Netanyahu: Israeli inataka uhusiano na Afrika

Ndege ya waziri Netanyahu
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ametua nchini Uganda katika ziara ya kwanza kabisa kwa kiongozi wa taifa hilo la kiyahudi kuzuru Afrika tangu mwaka wa 1987. Netanyahu anakutana na viongozi wa mataifa 6 ya Afrika

Ziara hiyo ya siku 5 imeanzia Uganda, na kisha waziri Netanyahu anatarajiwa kuzuru Kenya, Rwanda na kisha Ethiopia. Usalama uliimarishwa

Ilikuwa kihoja kwa wageni waalikwa kuingia kwenye uwanja huo wa ndege kwani usalama uliimarishwa huku maafisa wa usalama wa Israeli wakishika doria na mbwa na walenga shabaha, mbali na upekuzi wa kawaida wa maafisa wa usalama wa Uganda.

Bw Netanyahu ameandamana na mkewe Sarah na ujumbe wa wafanyibiashara wa sekta mbalimbali za uchumi wa Israeli. Netanyahu alipata fursa ya kuhudhuria misa ya ukumbusho wa kakake Yoni mmoja wa makomando wa Irsaeli waliokufa katika shambulizi hilo.

Alipotua katika uwanja huo wa ndege wa Entebbe eneo kulikotokea operesheni ya kipekee miaka 40 iliyopita, ya kuwanusuru mateka wayahudi waliokuwa wametekwa na wanamgambo wa kipalestina, Netanyahu alipata fursa ya kuhudhuria misa ya ukumbusho wa kakake Yoni mmoja wa makomando wa Irsaeli waliokufa katika shambulizi hilo. Mwenge wa ukumbusho uliashwa

Ndege iliyokuwa imewabeba wayahudi hao ilikuwa imetoka Israeli ikielekea Ufaransa.

Kabla ya hapo alikagua gwaride la heshima lililoandamana na makombora 19 kwa heshma yake.

Waziri Netanyahu anasema kuwa ziara hii inalenga kuimarisha uhusiano wa taifa hilo la kiyahudi na mataifa ya Afrika ambayo Israeli inatumai kuwavutia iliwasiwaunge mkono wanaharakati wa Palestina. Baadhi ya mateka wa Entebbe walihudhuria ukumbusho huu

Mwenyeji wake rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amewakaribisha marais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Paul Kagame wa Rwanda Salva Kiir Mayardit, wa Jamuhuri changa zaidi duniani ya Sudan Kusini Edgar Lungu wa Zambia, rais wa Malawi waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, na waziri wa maswala ya Kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga katika kikao cha faragha kinachotarajiwa kujadili maswala ya ugaidi na Usalama wa taifa ambayo Israeli imeahidi kuyasaidia kukabiliana nayo. Ndege aina ya Herculean iliyotumika katika operesheni hiyo

Mwandishi wetu aliyeko Kampala anasema kuwa makomando wa Israeli wameshika doria kote mjini Kampala atakozuru Waziri Netanyahu.

Israeli haijakuwa na uhusiano mwema na mataifa ya Afrika ambayo yaliiona kuwa saliti kwa kushirikiana na serikali dhalimu ya Afrika Kusini iliyokuwa ikiwatesa waafrika weusi. Eneo la mawasiliano lililoharibiwa katika makabiliano hayo ya Entebbe raid

Aidha mataifa ya Afrika yaliunga mkono jitihada za Uhuru wa wapalestina ambao wanakaliwa kimabavu na Isreali na hivyo kutenga taifa hilo la Kiyahudi haswa katika miaka ya 60 na 70 harakati za PLO ziliposhika kasi.

Ziara hii inatarajiwa kupunguza tofauti hizo na kuwapa chambo mataifa ya Afrika iliwalegeze misimamo mikali dhidi ya Israeli.
  Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatatu July 04, 2016  


Vibonzo:Katuni bora zaidi leo Jumatatu July 04, 2016 Bofya hapa 

LOWASSA APIGIWA SALUTI NA WANAJESHI LEO JUMAPILI JULY 03, 2016  Bofya hapa
CHADEMA Waapa Kutibua Mkutano wa CCM ,Vijana 2000 Kupelekwa Dodoma Kwa Ajili ya Kazi Hiyo Bofya hapa 

 Video:Chadema kuzuia Mkutano wa CCM wa kuchagua mwenyekiti wa chama Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa


Vibonzo: Katuni tano bora zaidi leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa

TFF wajichanganya kwa Muro bofya hapa

Tamko la RC Makonda kuhusu mashoga waliopo jijini Dar es Salaam 


 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top