KANGI Lugala, Mbunge wa Mwibara ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa onyo kwa Jamhuri kwa kukwamisha kuwasomea maelezo
ya awali katika kesi inayowakabili.
ya awali katika kesi inayowakabili.
Lugola, Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Lupa na Murad Sadiq, Mbunge wa Mvomero wanatuhumiwa kuomba rushwa ya Sh. 30 mil kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Gairo tarehe 15 Machi mwaka huu.
Lugola alitoa madai hayo jana mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo baada ya wakili wa serikali Denis Lekayo kueleza kuwa, waendesha mashtaka wa kesi hiyo hawapo.
Wakili Lekayo alidai kuwa, shauri hilo liliitishwa kwa ajili maelezo ya awali lakini waendesha mashtaka hawakupo.
Kutokana na maelezo hayo Lugola aliiomba mahakama ikemee tabia hiyo ya kuahirishwa kesi mara kwa mara.
Lugola alisema kitendo hicho kinawanyima haki yao ya msingi ya kufanya shughuli zao za Bunge.
Baada ya Lugola kueleza hayo, wakili wa Serikali, Denis Lekayo aliiomba mahakama radhi na kusema ‘tutafanya haraka kesi iendelee.’
Hakimu Simba alisema, kauli iliyotolea na mshitakiwa ni ya msingi. Baada ya kueleza hayo aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 12 Julai mwaka huu kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.
News alert:Mtuhumiwa wa Ujambazi Maduka ya Pesa, Mauaji Msikitini Awatoroka Polisi aliwatorokaje bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumanne July 05, 2016
AJALI: Masihara ya madereva yasababisha vifo na majeruhi wengi Singida Bofya hapa
LOWASSA APIGIWA SALUTI NA WANAJESHI LEO JUMAPILI JULY 03, 2016 Bofya hapa
Video:Chadema kuzuia Mkutano wa CCM wa kuchagua mwenyekiti wa chama Bofya hapaHabari zilizopo katika Magazeti ya leo Jumapili July 03, 2016 Bofya hapa
Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA