Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jana imezifungua ofisi za Kampuni maarufu ya uwakili ya Mbunge wa Butiama, Nimrod Mkono, ikiwa ni siku chache baada ya kuzifungia kwa madai kuwa kampuni hiyo inadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.
TRA waliwasili katika jengo la ofisi hizo zilizoko katika jengo la Bank ya Exim iliyoko jijini Dar es Salaam (ingawa ilikuwa sikukuu), pamoja na Kampuni ya udalali ya Yono na kuzifungua ofisi hizo mbele ya Nimrod Mkono na binti yake.
Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amekiri kufunguliwa kwa ofisi hizo. Kayombo amesema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuwepo kwa makubaliano kati ya pande mbili na ahadi ya kufanya malipo iliyowekwa na mkono.
“Ni kweli muda upo tuliokubaliana lakini hatutaki uwe katika vyombo vya habari, kutokana na nia ya dhati aliyoonesha Mkono ndio maana tumekubaliana nae,” Kayombo anakaririwa.
Hatua hiyo imefikiwa huku kukiwa na taarifa kuwa ingawa Mkono amefungiwa ofisi zake akidaiwa kodi ya shilingi bilioni 1, yeye anaidai Serikali takribani shilingi bilioni 9 kwa kazi alizofanya ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa July 08, 2016 bofya hapa
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA ahojiwa na Jeshi la Polisi Dar Bofya hapa
News alert: Ureno yatinga fainali kwa kuindoa Wales Bofya hapa
Yanga yapata pigo jingine tena Deus Kiseke apata ajali ya pikipiki Bofya hapa
Kocha Mkuu wa Yanga asema bado Yanga iko vizuri bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA