G7 watishia kuiwekea vikwazo zaidi Urusi

Viongozi wa mataifa saba tajiri kiviwanda G-7 wametishia kuiwekea vikwazo zaidi Urusi ikiwa haitachangia kupatikana ufumbuzi wa mzozo wa Mashariki ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Ukraine. Mataifa saba tajiri kiviwanda yako tayari "kuongezea gharama, pindi ikilazimika" imetajwa katika taarifa iliyochapishwa mwishoni mwa mkutano wa kilele katika mji wa Ise-Shima - Japan. Viongozi wa mataifa saba tajiri kiviwanda wanamaanisha vikwazo vya kiuchumi kwa Moscow havito ondolewa si mpaka makubaliano ya amani ya Minsk yanaheshimiwa kikamilifu. Viongozi wa taifa na serikali za Marekani, Canada, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Italia na Japan wamehudhuria mkutano huo wa Ise-Shima. Viongozi hao wamekubaliana pia kuipatia Iraq msaada wa dala bilioni 3.2 kwaajili ya kuijenga upya nchi hiyo . Kuhusu mzozo wa visiwa vilivyoko katika bahari ya kusini na mashariki mwa China, viongozi wa mataifa saba tajiri kiviwanda wamewaunga mkono majirani wa China na kuhimiza ufumbuzi wa amani. Na kutokana na kudorora ukuaji wa kiuchumi, viongozi wa mataifa saba tajiri kiviwanda wametoa wito vyanzo vyote vya kisiasa vitumiwe ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi ulimwenguni.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top