RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 17 & 18



MUANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA...
Samson alizungumza kwa sauti ya ukali, huku akimtumbulia mimacho Rahab
“Unaniuliza wewe kama nani?”
“Sio ninakuuliza kama nani
, ila nataka kujua unataoka wapi kumbuka kwamba hapa upo kwangu?”
“Hupaswi kujua, mwehu nini wewe?”
Samson akanyanyuka kwa hasira na kumzaba Rahab kibao cha shavuni kilicho myumbisha hadi kikamuangusha chini

ENDELEA...
Rahab akasimama kwa hasira, akarusha ngumi ambayo Samson aliidaka kwa mkono wake mmoja na kuachia kibaoa kingine kizoto kilicho myumbisha Rahaba na kumuangusha chini.
“Sikiliza wewe mwanamke, hata siku mmoja huto weza kunipiga sawa”
Samson alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama Rahab anaye jifikiria kunyanyuka kutoka katika sehemu aliyo angukia.Rahba akarusha teke akikusudia kuipiga miguu ya Samson, ila Samsona akaruka juu na kutua chini, akamnyanyua Rahab kwa mkono mmoja na kumvuta karibu yake
“Nitakuumiza”

Rahab akajaribu kumpiga Samson igoti cha tumbo ila Samson akawahi kurudi nyuma, huku akimsukumiza nyuma Rahab.Rahab kwa hasira akarusha teke, akiwa hewani Samson akamuwahi kwa kupiga tele la mbavu lililo sababisha Rahab kuangukia kitandani huku akihema
“Usijaribu tena siku nyingine”

Samson alizungumza huku akimtazama Rahab anaye ugulia maumivu ya mbavu zake.Rahab akamtazama Samson kwa jicho kali lililo jaa maswali na mashaka mengi juu ya Samson kwani kwa jinsi alivyokuwa anamchukulia sivyo jinsi Samson alivyo

“Wewe ni nani?” Rahab aliuliza
“Mimi ni Samson, au unahisi mimi ni nani?”
“Ninamaanisha unafanya kazi gani?”
“Haaaa mimi si fundi baiskeli”

Samson akafungua boksi lake la kuhifadhia nguo zake, akatoa bastola mbili na kumkabidhi Rahab,
“Nenda kafanye kazi yako kwa umakini”
Samson alizungumza huku akijilaza pembeni ya Rahab, huku akijifungua vifungo vya shati lake.Rahab akaichunguza moja ya bastola zake na kuikuta ikiwa na risasi za kutosha, kwa haraka akajigeuza na kumkala tumboni Samson na kumuweka bastola ya kichwa.
“Sema wewe ni nani?”

Rahab alizungumza huku jasho jingi likimwagika, Samsona akamtazama kwa umakini Rahab kisha akaunyanyua mkono wake wa kushoto pasipo kuwa na waga na kuushika mkono wa Rahab alio shika bastola yake na kuusogeza pembeni, mkono wa kulia wa Samson ukapakishika kiuno cha Rahab na kumvuta chini taratibu na sura zao zikawa zimesogeleana kwa ukaribu sana
“Mimi ni fundi baiskeli”

Samson alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa hisia nyingi za mapenzi, kisha taratibu akaukutanisha mdomo waka nawa Rahab, na kuanza kubadilishaa ladha ya mate yao, kila mmoja akajikuta mwili wake ukisisimka kwa kiasi cha kuzidi kuziinua hisia zao za mapenzi huku kila mmoja akijitahidi kumnyonya mwenzake vilivyo, wakaanza kuvuana nguo moja baada ya nyingine na kujikuta wakizama katika dimbwi kubwa la mapenzi, huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha ya kupata penzi la mwenzake

Ndege maalumu ya jeshi ikawekwa tayari kwa safari ya kuwasafirisha Fetty, Halima, Anna na Agnes, ambao tangu wakamatwe maisha yao yamekuwa ni yakufungwa vitambaa vyeusi machoni, huku mikononi na miguuni wakiwa wamefungwa cheni nzzito ambazo si rahisi kwa wao kuweza kuzifungua.Wakavalishwa mavazi ya rangi ya chungwa, yanayo endana na mavazi ya mafundi gereji wengi.Safari ikapangwa kuondoka nchini usiku wa saa nne

