Ufaransa yatinga fainali, Ujerumani nje





Wachezaji wa Ufaransa wakishangilia ushindi

Ufaransa imetinga katika hatua fainali ya Kombe la Mataifa barani Ulaya kwa mwaka huu 2016 baada ya kuifunga
Ujerumani 2 - 0.

Mshambuliaji Antoine Griezmann ndiye aliyeipeleka timu yake ya Ufaransa katika hatua fainali ya Kombe la Mataifa barani Ulaya kwa mwaka huu baada ya kuifungia magoli 2 na kuishangaza Ujerumani iliyokuwa imetawala mchezo huo wa nusu fainali.

Mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid alianza kwa kuandika bao la kwanza kwa njia ya penalti katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza kabla ya kupachika bao la pili na ushindi kipindi cha pili baada ya golikipa wa Ujerumani Manuel Neuer kufanya makosa golini.
(MAAMUZI YA TTF KUHUSU SAKATA LA JERRY MURO bofya hapa)
Kwa matokeo hayo sasa Ufaransa mwenyeji wa michuano hiyo itakutana na Ureno katika mechi ya fainali siku ya Jumapili.

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top