KWANINI YANGA HAWAVAI JEZI ZENYE NEMBO YA KILIMANJARO? MANJI AMETOA MSIMAMO MPYA

Mkataba wa kampuni ya bia nchini (TBL) na YANGA ulisainiwa miaka mitano iliyopita na mtangulizi wangu. Huu ulikuwa mkataba haramu kwani mamlaka ya kutia saini mikataba kwa mujibu wa Katiba ya Yanga yapo kwa wadhamini na hapana kitu kama azimio kutoka bodi ya wadhamini kuingia katika makubaliano kama haya, au mkataba kusainiwa na wadhamini.

Wakati wa kipindi changu kilichopita, nilijitahidi kurekebisha tofauti zote zilizokuwepo, lakini nilishindwa. TBL ni mara moja tu imetoa mara moja tu Sh. 20 Millioni kwa ajili ya tamasha la Yanga Day zilizoahidiwa kutolewa kila mwaka, haijailipa klabu fedha ya marekebisho inayofikia Sh. 30 Milioni wala haijatupa basi kwa kiwango sahihi tulichotaka kama ililoahidi katika mkataba. TBL imejulishwa kuhusu hili lakini haijalishughulikia.

Yanga imeingia katika mkataba wa masoko na kampuni ya International Marketing ili kupata wafadhili wake, ili kupunguza pengo la TBL kwa ajili ya mishahara ya Juni. Hii ni kampuni ambayo nilikuwa mwenyekiti wake na ikakubali ufadhili huo wa mwezi mmoja, jambo ambalo liliifanya Yanga kuvaa jezi za nembo yake katika mchezo dhidi ya TP Mazambe.

Iwapo wanachama wa Yanga wakihisi nilivunja katiba kwa maslahi yangu binafsi au wakiwa na sehemu nyingine bora zaidi ya kufanya hivyo, walifikishe suala hilo kwenye kamati ya maadili ya klabu kwa ajili ya uamuzi.

MUHTASARI

Nimechaguliwa katika mazingira ya amani zaidi miongoni mwa vyama vya soka nchini na ambapo hakuna hata senti moja ilitumika kwa ajili ya kumhonga yeyote.

Nilisimama bila kupingwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti na nikawaambia wapiga kura wangu waziwazi kwamba: Wakati huu nikiwa Mwenyekiti sitakaa kimya kwa wale watakaojikita katika kuhujumu masuala ya fedha klabuni na wale wanaoamini kwamba TFF iko juu ya sheria zinazohusu masuala ya biashara na haihusiki na Katiba ya Tanzania. Nawashukuru wapiga kura wangu ambao walinipigia kura kwa asilimia 100 ya ushindi wangu.

Masuala yanayotokea uwanjani au usajili wa wachezaji ni ya soka na kwamba TFF ina mamlaka ya kuipeleka mbele nchi yetu kwa kufuata miongozo ya FIFA. Lakini sitavumilia upuuzi wa TFF kutaka kuingilia masuala ya Yanga. Tunajua FIFA imechafuka kwa rushwa na kusababisha Sepp Blatter kuong’olewa na kukabiliwa na mashitaka: hata hivyo, iwapo tungetumia kauli za TFF, Blatter na Platini wasingefanywa chochote.

Masuala ya fedha ya klabu yetu, yawe kuhusu nembo ya klabu kwenye kituo cha televisheni bila ya kibali cha Yanga si ya kuamuliwa na TFF. Kilichopo ni kwamba kitu cha televisheni kinatengeneza fedha kutoka kwa Yanga, TFF inatengeneza fedha kutoka kituo cha televisheni. Hivyo, iwapo kuna mtu anafikiri sijui sheria za mashindano bora ya kibiashara na hakimiliki, basi wajue hilo litawagharimu.

Iwapo TFF inataka Mwenyekiti wa Yanga akubaliane na uwongo, basi katika miaka minne ijayo niko tayari kupambana na uovu huo na kusahihisha kila kitu. Hata hivyo, kwanza kabisa niko tayari kushirikiana kirafiki na wakati huohuo kupigania haki za klabu kwani daima nimekuwa mtu mwenye kupigania haki na masuala ya kikanuni ninayoyaamini ni ya kiadilifu.

Yanga ilikuwepo kabla yangu na itakuwapo baada yangu. Ni wajibu wangu kuiacha Yanga ikiwa klabu bora zaidi kuliko nilivyoikuta na nikiona siwezi tena kutumikia maslahi ya wanachama wake, sitasita kujiuzulu au kuitisha uchaguzi ili kujipanga upya.

MWISHO:

Kwa mashabiki wa soka wa Yanga na Tanzania nzima, tumefikia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho si kwa bahati. Mwaka jana tulitolewa kwa tofauti ya mabao ya kufunga. Na mwaka huu tumekutana na uhasama katika mechi zetu ambapo tulipigwa mabomu ya machozi, mbali na huko Misri ambako tulifanyiwa njama mbalimbali. Vilevile TFF nayo imekuwa haitupi msaada wowote bali kutuhujumu tena. Nasema sitavumilia hujuma hizi dhidi ya Yanga.

Sisi ni klabu ambayo tumejaa ujasiri, hatujalipiza kisasi kwa tulichofanyiwa wapinzani wetu wakija hapa. Ndiyo, tumeshindwa mechi mbili, lakini kwa heshima.

Hatutashusha vichwa vyetu kwa aibu au kutaka kufanikisha mambo yetu kwa njia za panya. Tutawekeza katika timu yetu kila raslimali.

Natoa wito kwa Yanga kutokata tama katika juhudi za kujenga uwanja wetu juu ya misingi aliyoiacha Mzee Karume.

Tusisahau kwamba tulikuwa msingi wa nguvu zilizomfanya Mwalimu Nyerere kuikomboa Tanzania na nchi nyingi za Afrika.

Historia yetu imejaa kila aina ya fahari.

Tumepigania yote tuliyoyaamini na tumeshinda.

Matumaini yetu ya kutwaa kombe la ushindi wa ubingwa katika Afrika yako karibu na kwamba kila hatua tufanyayo inatupeleka karibu na lengo hilo.

Mustakabali wetu unatuonyesha kwamba kama si mwaka huu, basi mnamo miaka mitatu ijayo tutafika katika fainali za michuano hii tukishirikiana vyema.

Ni kweli wasaliti wapo, lakini lazima tusonge mbele, kila tunapokatishwa na tama na watu wengine, basi tujue tunakaribia ushindi wetu.

Nataka kila mtu aamini kwamba hii ni timu yake si yangu mimi. Tunamtaka zaidi kila mtu hivi sasa kwani tunakaribia katika lengo letu la kutwaa ubingwa wa Afrika, japokuwa tunafahamu kwamba kuna mengi ya kufanya lakini mengi zaidi tumeishamaliza, kikubwa matunda yanaonekana na tunashiriki michuano ya kimataifa tunashiriki na tunapiga hatua moja mbele.

Si rahisi lakini tusilalamike. Hakuna kitu Mungu anatuwekea mbele yetu bila ya sisi kuwa na nguvu ya kuvuka. Kwa imani, DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO.


 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
 
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top