URENO NA REKODI ZA EURO 2016


Nusu fainali ya kwanza ya michuano ya 15 ya kusaka taifa bingwa la soka barani Ulaya, EURO 2016, imefanyika hapo jana na kushuhudia Ureno wakitangulia fainali baada ya kuwafunga Wales 2-0.

Mabao ya haraka haraka ya dakika 50 (Cristiano Ronaldo) na dakika 53 (Luis Nani) yalitosha kuiangamiza Wales ya Gareth Bale.

Bao la Ronaldo limemfanya afikishe mabao 9 kwenye fainali za Euro na kuikamata rekodi ya gwiji wa Ufaransa, Michel Platini, aliyoiweka 1984. Hata hivyo, Platini alifunga mabao hayo kwenye fainali moja tu za 1984…Ronaldo amefunga katika fainali nne.

Hii ni rekodi ya pili kwa Ronaldo mwaka huu. Rekodi ya kwanza ilikuwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye fainali nne mfululizo za Euro, akianzia 2004.

Lakini ukiacha rekodi hiyo binafsi kwa Ronaldo, timu yake nayo imeweka rekodi za aina yake mwaka huu.
Wamefika fainali kiujanja ujanja.

-Mpaka wanamaliza hatua ya makundi walikuwa hawajashinda hata mchezo mmoja. Ni mfumo tu wa mashindano ya mwaka huu ndiyo uliwapa nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora, kupitia mlango wa nyuma.

-Mechi ya yao katika hatua ya16 bora ilishuhudia dakika 90 zikiisha kwa sare. Bao la ushindi likapatikana dakika ya 117, dakika tatu kabla ya dakika za nyongeza kumalizika.

-Robo fainali wakaitoa Poland kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya 1-1 dakika 120. Kwenye kumbukumbu za UEFA na hata FIFA, mechi iliyoamuliwa kwa penati za baada ya dakika 120, huhesabiwa iliisha kwa sare.

-Ushindi wa kwanza katika muda wa kawaida wameupata kwenye nusu fainali.

Mara ya mwisho timu kutinga fainali kiujanja ujanja namna hii, ilikuwa Italia kwenye kombe la dunia 1982…mwisho wa siku wakawa mabingwa.
Wametoa mchezaji bora wa mchezo katika kila mechi.

(a) Luis Mani vs Iceland
(b) Joao Moutinho vs Austria
(c) Cristiano Ronaldo vs Hungary
(d) Renato Sanches vs Croatia
(e) Renato Sanches vs Poland
(f) Cristiano Ronaldo vs Wales
Wamepata ushindi katika muda wote wa mchezo.

(a) Dakika 90 vs Wales
(b) Dakika 120 vs Croatia
(c) Changamoto ya mikwaju ya penati vs Poland
Wametoa sare za aina zote.

(a) bila kufungana vs Austria
(b) kufungana mabao mengi vs Hungary
(c) Kuanza kufunga halafu wapinzani kusawazisha vs Iceland
(d) Wapinzani kuanza kufunga halafu wao kusawazisha vs Poland

Tusubiri muujiza wa fainali July 10, 2016
Breaking News : Orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri na Majiji walioteuliwa leo na Rais Magufuli bofya hapa

 
 

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top