Askofu Gwajima ni Mgonjwa, Ashindwa Kutokea Mahakamani Kwenye Kesi Inayomkabili

PETER Kibatala wakili wa Josephati Gwajima Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima jana aliiomba mahakama kuahirisha tarehe ya kusikiliza kesi inayomkabili askofu huyo sababu anaumwa.

Kibatala alidai mahakamani Kisutu kuwa kutotokea kwa mteja wake jana kulitokana na yeye kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.


Wakili huyo aliwasilisha madai hayo jana katika Mahakaama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Syprian Mkeha Hakimu Mfawidhi anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili Gwajima


Mahakama ilikubali ombi hilo na kwamba kesi hiyo itatajwa tena 2 Agosti mwaka huu.


Katika kesi hiyo Gwajima anadaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam.


Gwajima anadaiwa kufanya tukio hilo kati ya 16 na 25 Machi, mwaka 2015 katika Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.




 Hatimaye TAKUKURU na TRA Wamtaja Mtu Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Kila Dakika Bofya hapa

 Ufafanuzi wa TRA kuhusu ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha Bofya hapa









Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top