Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo, Bungeni Mjini Dodoma amewataka wabunge wa upinzani ambao wamesusia vikao vya Bunge tangu Mei 30 kuingia Bungeni na kuacha kususia vikao vya Bunge kwani hakuna tija kwa Taifa.
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akitoa hutuba ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja.
“Kitendo cha baadhi ya waheshimiwa wabunge kususia vikao vya Bunge hakitoi picha nzuri kwa wananchi waliotuchagua kuwasilisha matatizo yao katika Bunge hili, hivyo natoa rai kwa waheshimiwa wabunge hao kutafakari upya uamuzi wao na niwasihi kwa busara zao waingie ili kwa pamoja na kwa ushirikiano tuweze kutoa ushauri kwa Serikali,” alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha Mhe. Majaliwa alitoa ufafanuzi juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo imetoa haki na kinga kwa waheshimiwa wabunge ili kujadili na kuhoji utendaji wa Serikali kwa uhuru bila mashaka yoyote ya kuweza kushitakiwa wanapotimiza wajibu wao wakiwa Bungeni.
Aliendelea kwa kusema kuwa kinga ya aina hiyo haijatolewa kwa mwananchi yeyote yule Nchini ila kwa Wabunge, hivyo basi hakuna mbunge aliyefungwa mdomo labda aamue kujifunga mdomo yeye mwenyewe.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa Bunge linaongozwa na Katiba, Sheria na Kanuni za Kudumu za Bunge, hivyo ni vyema zikafuatwa kuondoa manung’uniko yasiyo ya lazima na endapo kuna utata katika jambo lolote ndani ya Bunge zipo taratibu zilizowekwa na kanuni za kufuata ili kupata ufumbuzi na si kwa kususa kuingia Bungeni kwani hakuna tija kwa Taifa.
Wabunge wa upinzani wamesusia vikao vya Bunge tangu Mei 30, 2016 mpaka leo Juni 30 ambapo Bunge limehitimishwa.
Aidha wabunge hao wamekuwa wakiingia Bungeni kila asubuhi na jioni kisha kutoka mara tu Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson anapomaliza kusoma Dua maalum la kuliombea Bunge na Taifa.
Breaking News: Wabunge wa CHADEMA Kubenea na James Millya wasimamisha kuhudhuria vikao vya Bunge bofya hapa
News alert: Mh. Joseph Mbilinyi (Sugu) asimashwa kuhudhuria vikao 10 vya bunge la 11 kuanzia leo bofya hapa
News alert: Hivi ndivyo walivyovaa wabunge wa UKAWA leo, watoka na mabango bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Alhamisi June 30, 2016 Bofya hapa
News alert: Mh. Joseph Mbilinyi (Sugu) asimashwa kuhudhuria vikao 10 vya bunge la 11 kuanzia leo bofya hapa
News alert: Hivi ndivyo walivyovaa wabunge wa UKAWA leo, watoka na mabango bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Alhamisi June 30, 2016 Bofya hapa
News alert:Lissu anyimwa Dhamana aweka Rumande, kupelekwa mahakamani kesho Bofya hapa
HIVI NDIVYO ALIVYOONGEA BOFYA HAPA
RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA BOFYA HAPA
Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo Jumatano June 29, 2016 Bofya hapa
Breaking news: Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA