UVCCM Yawapa Onyo Kali Vijana wa CHADEMA Walioandaliwa Kuvuruga Mkutano wa CCM Dodoma


Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) umeingia katika mvutano mkubwa na Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kuhusu Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho tawala uliopangwa kufanyika Julai 23 mwaka
huu mjini Dodoma.


UVCCM wameionya BAVICHA kuhusu mpango wao wa kutaka kukusanyika mjini Dodoma siku hiyo kwa lengo la kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa unakiuka amri halali ya polisi ya kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano yote ya kisiasa nchini.


Onyo hiyo limetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamda Shaka ambaye aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa watawakabili kwa nguvu zote BAVICHA endapo wataamua kuendesha siasa zinazolenga kuvuruga amani na kuleta hofu katika jamii na kutishia maisha.


Alisema umoja huo hautaona shaka kutumia mbinu zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau miongo kadhaa iliyopita nchini Kenya.


“Hatutaona muhali kupita njia zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau wa Kenya ili kukihami chama, kulinda viongozi wake na kupigania hadhi na heshima yetu,” alisema Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM.


CCM inatarajia kufanya mkutano mkuu maalum Julai 23 mwaka huu ambapo Rais John Magufuli atakabidhiwa rasmi uenyekiti wa chama hicho kutoka kwa mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete.


Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatatu July 04, 2016  


Vibonzo:Katuni bora zaidi leo Jumatatu July 04, 2016 Bofya hapa 

LOWASSA APIGIWA SALUTI NA WANAJESHI LEO JUMAPILI JULY 03, 2016  Bofya hapa
CHADEMA Waapa Kutibua Mkutano wa CCM ,Vijana 2000 Kupelekwa Dodoma Kwa Ajili ya Kazi Hiyo Bofya hapa 

 Video:Chadema kuzuia Mkutano wa CCM wa kuchagua mwenyekiti wa chama Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

Vibonzo: Katuni tano bora zaidi leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

TFF wajichanganya kwa Muro bofya hapa

Tamko la RC Makonda kuhusu mashoga waliopo jijini Dar es Salaam 


 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top