Video: MESSI AKOSA PENATI NA KUISHUHUDIA CHILE IKITWAA UBINGWA COPA AMERICA

Image result for messiLionel Messi bado anasubiri taji lake la kwanza akiwa na timu ya taifa ya Argetina.

Messi aliushuhudia mkwaju wake wa penati unagonga ‘mtambaa panya’ kisha Francisco Silva akakwamisha mkwaju wa mwisho wa Chile na kushinda ubingwa
wa Copa America kwa mara ya pili mfululizo kwa kuifunga Argentina kwa jumla ya penati 4-2 baada ya sare ya bila kufungana kwenye mchezo uliokwenda hadi dakika 120.

Akicheza mchezo wa fainali siku mbili baada ya kushrekea birthday yake ya kutimiza miaka 29, Messi amepoteza mchezo wa fainali kwa mara ya tatu mfululizo baada ya ile ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani mwaka 2024, kisha mwaka uliopita wakafungwa kwenye fainali ya Copa America na wenyeji wa michuano hiyo Chile kabla ya kupoteza fainali ya Copa America ya mwaka huu.

Mchezji huyo bora wa FIFA marea tano ameshinda taji la ligi ya mabingwa Ulaya mara nne na makombe nane ya La Liga akiwa na klabu ya FC Barcelona, lakini hajawahi kutwaa kombe lolote akiwa na timu ya wakubwa ya Argentina.

Wakiadhimisha miaka 100 ya shirikisho la soka la America ya kusini, michuano ya mwaka huu ilikuwa na ongezeko la timu na kufikia mataifa 16 ambayo yalichuana nchini Marekani huku Argentina wakiwa na matumaini makubwa ya kutwaa kombe la michuano mikubwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1993.
Tazama video hii mechi ilivyokuwa na jinsi Messi akikosa penati








Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA


HABARI KUU LEO BOFYA HAPA

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top