RONALDO AIFIKIA REKODI YA MFUNGAJI WA MUDA WOTE MICHUANO YA EURO



Cristiano Ronaldo inawezekana hafanyi vizuri kwenye michuano ya Euro 2016, lakini licha ya kutocheza katika kiwango chake kinachotarajiwa
, bado anauwezo wa kutengeneza na kuvunja rekodi.

Kuvunja rekodi imekuwa ni sehemu ya maisha ya ronaldo, mara kadhaa amefanya hivyo kwenye klabu yake ya Real Madrid, baada ya goli lake la kichwa dhidi ya Wales amefanikiwa pia kufikia rekodi iliyowekwa na Michel Platini miaka kibao iliyopita.

Ronaldo aliruka juu mithili ya mcheza kikapu Lebron James na kukutana na krosi ya Gueirrero kisha kuuzamisha mpira kambani.


Goli hilo liliipa Ureno uongozi wa goli 1-0 dhidi ya Wales kwenye mchezo wa nusu fainali ya Euro 2016 na kumfanya Ronaldo awe sambamba na rekodi ya legend wa Ufaransa Michel Platini ya kufunga magoli magoli 9 kwenye michuano ya Mataifa ya Ulaya.

Ronaldo alifunga goli lake la kwanza kwenye michuano ya Euro mwaka 2004.

Anahitaji goli moja ili kuwa mfungaji wa muda wote kwenye michuano ya Euro.

Video&Ubunifu:Adam wa Adam Auto Garage wa Tunduma aunda Helkopita huyu ni Mtanzania mwezetu, Kumbe inawezekana angalia ilivyo anasitahili kupongezwa bofya hapa kuona
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top