Waandishi wa habar pamoja na wananchi wenye hasira kali na wasichana hawa, wamejipanga pembezoni mwa barabara wakisubiria kuwaona wasichana hao wakipelekwa katika uwanja wa ndege kwa ajili ya kuanza safari ya kupelekwa mahakama kuu ya magaidi.Kila mmoja moyoni mwake akawa na sala kubwa ya kuomba wahukumiwe kifungo cha maisha kwani ukatili ambao wameufanya ni mkubwa, ambao haukuwahi kutokea katika nchi inayosifika kwamba ni nchi ya amani.

Kikosi maalumu cha wanajeshi wapatao ishirini na tano, wakiwa na bunduki zao mikononi, wamesimama nje ya magari kumi aina ya GVC yanayotumiwa kusafirishia wahalifu harari, Sifa ta magari haya ni kwamba hayaingii risasi na yametengeneza kwa uwezo mkubwa wa kuhimiili mikiki mikiki ya majambazi endapo wanaweza kuvamia msafara wao.Nitukio la kihistoria nchini Tanzania kwani haijawahi kutokea ndio maana watu wengi pamoja na waandishi wa habari wanaamu ya kushuhudia jinsi msafara huo utakavyokuwa na ulinzi mkali kupita misafara yote ya magaidi walio wahi kukamatwa na jeshi la polisi

Magari yote kumi yakawa yapo tayari kwa safari, wanajeshi hao wakiwa wanasubiria kuletwa kwa magaidi hao walio chini ya ulinzi mkali wa askari.Simu ya IGP Bwana G.Nyangoi inata zikiwa zimesalia dakika tano tu kabla hawajawafungulia magaidi kutoka kwenye chumba maalimu kilicho tengenezwa kwa kuta za chuma, na kuwakabidhi katika kikosi maalumu cha jeshi

“Ndio mkuu” Bwana Nyangoi alizungumza baada ya kuipokea simu yake
“Wahalifu , wabadilishieni msafara”
“Muheshimiwa mbona kila kitu tumeshakiweka kwenye utaratibu”
“Hii ni amri na sio ombi, wasafirisheni na sabmarine”

Rahab na Samson, wakiwa wamevalia nguo za wahudumu wa ndege ya raisi aina ya Air Force, wanafnikiwa kuingia katika ndege, pasipo kustukiwa huku Samson akiwa ametengeneza vitambulisho bandia vinavyo endana na wahudumu kwenye ndege ya Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Praygod MakuyaMbaya zaidi katika siku hii, mtaalamu anaye kagua watu wanao ingia kwenye ndege ya raisi kwa kutumia mashine maalumu, anaumwa sana kiasi kwamba ameshindwa kuwemo katika ndege hii ya raisi, na watu wengine hawana utaalamu wa kuitumia mashine hii kutoka ndege ni mpya katika maisha yao.Samson katika mfuko wake wa nyuma wa suruali ameweka kipakti kidogo chenye madawa ya kulevya yenye nguvu kubwa ya kumlewesha mtu katika muda wa dakika tano tuu

Watu wengi wamezoea kumuona Samson kama fundi baiskeli, na ndivyo jinsi watu wengi wanavyo aminni katika hilo, ila sivyo kama watu wengi wanavyo dhania.Samson ni miongoni mwa wapelelezi wa hatari kutoka nchini Somalia katika kundi la Al-Shabab, Wazazi wake ambao kwa sasa ni marehemu ni watanzania na ameishi Tanzani tangu akiwa mtoto mdogo na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya St. Mary, ila alipo timiza umri wa miaka kumi na mbili aliwashuhudia wazizi wake, baba na mama wakiuwa kinyama na Bwana Praygod Makuya ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ni waziri wa mambo ya nje, wazazi wake walikuwa ni walikuwa ni miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Tanzania kutoka katika chama pinzani, kinachokichua chama kilichopo madarakani katika nafasi za kugombania madaraka ya uraisi.

