Leicester yamnasa mshambuliaji wa Nigeria

MABINGWA wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Leicester City wamefanikiwa kumnasa mshambuliaji wa Nigeria, Ahmed Musa anayekipiga katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi.


Ahmed Musa mwenye umri wa miaka 23, aliyejiunga na CSKA mwaka 2012 na kufunga mabao 54 katika mechi 168 anatarajiwa kutia saini kile muda wowote huku taarifa zikieleza kuwa huenda ikawa kitita kikubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa mchezaji katika klabu hiyo.

”Kila kitu kimefanikishwa na Musa atakuwa nchini Uingereza ili kufanyiwa vipimo vya kimatibabu siku ya Jumatano”.

Hivi karibuni, Musa alikataa wito wa Southampton,Everton na West Ham.

Mkufunzi wa CSKA Moscow Leonid Slutsky alikiri kwamba raia huyo wa Nigeria ambaye anaweza kucheza kama winga anakaribia kuondoka katika klabu hiyo.

”Atandoka siku ya Jumanne”, Slutsky alivambia vyombo vya habari vya Urusi.
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
















Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top