FERGUSON AUNGA NA MOURINHO KUMSALITI GIGGS UNITED


Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametetea uamuzi wa Jose Mourinho kutomjumuisha Ryan Giggs kwenye timu yake ya benchi la ufundi
la klabu hiyo.

Giggs, ambaye ni mchezaji aliyedumu United kwa kipindi kirefu zaidi, na aliyekuwa meneja msaidizi wa Louis van Gaal, ametangaza kuondoka Old Trafford mwishoni mwa wiki hii, na kukamilisha miaka yake 29 aliyodumu klabuni hapo kama kocha na mchezaji.

Ferguson anaamini kwamba Mourinho alikuwa sahihi kabisa kumleta msaidizi wake anayemwamini kwa kiasi kikubwa Rui Fara, ambaye amekuwa akifanya naye kazi kokote aendapo.

“Unatakiwa uwe na msaidizi wako ambaye umekuwa ukimwamini kwenye maisha yako yote,” Ferguson amesema.

“Wakati nilipokuja Man United, nilimleta Archie Knox, kwasabau alikuwa mtu mwenye thamani sana kwangu.

“Nilimwamini kwa asilimia 100, Jose Mourinho amekuwa na msaidizi wake kwa miaka nenda-rudi, kitu ambacho ni kizuri kwake kwa kudumu na mtu mmoja.

Kama Jose asingekuwa na msaidizi, nafahamu fika kwamba angemchukua Ryan.

“Ni muda mwafaka sasa kwa Ryan kusimama mwenyewe, aondoke pale na kutafuta changamoto mpya.

Ferguson,ambaye alistaafu kuifundisha United mwaka 2013 baada ya kudumu kwa miaka 26, amesema Giggs ana kila sababu ya kutafuta timu kubwa na kuweza kuifundisha kwa sababu anao uwezo.

“Nadhani kwa sasa ameshakuwa tayari kuweza kufundisha timu yoyote na kimsingi ana ubora wote unaostahili,” Ferguson aliongeza.

“Hatakiwi kwenda kwenye klabu ambayo inafukuza makocha kila baada ya dakika mbili.” alimalizia.


HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
















Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top