Kitendo cha wazazi wake kuuawa kikatili katika jumba lao la kifahari lililopo maeneo ya Mbezi beach anaamua kukimbilia nchini Somalia alipo olewa dada yake, alijikuta akivutiwa sana na taarifa za kikundi cha kigaidi kinacho isumbua serikali ya Somalia, ndipo alipo amua kutafuta uwezekano wa yeye kujiunga na kikundi hicho pasipo kumueleza dada yake juu ya nia yake, anafanikiwa kujiunga na kikundi cha Al-Shabab na anapata mafunzo kwa miaka zaidi ya kumi, na anarudi Tanzania na kuanza kujihusisha na utengenezaji wa baiskeil na ukodishaji, na anakuwa ni miongoni mwa mafundi maarufu sana katika mitaa ya Post.

Kazi yake kubwa ambayo amepewa kuifanya ni kuchunguza mfumo mzima wa wapi wanweza kuteka na kusababisha maafa makubwa katika nchi ya Tanzania ndio maana anamua kufanya shuhuli zake nyingi karibu na majengo ya kibiashara ili kujua mfumo mzima wa shuhuli zinazo husika katika maeneo hayo.Utaalamu mkubwa wa utengenezaji wa vyeti au hati bandia, unamuwezesha kufanikiwa kutengeneza vitambulisho vya wafanyakazi katika ndege ya Raisi kwa muda mchache tu, baada ya kuelezwa kila kitu na Rabab, walipo maliza kupeana raha za kitandani

Ndani ya ndege hakuna mtu ambaye alikuwa na shuhuli nao, kila mmoja alikuwa bize na kazi zake, zilizo mpeleka ndani ya ndege hiyo, majira ya saa mbili masafara wa Raisi ukafika uwanja wa ndege na raisi akaingia ndani ya ndege, huku akiwa na furaha kubwa kwa kufanikiwa kuwakamata magaidi walio iaibisha nchi yake na kuonekana ni wazembe katika swala zima la ulinzi

“Tunatakiwa kuwa makini”
Samson alizungumza kwa sauti ya chini, akimnong’oneza Rahab abaada ya watu wote kuombwa na rubani kukaa kwenye viti vyao kwani ndege inajiandaa kuruka hewani, muda mchache kutoka sasa
“Sawa”

Ndege ikaanza kuondoka taratibu kwenye uwanja wa taifa wa mwalimu Julius K.Nyerere, na muda mchache kidogo ikaanza kupaa hewani.Baada ya ndege kukaa sawa hewani watu wakaruhusiwa kuendelea na shuhuli zao, Rahab na Samson wakaingia kwenye chumba kinacho tumika kama baa, na kukaa kama wahudumu wa sehemu hiyo, na kuanza kuwahudumia baadhi ya watu wanao hitaji vinywaji kutoka kwao

“Una simu?”
Samson alimuuliza Rahab
“Hapana, unataka ya nini?”
“Ahaaa, basi”

Wakasitisha mazungumzo yao baada ya Raisi kuingia akiwa na jopo la walinzi wake wapatao sita pamoja na washauri wake wawili.Raisi na washauri wake wakatafuta sehemu na kukaa huku walinzi wake wakiwa wemeizunguka wakiwa makini kwa kila kitu kinacho endelea, Samson akawafwata kwa heshima kubwa, akiwauliza awasaidie kitu gani, kila mmoja akaagizia kinywaji chake, isipo kuwa raisi.Samson akarudi sehemu alipo Rahab na kuchukua vinjwaji alivyo agizwa

“Muheshimiwa wewe hunyi leo?” Mshauri mmoja wa raisi alimuuliza raisi
“Hapana, sijisikii kunywa leo”
“Hivi wale wasichana wanasafiishwa kwa ndege?” Mmoja aliuliza

“Ndio, hapa ndio ninawaza endapo ndege ikianguka itakuwaje?”
“Muheshimiwa raisi, itatubidi tufanye jitihada za za kubadilisha usafiri wao, na mbaya zaidi nasikia wanapitishwa kwenye barabara hizi zetu, je msafara ukivamiwa?”
“Ndio hapa, ninaumiza kichwa changu kujua nini nifanye, nisije nikaingia aibu”

