NEWS ALERT: RAIS DKT. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA MAENDELEO YA TIB WILLIUM LYAKURWA.

Dkt. John Pombe Joseph Magufuli


Rais Dkt Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, leo tarehe 5 Julai, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIBProf. William Lyakurwa.

Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act) Sura 257, Mhe. Rais amemteua Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, ametengua uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB. Aidha, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act, Sura 257) Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua wajumbe wapya wa Bodi wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu:
                         1. Brig. Gen (Rtd) Mabula Mashauri

2. Dkt. Razack B. Lokina

3. Bi. Rose Aiko

4. Prof. Joseph Bwechweshaija

5. Bw. Said Seif Mzee

6. Dkt. Arnold M. Kihaule

7. Bw. Maduka Paul Kessy

8. Bw. Charles Singili
Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi unaanza tarehe leo 5 Julai, 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam
05 Julai, 2016.


HABARI KUU LEO BOFYA HAPA


















Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top