News alert: Tundu Lissu apandishwa kizimbani leo, apata dhamana

IMG-20160630-WA0049.jpg
Mh Tundu Lissu a pandishwa kizimbani mahakama ya kisutu kwa zile tuhuma za maneno ya kuudhi. Katika kesi hiyo Lissu anatetewa na wanasheria 17 wakiongozwa na John Mallya Peter Kibatala na timu nyingine toka makao makao makuu ya Chama.

Katika kesi hiyo Mwendesha mashitaka alisoma shitaka lake kuwa; Mtuhumiwa Mh.Tundu Lisu anashitakiwa kwa makosa ya uchochezi, mnamo tarehe 28/06/2016 akiwa eneo la mahakama kwania ya kudhalau umma dhidi ya mamlaka yao walioyoichagua kihalali, alisema huyu dikteta uchwara lazima tumpinge kila kona" alisema mwendesha mashikata. Mtuhumiwa Tundu Lisu alikataa mashitaka yote. Baadaye Mwendesha mashitaka amlimtaarifu Mh Hakimu kuwa ushahidi wa shauri hili umekamilika, akaomba tarehe ya kuanza usikilizwa,

Katika hatua nyingine Mawakili wa utetezi waliomba mteja wao ambeo dhamana kwa madaio kuwa shauri hilo linadhaminika." Mheshimiwa kwamjibu wa kifungu cha sheria (akataja) Mshitakiwa kosa aliloshitakiwa linadhaminika, hapa tunao wadhamini na zaidi mshitakiwa ni mbunge na mwanasheria wa chama, hivyo anadhaminika, na zaidi mshitakiwa aliliripoti mwenyewe mbele ya polisi baada ya kuitwa tu kwa simu" alisema wakili wa mshitakiwa 

Kwa upande wa wakili wa Sertikali alidai kuwa Mtuhumiwa amekuwa na kawaida ya kutoa tuhuma mbalimbali hivyo kuomba mahakama isikubali mtuhumiwa kupewa dhamani kwa maelezo kuwa anaweza kuibua mambo mengine na kusababisha madhara makubwa zaidi.

Hata hivyo maelezo ya upande wa mashitaka hayakuweza kufua dafu, Hakimu alisema ''Jamhuri haijajenga hoja za kutosha kuzuia dhamana''.Kwahiyo hakuna Pingamizi la Dhamana ambapo Mahakama iliamua kuwa mtuhumiwa apewe dhamana, ndipo wadhamini wa mtuhumiwa wakaitwa mbele kwa ajili ya kuhakiki nyaraka zao


Baada ya taratibu kukamilika,Wamejitokeza Mbunge Susan Lyimo, Madiwani Humphrey Sambo na Rose Moshi Kwa ajili ya kudhamini. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 2, 2016
News alert:Lissu anyimwa Dhamana aweka Rumande, kupelekwa mahakamani kesho Bofya hapa

HIVI NDIVYO ALIVYOONGEA BOFYA HAPA

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA BOFYA HAPA

Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo Jumatano June 29, 2016 Bofya hapa


Breaking news: Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa bofya hapa  




Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top