“Ila muheshimiwa, unaonaje wakatumia usafiri wa majini?”
“Maji, maji etii ehee?”
“Ndio kwa maana majini kuna usalama zaidi kuliko angani, kwa maana wanaweza kutunguliwa, huwezi jua wanamtandao gani wale mabinti”
“Karibuni vinjwaji” Samson alizungumza kwa sauti ya upole na kuondoka zake

“Hi naomba muniletee simu”
Raisi alizungumza na mmoja wa walinzi wake akaondoka na kwenda ofisini kwake, baada ya muda kidogo akarudi akiwa ameshika simu.Raisi akaminya baadhi ya namba na kisha akaiweka sikioni simu yake
“Andaeni, submarine(Nyambizi), wasichana nahitaji muwasafirishe nyinyi sawa?”

“Ndio muheshimiwa Raisi”
Raisi akakata simu, na kuminya baadhi ya namba na kumpigia IGP Bwana G.Nyangoi
“Na huo msafara uende kama mulivyo panga, ila mabinti wachukuliwe na kikosi cha majini sawa”
“Ndio muheshimiwa raisi”
Muheshimiwa Raisi akakata simu huku akiwa na jazba kidogo

“Vipi mbona umekasirika?”
“Huyu nyangoi ninamuambia afanye ninavyo taka mimi anadai kila kitu wamekipanga kimekamilika”
“Haaaa…..!!”

“Huyu naye dawa yake inachemka, nitavua madaraka”
“Usifanye hivyo muheshimiwa mpe muda kidogo”
Samson akaachia tabasamu pana baada ya kusikia kwamba wasichana walio kamata wanasafirishwa kwa Sabmarine.
“Nakuja”

Samson alimuaga Rahab na moja kwa moja akaelekea kwenye chumba cha mawasiliano, na kuwakuta wwatu wanao husika kwenye chumba hicho wakiwa wanaendelea na kazi yao
“Munahitaji vinjwaji wapendwa?”

Samson aliwauliza, na watu wanne walipo humo walimtazama kila mmoja akatingisha kichwa akiomba kuletewa chochote kitu, Samson akarudi sehemu ya vinjwaji na kuchukua vinjwaji alivyo ona vitawapendeza watu hao, akajibanza sehemu na kutoa pakti yenye unga kidogo wa madawa ya kulevya na kuweka kwenye kila glasi pasipo mtu yoyote kuona na kuwapelekea.Akawakabidhi kila mmoja glasi yake kisha akatoka na kuanza kuzuga nje ya mlango wa chumba hicho, ndani ya dakika kumi akarudi ndni ya chumba na kuwakuta wote wakiwa wamepitiwa na usingizi fofofo.

Akakaa kwenye moja ya kiti na kuchukua moja ya laptop na kuandika ujumbe mfupi wa meseji kwenda katika makao makuu ya kundi lake la kigaidi la Al-Shabab

SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……18
Samson kabla hajautuma ujembe kwenye kundi la Al-Shabab akapata wazo, akasimama kwenye kiti huku akitabasamu, akawatizama watu wote waliolala kwa kunywa vinjwaji alivyo wapa, akawachukua mmoja baada ya mwengine na kuwiangiza kwenye kijichumba kidogo na kuwafungia.Kisha akarudi kwenye mitamba na kukaa.Kwa elimu ya maswala ya maswasiliana aliyo ipata katika chuo kimoja Afrika kusini alipo pelekwa na kundi hilo la kigaidi la Al-Shabab.Ikamsaidia sana kuweza kukata mawasiliano ya Satelie yanayo ionyeshesha ni wapi ndege ya raisi ipo.

