Afisa habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro
Baada ya Ofisa wa habari wa Yanga, Jerry Muro kuitwa mbele ya kamati kujibu tuhuma za kupingana na maamuzi pamoja na kuishambulia TFF kwenye vyombo vya habari, Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji ameandika waraka ambao sehemu ya waraka huo unasema, Yanga haitakubali Mkurugenzi wake wa Habari afungiwe kushiriki katika shughuli za soka.
Hati za TFF za kuitwa kwa Jerry Murro hazionyeshi wazi sababu ya Mkurugenzi wa Habari huyo wa Yanga kutakiwa kufanya hivyo ambapo atakuwa akihudhuria si kwa cheo chake katika klabu, lakini ifahamike wazi kwamba Yanga haitakubali Mkurugenzi wake wa Habari afungiwe kushiriki katika shughuli za soka. Tukiwa kama klabu tuko tayari hata kuunga mkono hatua zozote za kisheria dhidi ya TFF na iwapo TFF itajaribu kuifungia Yanga, tutalichukua suala hili hadi katika vyombo vya juu zaidi vya michezo.
Hata hivyo, iwapo kuitwa huko kunahusu suala la faini ya Sh. 5 Milioni dhidi ya Jerry, fedha hiyo ilikwishatolewa kwa TFF.
Wanaokula njama ndani ya TFF kuwanyamazisha au kuwafungia ambao wanaeleza mawazo yao kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, lazima wafahamu kwamba kuikosoa TFF hakupingani na sheria, na wafahamu pia kwamba Yanga chini ya uenyekiti wangu haitakubali wanachama au wafanyakazi wa klabu kudhalilishwa au kutishwa.

Credit:Dauda
Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa
Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA