili beki kutoka Senegal, Kalidou Koulibaly, 25, anayechezea Napoli kwa pauni milioni 30 (Sunday Mirror). Tetesi za soka Ulaya- leo Jumapili

Tottenham wanajiandaa kutoa pauni milioni 38, kumtaka mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi, 23, na tayari wamepeleka wawakilishi wao Italy kuzungumza na mchezaji huyo kutoka Argentina (GianlucaDiMarzio), kipa wa Spurs Hugo Lloris, 29, ananyatiwa na Real Madrid kwa pauni milioni 35 (Sunday Mirror).

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino yuko tayari kumuuza Ryan Mason, 25, kwenda Hull City iliyopanda daraja kwa pauni milioni 10 (Sun on Sunday), kiungo wa Watford Jose Manuel Jurado, 30, amehusishwa na kuhamia Espanyol na kuungana na meneja wake wa zamani Quique Sanchez Flores (Fichajes). Fernabahce ya Uturuki wamewaambia West Ham na Crystal Palace kuwa wanaweza kumsajili Robin van Persie.

Middlesbrough watakamilisha usajili wa pauni milioni 11.75 wa kiungo kutoka Atalanta, Marten de Roon, 25, baada ya kukubaliana maslahi binafsi na mkataba wa miaka minne (Gazette),

Timu nne za EPL zimekuwa zikiwasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Wales, Hal Robson Kanu tangu alipopachika bao dhidi ya Ubelgiji kwenye michuano ya Euro 2016.

Kanu ni mchezaji huru baada ya kuachiliwa na klabu yake ya Reading (Sky Sports).

Stoke huenda wakalazimika kulipa takriban pauni milioni 20 kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22 (Stoke Sentinel).

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
 
 HABARI KUU LEO BOFYA HAPA

CHADEMA Waapa Kutibua Mkutano wa CCM ,Vijana 2000 Kupelekwa Dodoma Kwa Ajili ya Kazi Hiyo Bofya hapa

 Video:Chadema kuzuia Mkutano wa CCM wa kuchagua mwenyekiti wa chama Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

Vibonzo: Katuni tano bora zaidi leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

TFF wajichanganya kwa Muro bofya hapa

Tamko la RC Makonda kuhusu mashoga waliopo jijini Dar es Salaam 


 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top