Bwawa Nyumba ya Mungu Lafungwa kwa Miezi 12

SERIKALI za mikoa ya Kilimanjaro na Manyara zimelifunga Bwawa la Nyumba ya Mungu kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kuepusha kutoweka kwa viumbe hai wakiwamo samaki kutokana na kushamiri kwa uvuvi haramu.


Aidha, wakuu wa wilaya za Moshi, Mwanga na Simanjiro wametakiwa kusimamia maamuzi hayo na kuchukua hatua kali za kisheria kwa watakaokaidi agizo hilo.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadiki alisema hayo wakati wa hafla maalumu ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya mkoani Kilimanjaro iliyofanyika mjini Moshi, juzi.


Alisema uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha ujirani mwema baina ya mikoa hiyo kupitia wilaya tatu zinazolizunguka bwawa hilo na kwamba utekelezaji wa agizo hilo umeanza rasmi Julai Mosi mwaka huu.


“Hali ya uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ni mbaya sana, mazingira yameharibiwa, kuna athari nyingi zinajitokeza ikiwamo ya kupungua kwa maji katika bwawa hilo na hii huenda ikaathiri uzalishaji umeme na kutoweka kwa viumbe hai....kama serikali hatuwezi kuvumilia tena,” alisema Sadiki.


Pamoja na bwawa hilo, Sadiki alitaka wakuu wa wilaya kusimamia agizo la Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), kupiga marufuku misumeno ya mnyororo, kwani imebaini ni adui mkubwa wa misitu.


Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa aliwakabidhi wakuu hao wa wilaya migogoro mikubwa mitano iliyopo katika hatua mbalimbali za utatuzi wake kupitia viongozi waliowatangulia na kutaka kufuata sheria katika kuishughulikia.


Miongoni mwa migogoro aliyoitaja ni unaohusisha jamii ya wafugaji wanaozunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kampuni inayohudumia uwanja huo ya KADCO kuhusu umiliki wa eneo la ardhi.


Mgogoro mwingine ni wananchi wa wilaya ya Longido mkoani Arusha na mwekezaji wa eneo la utalii la Ndarakwai uliowahi kusababisha kuchomwa moto kwa eneo hilo.
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatatu July 04, 2016  


Vibonzo:Katuni bora zaidi leo Jumatatu July 04, 2016 Bofya hapa 

LOWASSA APIGIWA SALUTI NA WANAJESHI LEO JUMAPILI JULY 03, 2016  Bofya hapa
CHADEMA Waapa Kutibua Mkutano wa CCM ,Vijana 2000 Kupelekwa Dodoma Kwa Ajili ya Kazi Hiyo Bofya hapa 

 Video:Chadema kuzuia Mkutano wa CCM wa kuchagua mwenyekiti wa chama Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

Vibonzo: Katuni tano bora zaidi leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

TFF wajichanganya kwa Muro bofya hapa

Tamko la RC Makonda kuhusu mashoga waliopo jijini Dar es Salaam 


 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top