Rais Dkt Magufuli: AirTanzania kupaa tena Septemba




Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa shirika la ndege la Tanzania litarejea angani ''kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka
huu 2016''.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya ikulu ya Tanzania bw Gerson Msigwa

''Dkt. Magufuli amesema serikali yake imechukua hatua madhubuti za kulifufua shirika la ndege la Taifa.

Tayari mipango imefanywa kuhakikisha ndege mbili aina Bombadier Q400 zinanunuliwa na zitatua hapa nchini kabla ya mwisho wa mwezi Septemba Mwaka huu 2016.'' taarifa hiyo inaeleza.

Tamko hilo ni ishara nzuri kwa sekta ya uchukuzi nchini Tanzania na vilevile kanda nzima ya Afrika Mashariki ambayo imekuwa ikikabiliwa na gharama za juu za usafiri kutoka kwa mashirika ya kigeni.BIASHARA NA RWANDA

Wakati huohuo rais Magufuli aliueleza ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Rwanda kuwa China imeonesha nia ya kushirikiana na Tanzania kujenga reli ya kisasa yaani “Standard Gauge” kwa nia ya kurahisisha uchukuzi wa mizigo kutoka bandari ya Dar es salaam kwa manufaa ya wafanyabiashara. Marais Paul Kagame na mwenyeji wake John Magufuli

''Tanzania imeamua kuipatia Rwanda eneo la kujenga bandari kavu kwa ajili ya mizigo ya wafanyabiashara wake na pia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) itafungua ofisi mjini Kigali nchini Rwanda ikiwa ni juhudi za kurahisisha na kuongeza biashara kati ya nchi hizi mbili.''

Juhudi hizo bw Magufuli anasema ni kuwahakikishia wafanyabiashara wa Rwanda kuwa bandari ya Dar es salaam ni salama kwao kupitisha mizigo na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha bandari hiyo na kurahisisha biashara kati ya nchi hizi mbili.

Kwa upande wake rais Paul Kagame wa Rwanda alitoa wito kwa ''Tanzania na Rwanda pamoja na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana na sekta binafsi katika kutumia fursa nyingi za kibiashara zilizopo baina yake na kuwaletea manufaa wananchi''.

 HABARI KUU LEO BOFYA HAPA

CHADEMA Waapa Kutibua Mkutano wa CCM ,Vijana 2000 Kupelekwa Dodoma Kwa Ajili ya Kazi Hiyo Bofya hapa

 Video:Chadema kuzuia Mkutano wa CCM wa kuchagua mwenyekiti wa chama Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

Vibonzo: Katuni tano bora zaidi leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

TFF wajichanganya kwa Muro bofya hapa

Tamko la RC Makonda kuhusu mashoga waliopo jijini Dar es Salaam 


 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top