MARA 7 CHELSEA WALIPOINGILIA MADILI YA WATU


Chelsea wamefanikiwa kumnyakua Mitchy Batshuayi kutoka mikononi mwa klabu nyingi za EPL ambazo ziikuwa zinamtaka, lakini hii si mara ya kwanza
kwa Chelsea kufanya kitu kama hiki.

ARJEN ROBBEN 2004


“Old trafford ndiyo sehemu pekee ambayo anataka kucheza na kama hawezi kucheza huko basi bora abaki PSV, tena bora acheze timu ya vijana kuliko kwenda Chelsea. Mtoto wangu hatoenda Chelsea, labda niwe mfu ndiyo ataenda huko.” Haya yalikuwa maneno ya baba yake Robben ambaye bado yuko hai mpaka sasahivi. Robben alipanda ndege kwenda kumuona Ferguson mwaka 2004 na kama baba yake, Robben alifurahi sana na alichokiona. “Ntakuwa na furaha sana kama nikichezea Manchester United.” Alisema winga huyu ambaye kwa wakati huo alikuwa na miaka 19 tu.

PSV walikasirishwa na Robben kukutana na United kwa sababu kitendo cha Chelsea kujiweka kwenye kinyanganyiro cha saini ya Robben kilibadilisha mambo kidogo. Dau la Chelsea lilikuwa kubwa sana na kama maajabu vile Robben alisajiliwa na Chelsea ambapo aliweza kuisaidia klabu hiyo kutwaa mataji mawili ya Ligi kabla ya kujiunga na Real Madrid. “Hatoenda Real”, alisema baba ake Robben miaka kadhaa kabla. “Kwanza hiyo Real yenyewe haipendi, nilivyokuwa naye likizo Spain alikuwa anaipenda Barcelona.” Hakika baba yake Robben anatakiwa aachane na fani ya Utabiri.

JOHN OBI MIKEL 2006


Hili ndiyo baba la mabishano yote ya usajili kati ya klabu ya Chelsea na Mancheter United. Safari hii Man United waliamini kwamba walikuwa na dili ambalo tayari lishawekwa kwenye wino. Mwenyekiti wa Man United David Gill hata aliongea na Mancheter United Tv huku ameshika mkataba. Mambo hayakuwa hivyo lakini kwani wakati Man Utd walikuwa wameweka makubaliano na Mikel pamoja na klabu yake ya Norway Lyn Oslo, Chelsea wao kwa wakati huohuo walikuwa wamekubaliana na Mikel pamoja na watu wake.

Man Utd na Lyn Oslo walikasirishwa na kitendo hiki lakini Chelsea wao wakasema kwamba walimsaidia Mikel kuhamia Uingereza kutokea Nigeria huko zamani na walikubaliana kumsajili huko baadaye. Mikel alifanya hata mazoezi na klabu ya Chelsea miaka miwili kabla lakini alifanyiwa majaribio na klabu ya Man Utd vilevile.

Wakati Sir Alex Ferguson akiwa anafikiria kwenda Norway ili kutatua swala hili, Mikel alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha na akasafiri kwenda mjini London kabla ya kutangaza kwenye vyombo vya habari kwamba yeye alitaka asajiliwe Chelsea.

United walikubali matokeo baada ya ubishani wa mda mefu na wakakubali kifutia machozi cha paundi millioni 12 kutoka kwa klabu ya Chelsea ili kuvunja mkataba wao na Mikel. The Blues pia waliilipa klabu ya Lyn Oslo million 4 tu kama dau la usajili.

FLORENT MALOUDA 2007


Liverpool walionekana kuwa mstari wa mbele kabisa kumsajili Malouda mwaka 2007 lakini hawakufikiria swala moja: Malouda hakutaka kwenda Liverpool. “Benitez alinipigia mara nyingi na ni mtu mwema sana na kocha mzuri lakini hakuweza kunishawishi nijiunge na klabu yake.”

Klabu ambayo Malouda alikuwa akitaka kujiunga nayo ilikuwa Chelsea kwa sababu huko ndipo alipokuwa anacheza mchezaji mwenzake wa zamani kwenye timu ya Guingamp Didier Drogba. “Alikuwa ananisumbua nijiunge nae tangu siku ya kwanza kabisa alipoichezea Chelsea,” Malouda alisema. Tatizo ni kwamba Chelsea walikuwa bado hawajafikia makubaliano na klabu ya Lyon.

