Video: MAGOLI MAWILI YA RONALDO YAINUSURU URENO KUTUPWA NJE YA EURO



Ureno itacheza dhidi ya Croatia kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro 2016 baada ya Cristiano Ronaldo kufunga bao mbili kwenye mchezo ulioshuhudiwa mabao sita yakifungwa walipopambana
na Hungary huko Lyon.

Zoltan Gera aliifungia Hungary bao la kuongoza lakini Nani aliisawazishia Ureno akimalizia kazi nzuri ya Ronaldo kabla ya mapumziko.

Balazs Dzsudzsak alipiga bao mbili na kuiweka Hungary mbele kwa mara nyingine tena lakini Ronaldo akafanya yake na kuisawazishia Ureno.

Matokeo hayo yanaipa Hungary fursa ya kuongoza Kundi F wakiwa na pointi 5 sawa na Iceland wakitofautishwa na magoli huku Ureno ikikamata nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu wakati Austria ikiyaaga mashindano katika makundi baada ya kumaliza nafasi ya mwisho ikiwa na pointi moja.

Rekodi zilizowekwa
Magoli mawili ya Ronaldo yanamfanya afikishe jumla ya magoli nane kwenye michuano ya Ulaya. Michel Platini pekee ndiye mwenye magoli mengi zaidi ya Cristiano Ronaldo kwenye michuano ya Ulaya (anamagoli 9).
Zoltan Gera ni mchezaji wa pili mzee kufunga goli kwenye michuano ya Euro (miaka 37 na siku 61) akitanguliwa na Ivica Vastic wa Austria mwenye miaka 38 na siku 256.
Gera ni la kwanza tangu alipoifungia Hungary mara ya mwisho November 14, 2014 dhidi ya Finland (sawa na siku 586).
Dzsudzsak ni mchezaji wa kwanza kufunga magoli mawili akiwa nje ya box kwenye mechi moja tangu Wayne Rooney alipofanya hivyo kwenye mchezo wa England v Croatia mwaka 2004.

 Tazama Magoli yote ya mchezo kati ya Hungary v Ureno
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top