Alipo fanikiwa katika hilo, akafungua moja ya computer inayo shuhulika na maswala mazima ya mfumo wa ndege hii ya raisi, kuanzia kwenye injini ya ndege hadi chumba cha marubani.Kitu alicho anza kukifanya ni kutafuta ni wapi kilipo chumba cha kuhifadhia silaha, na kufanikiwa kukiona, akazitafuta ‘seria number’ za mlango wa chumba hicho, na kufanikiwa kuuufungua.
Marubani wa ndege ya raisi wanaanza kuchanganyikiwa baada ya ramani, inayo waongoza wanapo elekea kufutika kwenye kioo chao, kilichoo pembeni yao.
“Shitii ramani imepote”

Rubani mmoja alizungumza huku akiitazama kioo, wakaanza kufanya kila wanacho jaribu kufanya ila mambo yakawa magumu, wakajaribu kufanya mawasiliano na makao makuu ya uwanja wa ndege wa mwalimu Julius K.Nyerere ila simu zote hazikuweza kwenda sehemu yoyote.

“Jamani tunafanyaje?”
Rubani mmoja alizungumza huku akiwatazama wezake watatu waliopo kwenye chumba chao cha kuiongoza ndege hiyo a raisi ambayo ni yakisasa sana
“Tusimuambie yoyote tuendelee kufanya liwezekanalo?”
“Mmoja aende chumba cha mawasiliano kuangalia kuna nini?”

“Jaribu kuwapigia simu kwanza”
Mmoja wa marubani akachukua simu iliyopo pembeni yake na kujaribu kuwapigia ila hapakuwa na mawasiliano yoyote zaidi ya simu hiyo kutoa mlio wa kukatika
“Simu hazitoki”
“Ngoja niende kutazama kinacho endelea”
Rubani mmoja akatoka ndani ya chumba chao na kuanza kuelekea chumba cha mawasiliano ambacho kipo mbali kidogo na sehemu walipo wao

Hapakuwa na ubishi zaidi ya kamanda mkuu wa polisi kukubaliana na amri ya Raisi Praygod Makuya, akaagiza misafara kupangwa kama kaaida, huku kikosi cha wanajeshi watano wa majini, ambao wanaaminika sana, wakawasili kwenye makao makuu ya jeshi la polisi pasipo mtu raia wa kawaida kuelewa jambo linalo endelea,

Gari zilizo kuwa zimeandaliwa kwa safari ya kuelekea uwanja wa ndege zikaanza kutoka moja baada ya nyingine, huku helcoptar zipatazo sita zikiwa juu angani, zikilinda ulinzi wa magari hayo yanayo tembea kwenye msururu mmoja, huku pembeni wakiwa wamening’inia wanajeshi wawili wawili wakiwa wameshika bunduki zao.


Kila mwenye kamera yake, iwe ya simu au kamera halisi, hakusita kuchukua video au kupiga picha msafara huo ambao, una ulinzi mkali na kwatanzania haikuwahi kutokea tukio la namna hii, tangu nchi kupata uhuru na watu wengi wamezoea kuona misafara ya maraisi haswa maraisi wa marekani kuwa na ulinzi mkali wa namna hii,

Fetty, Halima, Anna na Agnes wakaingizwa kwenye moja ya gari ambalo hutumiwa na jeshi la polisi kwa ajili ya kusafirisha kiasi kikubwa cha pesa kutoka benki moja kwenda benki nyingine, sifa ya gari hili, halipitishi risasi hata moja, kwani limetengenezwa kwa kiwango cha bati gumu, lisilo weza kutetereka kiraisi kwa kupigwa risasi, matairi yake yametengenezwa pira gumu lisilo jazwa upepo wa aina yoyote.


Safari ikaanza huku wakiwa wamevalishwa vitambaa vyeusi kichwani mwao, kila mmoja wao mikononi mwake amefungwa pingu ngumu isiyo weza kufunguka kirahisi, miguuni mwao wamefungwa nyororo ya pamoja inayo walazimu kutembea kwa mstari mmoja.Mwendo wa kufika bandarini haikuchukua muda mrefu sana, huku wakiwa chini ya ulinzi wa askari hao wa majini.Wakashushwa kwenye gari pasipo wao kujua ni wapi wanapo elekea

Wakaingizwa kwenye moja ya boti ya jeshi iliyokuwa ikiwasubiria, na boti hiyo ya jeshi ikaelekea kwa umbali wa kilomita kumi na tano kutoka ilipo ichi kavu, na kukuta, meli ya kijeshi inayo pita chini ya maji(Nyambizi au submarine) ikiwasubiria,
“Jamani tunaelekewa wapi?”
Anna aliuliza kwa sauti ya chini, ila akastukia akibipigwa ngumi ya mgono na askari mmoja
“Munakwenda kuzimu”

