Mchezaji wa asili ya DR Congo ajiunga na Chelsea

Michy alifunga dhidi ya Hungary baada ya kuingia nafasi ya Romelu LukakuKlabu ya Chelsea ya Uingereza imemsajili mshambuliaji wa Ubelgiji mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Michy Batshuayi amehamia Chelsea kutoka klabu ya Marseille ya Ufaransa na kutia saini mkataba wa miaka mitano.

Mamake ni Viviane Leya Iseka na babake Pino Batshuayi.

Michy alikuwa na fursa ya kuchezea timu ya taifa ya DR Congo kutokana na asili ya wazazi wake lakini mwaka jana aliamua kuwa mchezaji wa Ubelgiji.

Aliwachezea mechi ya kwanza dhidi ya Cyprus Machi 2015 na kufunga bao.

Michy, 22, ambaye ndiye mchezaji wa kwanza kununuliwa na meneja mpya wa Chelsea Antonio Conte Stamford Bridge, hujulikana kwa jina la utani kama Batsman.

Kakake Aaron Leya Iseka ni mchezaji wa klabu ya Anderlecht ya Ubelgiji.

Chelsea hawakutangaza wazi bei waliyomnunua Michy lakini inaaminika kuwa takriban £33m (euro 40m).

Mshambuliaji huyo, aliyefunga mabao 23 akichezea Marseille msimu uliopita, alifungia Ubelgiji wakati wa ushindi wao hatua ya 16 bora dhidi ya Hungary katika Euro 2016 na pia aliwachezea walipotolewa kwenye michuano hiyo hatua ya robofainali na Wales.

"Nina furaha isiyo na kifani kujiunga na moja ya klabu kubwa Zaidi Ulaya,” alisema Batshuayi.

"[Wachezaji wenzangu Ubelgiji] Eden Hazard na Thibaut Courtois wameniambia mambo mengi mema kuhusu klabu hii, na ikizingatiwa kwamba Antonio Conte anaingia, ni wakati mzuri sana kuwa mchezaji wa Chelsea."
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatatu July 04, 2016  


Vibonzo:Katuni bora zaidi leo Jumatatu July 04, 2016 Bofya hapa 

LOWASSA APIGIWA SALUTI NA WANAJESHI LEO JUMAPILI JULY 03, 2016  Bofya hapa
CHADEMA Waapa Kutibua Mkutano wa CCM ,Vijana 2000 Kupelekwa Dodoma Kwa Ajili ya Kazi Hiyo Bofya hapa 

 Video:Chadema kuzuia Mkutano wa CCM wa kuchagua mwenyekiti wa chama Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa


Vibonzo: Katuni tano bora zaidi leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

TFF wajichanganya kwa Muro bofya hapa

Tamko la RC Makonda kuhusu mashoga waliopo jijini Dar es Salaam 


 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top