Ujerumani yatinga nusu fainali baada ya kuifunga Italia



Baada ya kujaribu kwa takribani mara 9 hatimaye usiku wa leo timu ya taifa ya Ujerumani imefanikiwa kuwafunga Italy katika mashindano makubwa
na kufanikiqa kusonga mbele hadi nusu fainali ya michuano ya Euro 2016. 
 Timu hizo zilikwenda sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 na ilipofika hatua ya mikwaju ya penalti Ujerumani wakashinda 6-5.
Miamba hiyo ya soka barani Ulaya ililazimika kwenda hadi penalti ya tisa ndipo mshindi alipopatikana kwa Italia kupoteza jumla ya penalti nne huku Ujerumani wakipoteza tatu.
Ujerumani walipata bao la kuongoza dakika ya 65 kupitia kwa Mesut Ozil lakini Leonardo Bonucci akaisawazishia Italia kwa njia ya penalti dakika ya 78.

Mchezo huu umeweka rekodi ya kuwa na mikwaju mingi ya penati zaidi katika kipindi cha miaka 36, zimepigwa jumla ya penati 18 – mara ya mwisho kwa mchezo wa Euro kuamuliwa na idadi kama hii ya penati ilikuwa mwaka 1980 wakati Italy walipofungwa 8-9 na CzechSlovakia.

Pia Ujerumani wameendelea kuwa na rekodi nzuri ya kutopoteza mechi kwa mikwaju ya penati kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita – historia inaonesha wamefanikiwa mikwaju mara 7 kati ya 8.

CHADEMA Waapa Kutibua Mkutano wa CCM ,Vijana 2000 Kupelekwa Dodoma Kwa Ajili ya Kazi Hiyo Bofya hapa

 Video:Chadema kuzuia Mkutano wa CCM wa kuchagua mwenyekiti wa chama Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

Vibonzo: Katuni tano bora zaidi leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

TFF wajichanganya kwa Muro bofya hapa

Tamko la RC Makonda kuhusu mashoga waliopo jijini Dar es Salaam 


 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top