Askari alimjibu Anna kwa dharau kubwa, wakawapandisha kwenye meli hiyo ya kivita, na kuwaingiza ndani kwenye moja ya chumba ambacho sio rahisi kwa wao kutoka,Taratibu meli ikawashwa, ilipo anza kuchanganya, ikaanza kuzama ndani ya maji taratibu na kushuka kina kirefu na kuanza safari
Kupotea kwa mawasiliano kwa ndege ya raisi inaanza kuwaumiza kichwa, viongozi wa kitengo mawasiliano kilichopo kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu Juliusi Kambarage nyerere, wanajaribu kuseti mtambo wao wa rada vizuri kuona ni kitu gani kimeipata ndege ya raisi ila wanashindwa, wanafanya mawasiliano na serikali ya Marekani kuomba msaada wa kijeshi kuitafuta ndege ya raisi wa Tanzania.


Kutokanana ushirikiano mzuri wa serikali mbili hizi, ombi lao linafanyiwa kazi mara moja na wanaanza kutumia Satelaiti zao kuitafuta ndege ya raisi ila wanashindwa kufanikiwa, kila mbinu na jitihada za kuitafuta ndege hiyo inashindikana, jambo linaloanza kuzua hofu miongoni mwa viongozi wa nchi mbili hizi.

“Ni kitu gani tunaweza kufanya?”
Ni swali la mkuu wa jeshi wa anga wa Tanzania akizungumza na mkuu wa jeshi la anga nchini Marekani kwa kutumia simu
“Tumefanya kila liwezekanano kuhakikisha tunaipata ndege ya raisi ila imeshindikana, laiti kama ingekuwa imeanguka tungefahamu”

“Sasa inakuwaje?”
“Tuendeleeni kufanya jituhada za kuitafuta, kwani ningesema nitume ndege zangu za kijeshi kwenda kuitafuta itakuwa ni ngumu, kutokana hatujui ni wapi ilipo”
“Sawa tutaendelea kuwasiliana kwa kila ambalo litakuwa linaendelea”
“Sawa”

Mkuu wa jeshi anga la anga la Tanzania anakata simu na kumgeukia makumu wa Raisi wa Tanzania, ambaye ameitisha kikao cha dharura kwa wakuu wote wa jeshi na mawaziri, baada ya kupokea taarifa ya kupotea kwa ndege ya raisi.
“Hawajaipata bado”
“Tunafanye nini?”
“Mkuu hata mimi, sifahamu, vijana wanaendelea kucheza na mitambo kujua ni kitu gani ambacho kinaendelea”
Rahab baada ya kuona, Samson anakawia kurudi kwenye chumba cha mawasiliano kama alivyo muaga, anaondoka na kwenda kilipo chumba hicho kabla hajaingia anakutana na rubani, akitaka kuingia kwenye chumba hicho
“Samahani kaka yangu”

Rahab anazungumza huku, akifungua kifungo cha shati lake alilo livaa na kuyapandisha maziwa yake juu kidogo na kumfanya rubani, huyo kubaki akiwa ameshika kitasa cha mlango pasipo kufungu, huku mimacho yake yote akiwa ameyatulisha kwenye kifua cha Rahab.

“Bila samahani?”
“Umemuona kaka mmoja, mrefu hivi?”
“Hapana”
Mazungumzo ya Rahab na rubani nje ya mlango yanamstua Samson, anaye endelea kufunga mawasiliano ya ndege hii ya raisi kwa kutumia utaalamu mkubwa alio nao.
“Shiti amekuja kufanya nini huyu?”

