Video:Rais Dkt Magufuli atamka rasmi kusitishwa ajira mpya serikalini hii ndio sababu ya kufanya hivyo

 
Tazama video hii chini Rais Dkt Magufuli akitoa ufafanuzi



Rais Dk John Pombe Magufuli, amesitisha ajira mpya serikalini pamoja na upandishwaji wa madaraja na vyeo kwa muda wa mwezi mmoja hadi miwili ili kushughulikia suala la watumishi hewa serikalini.

Rais ametoa agizo hilo katika kilele cha maadhimisho ya miaka hamsini ya benki kuu ya Tanzania BoT, ambapo amesema tatizo la watumishi hewa ni kubwa na linahitaji hatua za dhati na serikali kujipanga ili kuweza kulitokomeza ambapo mpaka sasa aini takriban watumishi hewa 12,446 wamebainika pamoja na wastaafu hewa wanaopata pensheni 2,800.

Rais pia ameziagiza BOT na HAZINA kuhakikisha serikali inapata mapato yake kutoka makampuni ya simu na madini na kulishughulikia tatizo la riba kubwa ambalo limewafanya wananchi wengi kushindwa kutumia fursa ya mikopo.

Akizungumzia sarafu ya Tanzania, Rais ameitaka Benki Kuu ya Tanzania kulinda thamani ya shilingi kwa kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni (dolarization)na kusimamia maduka ya kubadilisha fedha kikamilifu ambako kutasaidia kuimarisha thamani ya shilingi ya Tanzania pamoja na kuepusha utakatishaji wa fedha haramu.

Awali akizungumza katika maadhimisho hayo katibu mkuu wizara ya fedha, LWIKELILE, ameelezea hatua zilizopigwa na benki kuu ya Tanzania tangu kuanzishwa ambapo pia gavana wa benki kuu Profesa Benno Ndullu amemkabidhi Rais Magufuli hundi ya shilingi bilioni nne ikiwa ni mchango wa benki kuu kuunga mkono jitihada za kumaliza tatizo la madawati mashuleni.

Maadhimisho hayo yameambatana na kongamano linaloshirikisha wataalam wa uchumi kutoka ndani na nje ya nchi, wakiwemo magavana 20 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) na wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), mada kuu ikiwa ni: namna ya kupata fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya misaada na mikopo nafuu na athari zake’, mada iliyochaguliwa kwa kuzingatia changamoto ambazo serikali za Afrika zinakumbana nazo katika kugharamia miradi ya maendeleo wakati ambapo misaada na mikopo nafuu imekuwa ikipungua kwa kiasi kikubwa.

Aidha umefanyika uzinduzi wa sarafu ya ukumbusho ya shilingi 50,000 na vitabu viwili, kimoja kikielezea masuala ya sera za uchumi nchini Tanzania na cha pili ni cha miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania kinachoelezea historia, majukumu, mafanikio na changamoto za Benki Kuu katika kipindi hicho na matarajio katika maendeleo ya taifa miaka 50 ijayo.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top