Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kumuwakilisha Rais Magufuli Kesho Botswana



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo Juni 27 kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wa
Double Troika ya Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama (SADC Double Troika Summit) utakaofanyika kesho Juni 28, 2016.


Mhe. Waziri Mkuu anamuwakilisha Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Gaborone (GICC).


Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Botswana Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama ambaye ni SADC, utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Lesotho. Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu ambao utafanyika leo.


Pia mkutano huo utahudhuriwa na Marais wa Afrika Kusini, Mwenyekiti aliyetoka (outgoing chair) wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama Mhe. Jacob Zuma , Mhe. Jacinto Filipe Nyusi, Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama.


Wengine ni Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Mwenyekiti anayeondoka wa SADC.


Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Aziz Mlima na Maofisa wengine waandamizi.


Breaking news: Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa bofya hapa 







Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA

HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top