Malouda alikuwa tayari kusubiria lakini wiki kadhaa baadae Chelsea walifikia makubaliono ya dau la paundi millioni 13.5 kumleta Malouda Stamford Bridge. Benitez baadaye alikuja kuwa kocha wa mwisho wa Malouda Chelsea na hakumchezesha hata mara moja lakini kiukweli kiwango cha Malouda kilikuwa kishakwisha hadi hapo. Malouda sasa hivi yuko kwenye mazumgumzo ya kujiunga na klabu ya Delhi Dynamos nchini India.

NICOLAS ANELKA 2008


Manchester United imeona madili yake mengi yakiharibiwa na klabu ya Chelsea dakika za mwisho, na hivi ndio ilivyokuwa kwa Nicolas Anelka Januari 2008. Mfaransa huyu alikuwa akitakiwa na vilabu vingi akitokea Bolton na ilionekana kama Man Utd ndio ilikuwa klabu yake inayofuata.

Anelka aliwaambia wafanyakazi Bolton kwamba alikuwa anaelekea United ndani ya siku kadhaa zinazofuata, hakika wafanyakazi hao walishangaa walipomwona Anelka akivaa uzi wa Chelsea kwa dau la Paundi million 15 siku kadhaa zilizofuata.

Lakini United ndiyo waliobaki wanacheka kwani Anelka alikosa penati ya mwisho ya Chelsea timu hizi mbili zilipokutana kwenye fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya mwaka huo. Anelka alimlaumu kocha Avram Grant kwa kumuweka Winga.”Niliombwa nipige penati moja kati ya tano za mwanzo, lakini nikasema siwezi kufanya hivyo kwani yeye ameniweka kwenye hii mechi kama beki wa kulia.”

JUAN MATA 2011


Safari hii ilikuwa Arsenal waliobaki wanalia. The Gunners walianza kwa dau la paundi Millioni 15 kwa Mata na mwezi mmoja baadae wakaongeza adi kufikia Million 18, dau ambalo lingevunja rekodi ya Arsenal ya paundi million 12 iliyomleta Andrey Arshavin uwanja wa Emirates. Valencia walikataa dau lao kabla ya kumuuza Mata kwa Chelsea kwa dau la Paundi million 23.5 wiki tatu baadae. Mata aliwasaidia Chelsea kushinda ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2012 na alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Chelsea mara mbili kabla ya kuuzwa kwa klabu ya Manchester United kwa dau la million 37.1, Chelsea wakipata faida

WILLIAN 2013


Ilisemekana kuwa yalibaki masaa tu kwa klabu ya Tottenham kutangaza usajili wao wa mbrazil huyu kwa dau la Paundi million 30 August 2013. Willian alifanyiwa hata vipimo na klabu ya Tottenham. Willian alikubaliana mshahara na alikuwa akijiandaa kuwa tegemezi wa klabu ya Tottenham kwa sababu usajili wa Gareth Bale kwenda Madrid ulikuwa unakaribia kukamilika.

Roman Abrahamovich akaingilia dakika za mwisho. Chelsea walikubaliana na klabu ya Willian kwa haraka sana na mchezaji huyo akapanda pipa kuelekea London.

“Hilo ndiyo tatizo la kufanya vipimo kabla ya kusaini mkataba, bora ufanye vipimo kwa siri tu.” alisema Jose Mourinho huku akioneshwa kufurahishwa kidogo na swala hili kwa sababu alikuwa amempiku msaidizi wake wa zamani Andre Villas Boas kumpata mchezaji huyu.

Mzogo huu ulizua hata nyimbo mpya ya mashabiki wa Chelsea ambayo wanaitumia kuwatania Tottenham kila wanapokutana.

MOHAMMED SALAH 2014


Kwa wakati ule ilionekana kuwa ni wazo zuri sana kwa Chelsea kumnyakua winga huyu mwenye Spidi kutoka mikononi mwa Liverpool Januari 2014.

Liverpool walikuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Salah FC Basel kwa wiki nyingi na ilionekana kuwa ni kitu cha uhakika kabisa Salah kutua Merseyside.

“Yalikuwa majadiliano marefu na mazuri na Liverpool ila yalichelewa kwa miezi miwili na nusu.” Alisema mzungumzaji wa Salah ambaye ana jina linalofurahisha la Sascha Embacher. “Klabu zote mbili zilishindwa kukubaliana vizuri na Chelsea walipoipigia simu Basel, alifurahi na akachukua nafasi yake, halikuwa swala la hela.”

Lakini hakika Chelsea wamebaki wakijiuliza hata kwanini walijisumbua. Salah aliichezea Chelsea mara 19 tu kabla ya kupelekwa kwa mkopo klabu ya Fiorentina na kwa sasa yuko Roma kwa mkopo mwingine.
Credit:Dauda
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
















Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top