Waziri mkuu wa Israeli awasili Uganda

Image captionWaziri mkuu wa Israeli amewasili nchini Uganda katika ziara ya kihistoria

Hali ya usalama imeimarishwa maradufu mjini Kampala na Entebbe Uganda baada ya kutua kwa ndege inayombeba Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Bw Netanyahu ambaye ameandamana na mkewe Sarah anaanzia ziara yake ya siku 5 barani Afrika nchini Uganda.

Netanyahu atazuru uwanja wa ndege wa Entebbe na kukagua gwaride la heshima litakaloandamana na makombora 19 kwa heshma yake.Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Bw Netanyahu atahudhuria sherehe rasmi ya ukumbusho wa mika 40 tangu uvamizi wa uwanja wa ndege wa Entebbe na makomando wa kiyahudi kuwaokoa abiria wa ndege moja wayahudi waliokuwa wametekwa nyara na wanamgambo wa kipalestina .

Ndege hiyo ilikuwa imetoka Israeli ikielekea Ufaransa.

Kwa waziri Netanyahu, hii sio kumbukumbu rasmi ya kitaifa ila ina maana kwake binafsi kwani kakake Yoni, ni mmoja kati ya makomando wayahudi waliouawa katika operesheni hiyo ya kihistoria.Mwenyeji wake rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amewakaribisha viongozi 5 wa mataifa ya Afrika kukutana naye

Kwa Israeli ziara hii inalenga kuimarisha uhusiano wa taifa hilo la kiyahudi.

Mwenyeji wake rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amewakaribisha marais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Paul Kagame wa Rwanda Salva Kiir Mayardit, wa Jamuhuri changa zaidi duniani ya Sudan Kusini Edgar Lungu wa Zambia waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, na waziri wa maswala ya Kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga katika kikao cha faragha kinachotarajiwa kujadili maswala ya ugaidi na Usalama wa taifa ambayo Israeli imeahidi kuyasaidia kukabiliana nayo.Maswala ya ugaidi na usalama wa taifa yatajadiliwa na Israeli imeahidi kuyasaidia kukabiliana nayo.

Duru kutoka Kampala zinaeleza kuwa makomando wa Israeli tayari wameshika doria kote mjini Kampala dakika chache tu kabla ya ndege iliyombeba Waziri Benjamin Netanyahuna ujumbe wake kutua.

Israeli haijakuwa na uhusiano mwema na mataifa ya Afrika ambayo yaliiona kama saliti kwa kushirikiana na serikali dhalimu ya Afrika Kusini iliyokuwa ikiwatesa waafrika weusi.

Aidha mataifa ya Afrika yaliunga mkono jitihada za Uhuru wa wapalestina na hivyo kutenga taifa hilo la Kiyahudi haswa katika miaka ya 60 na 70 harakati za PLO ziliposhika kasi.
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatatu July 04, 2016  


Vibonzo:Katuni bora zaidi leo Jumatatu July 04, 2016 Bofya hapa 

LOWASSA APIGIWA SALUTI NA WANAJESHI LEO JUMAPILI JULY 03, 2016  Bofya hapa
CHADEMA Waapa Kutibua Mkutano wa CCM ,Vijana 2000 Kupelekwa Dodoma Kwa Ajili ya Kazi Hiyo Bofya hapa 

 Video:Chadema kuzuia Mkutano wa CCM wa kuchagua mwenyekiti wa chama Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa


Vibonzo: Katuni tano bora zaidi leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

TFF wajichanganya kwa Muro bofya hapa

Tamko la RC Makonda kuhusu mashoga waliopo jijini Dar es Salaam 


 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top