Samson alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti alicho kikalia, akapiga hatua hadi mlangoni na kufungua mlango na kumkuta rubani akiwa amesimama na Rahab, Samson hakutaka kuuliza na alicho kifanya ni kumvuta ndani rubani, huyo, na pasipo kuwa na haruma akamvunja shingo rubani na kumuua hapo hapo
“Funga mlango kwa ndani”

Rahab akabaki akiwa ameduwaa, kwani tukio la kuuliwa kwa rubani huyo limechukua sekunde kadhaa.Rahab akafanya kama alivyo agizwa na Samson, ambaye alishaanza kuvuta rubani huyo na kumuingizwa kwenye chumba cha alicho waingiza wahudumu wanao shuhulika na mawasiliano
“Unaweza kutumia computer?”
Samson alizungumza huku jasho likimwagika
“Kidogo?”
“Kama huwezi, kaa uangalie ninicho kifanya”

Samson akaka kwenye moja ya cumputer inayo onyesha mfumo wa vyumba vyote kwenye ndege, akaanza kufunga mlango wa chumba cha marubani, na kubadilisha namba za siri za kufungulia mlango huo.Ukafwatia mlango wa chumba alichopo raisi na watu wake, pasipo wao kujua.Akaangalia kwenye computer nyingine inayo onyesha picha za rada(kamera za ulinzi) zilizopo kwenye ndege hiyo, akaaona idadi kubwa ya watu wamelala, kwenye siti zao.
“Unaona hii ni chumba namba moja, ninafunga, milango yao, hakuna mtu kutoka.Kina abiria saba”

Samson alizungumza, huku akimuonyesha Rahab jinsi anavyo fanya.Na kila kitu anacho kifanya Samson ni kigeni mwachoni mwa Rahab, hadi sasa hivi haamini kwamba Samson anaye mjua ndio anayefanya kazi kubwa kiasi hichi.Samson baada ya kukamilisha zoezi zima la kufunga milango yote kasoro chumba cha kuhifadhia silaha akamuagiza Rahab

“Hili chumba kipo chini, unapita kwenye hii kordo kunangazi utaziona za kushuka chini, hapo ndipo utakapo shuka na kukikuta hichi chumba, chukua bunduki unazo ona zitatutosha sawa”
Samson alizungumza huku akimuonyesha Rahaba sehemu anayo paswa kwenda kupitia kwenye computer
“Dakika tano uwe umesharudi hapa”
“Sawa”

Rahab akatoka na kwenda sehemu kilipo chumba cha kuhifadhia silaha, akaanza kuchagua bunduki moja baada ya ningine, akaziweka kwenye mfuko mkubwa alio uona pembeni ya chumba hicho, ulio tengenezwa kitambaa kigumu.Akaweka na boksi nyingi za risasi pamoja na magazine zake.Kabla hajatoka akaona nguo za kijeshi pamoja na majaketi ya kuzuia risasi, akavua nguo zake na kuvaa nguo alizo ziona kisha kabeba na nguo za Samson na kurudi kwenye chumba hicho.Akamkuta Samson akiitegesha video camera vizuri
“Hiyo nayo ni yakazi gani?”
“Kuna kitu nataka kufanya”

Samson akavaa nguo alizo pewa na Rahab na kujiweka sawa, na kuiwesha video camera hiyo na kukaa kwenye moja ya kiti huku Camera hiyo ikianza kuchukua picha kuanzia kifuani hadi miguuni.Video zote zilizopo ndani ya ndee zikakata vipindi vinavyo onyesha na kuonyesha video ya mtu anaye onekana kuanzia kifuani hadi miguuni

“NDUGU ABIRIA, NIFURAHA YANGU KUWA NANYI KATIKA SAFARI HII, NIMETOA LISAA MOJA KWA KILA ABIRIA KUSALI SALA YAKE YA MWISHO KWANI NDEGE INAKWENDA KULIPUKA NDANI YA LISAA HILO KUTIMIA KAMA HUAMINI, TIZAMA HII”
Samson akaishika camera na kuigeuzia kwenye computer aliyo iietega mwendo kasi wa saa, unao onyesha dakika zake zikirudi nyuma, kwani ikifika ndani ya muda alio upanga, mfumo mzima wa ndege unakwenda kuzima, na litakalo tokea hapo ni ndege kulipuka, jambo lililo anza kumuogopesha kila mmoja aliyomo ndani ya ndege hadi raisi mwenyewe
 ITAENDELEA.....


RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 15 & 16 bofya hapa 


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top