Video: Wales kucheza na Ureno .......BALE, RONALDO, USO KWA USO NUSU FAINALI EURO 2016



Wales
Wales wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano mikubwa kwa mara ya kwanza baada ya kutoka nyuma na kuichapa Ubelgiji kwenye robo
fainali ya michuano ya Ulaya.

Radja Nainggolan aliitanguliza mbele Ubelgiji kwa bao lake la mkwaju wa mita 25 lakini nahodha wa Wales Ashley Williams aliifungia timu yake bao la kusawazisha kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliokuwa wa mchakamchaka mwanzo mwisho.

Sherehe za Wales zilipamba moto wakati Hal Robson-Kanu striker asiye na timu alipoipa Wales bao la kuongoza.

Baada ya presha kubwa iliyokuwa ikiletwa na Ubelgiji, Wales wakapachika bao jingine kupitia kwa Sam Vokes aliyeingia kutokea benchi na kuhakikishia timu yake kucheza nusu fainali dhidi ya Ureno mchezo unaotarajiwa kuwa ni wa kufa au kupona kwa Gareth Bale na Cristiano Ronaldo nyota wawili wanaokipiga Real Madrid wakikutana kwenye mataifa tofauti.

Kocha wa Wales Chris Coleman alisema, hatua ya robo fainali kwa Wales ni mafanikio makubwa sana tangu mwaka 1958 walipofanikiwa kufika hatua ya robo fainali ya kombe la dunia na kuchapwa na Brazil lakini mara zote wamekuwa wakiishia njiani kabla ya robo fainali.

Vijana wake walipambana kwa kujitoa kutoka nyuma na kuibuka washindi kitu ambacho kinachofanya ushindi huo kuwa wa aina yake kwenye soka la Wales.

Ranked second in the world, Belgium were strong favourites and under pressure to deliver with a prodigiously talented generation of players.

Wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa viwango vya FIFA, Ubelgiji walikuwa wanapewa nafasi kubwa kutokana na kikosi chao kusheheni nyota wengi wenye majina makubwa kwenye soka la Ulaya ukilinganisha na Wales.

Video ya magoli yote Wales vs Belgium

Credit:Dauda 



 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top