Michuano ya fainali ya Copa America yamalizika,Kwenye mchezo wa fainali uliokuwa mgumu na upinzani mkali, ulishuhudiwa kila upande ukipoteza
mchezaji mmoja kwa kadi nyekundu huku zikitoka jumla ya kadi nane za njano kwenye pambano hilo lililomalizika bila goli ndani ya dakika 90 na kuongezwa nyingine 30.
mchezaji mmoja kwa kadi nyekundu huku zikitoka jumla ya kadi nane za njano kwenye pambano hilo lililomalizika bila goli ndani ya dakika 90 na kuongezwa nyingine 30.
Messi ambaye amefunga magoli matano kwenye michuano hii, alipiga free-kick ya umbali wa mita 28 baada ya yeye mweyewe kufanyiwa madhambi na Francisco Silva lakini mpira uligonga mabeki na kupita juu kidogo ya mtambaa panya.
Golikipa wa Argentina Sergio Romero alipangua tuta la Arturo Vidal na ikawa zamu ya Messi anayetajwa kuwa mcheaji bora wa kizazi chake huku akifananishwa na mkongwe wa Brazil Pele na Diego Maradona wa Argentina kwa kuwa wachezaji bora wa soka wa muda wote.
Akiwa ameshinda tajia la Olympic akiwa na kikosi cha Argentina cha Under-20, watu wengi wanaamini anahitaji kombe akiwa na timu yake ya taifa kuuhakikishia ulimwengu anaingia kwenye kundi la wachezaji bora wa muda wote duniani.
Nicolas Castillo na Charles Aranguiz wakakwamisha mikwaju yao ya penati kwa upande wa Chile, wakati Javier Mascherano na Aguero nao wakafunga yakwao na kutengeneza sare ya 2-2 baada ya kila upande kupiga penati tatu.
Jean Beausejour akaiweka mbele Chile kisha Bravo akaokoa penati ya Lucas Biglia kisha ikafika zamu ya Silva, kiungo mwenye miaka 30. Messi akajifunika uso kwa jezi yake asione kinachotokea.
Ilikuwa ni fainali ya nne nne kwa Messi kupoteza ambaye alikuwepo pia kwenye kikosi cha Argentina kilichofungwa kwa penati na Brazil kwenye mchezo wa fainali mwaka 2004.
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Jumatatu June 27, 2016 bofya hapa Vibonzo:Katuni tano bora zaidi leo Jumatatu June 27, 2016 bofya hapa
Video: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa Mikoa BOFYA HAPA
News alert:Maombi Ya Mikopo Ya Wanafunzi Wa Elimu Ya Juu 2016/2017Bofya hapa
Breaking news: Rais Magufuli ateua Wakuu wa Wilaya na kufanya mabadiliko kidogo ya wakuu wa mikoa bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA