RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 21 & 22


MUANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA...
“TATU, MBILI, MOJA”
Mlipuko mkubwa ulio ambatana na moto ukasikika machoni masikioni na watazamaji wa Tv walio kuwa wakilifwatilia tukio zima, na Tv zao zote, ndani ya sekunde mbili zikabadilika na kuwa chenga
jambo lililo waacha midomo wazi Watanzania wengine na wengine kushindwa kustamihili ujasiri na kujikuta wakiangua vilio hadharani

ENDELEA...
Ukimya ukatawala miongoni mwa watu wengi walio kuwa wakitazama taarifa ya hivi punde, juu ya Raisi Praygod Makuya kutekwa na kulipuliwa kwenye ndege yake na watu ambao hadi sasa hivi hawajajulikana ni kina nani.Kila mmoja akaanza kuhisi kwamba ni ndoto ya asubuhi ila ndio ukweli halisi kwao, Tv zao zote zikaendelea kuonyesha chenga, jambo ambalo kwa kipindi hicho cha nchi ya Tanzania kutumiamfumo wa ‘Digital’ ni ngumu sana, kuziona chenga za namna hii kama ilivyo kuwa kipindi cha ‘Analogia’

Viongozi wote walio kuwa wamejikusanya kwenye chumba cha mikutano wakifanya wawasiliano namkuu wa jeshi la anga nchini Marekanani, wanabaki midomo wazi huku wengine wenye mioyo myepesi wakijikuta wakimwagikwa na machozi pasipo wao kutarajia.

“Mmmm”
Makamu wa raisi bwana Gift Kalunde anaguna nia yake ni kuwastua ambao bado wamepigwa na bumbuwazi.
“Jamani, kila mmoja amejionea kilicho tokea.Ila niawaomba muendelee na kazi”

Muheshimiwa Gift alizungumza kwa sauti ya unyonge yenye simanzi ndani yake, akajizoa kimya kimya na kutoka ndani ya ukumbi na kuingia kwenye moja ya chumba akajifungia na kuanza kushangilia hadi jasho la mwili likaanza kumwagika.Furaha yake si kuwa raisi wa muda ila furaha yake ni kuona adui yake namba moja ameondoka kwenye hii dunia.
Anna baada ya kuvuta pumzi ya kutosha akajinyanyua na kushuka kitandani, akapiga hatua hadi mlangoni, akaufunga mlango kwa ndani kisha akarudi kwenye meza yenye computer kadhaa, akazitumbulia mimacho na kuwaona wezake wakiwa kwenye moja ya chumba, akaaendelea kuchunguza chunguza kwenye kila computer, akagundua wapo kwenye Nyambizi ya kijeshi(Submarine)
“Tutatokaje humu?”

Anna alijiuliza swali, huku akitazama kila sehemu ya chumba alichopo, akapiga hatua hadi kwenye moja ya kabati kubwa, akalifungua na kukuta shehena kubwa ya silaha zilizo pangwa vzuri, akachukua moja ya bastola aina ya ‘browning SFS’ na kuichomoa magazine akakuta risasi za kutosha, bila ya kupoteza muda akaanza kukusanya bastola ambazo anaweza kuzibeba kwa wakati mmoja, ambazo zote ni zaaina moja, akaiokota nguo yake na kukuta ikiwa imechanika sana kiasi cha kutowezekana kuvaliwa, Akayazungusha macho yake kwenye kila pande ya chumba na kukuta nguo za Mathias ambazo ni za jeshi zikiwa zimening’inizwa kwenye moja ya msumari, akachukua shati moja, na kulivaa, ambalo ukubwa wake kwake ukawa kama gauni,
“Ni nzuri”

Anna alijisemea mwenyewe kimoyo moyo huku akijitazama kwenye kioo kikubwa cha kabati.Akachukua mkanda wa suruali wa Mathias na kujifunga kiunoni, kutokana na wembamba ikamlazimu kutoboa tobo jipya katika mkanda huo, ili umbane vizuri.Akazichomeka bastola nane kiunoni mwake zote zikiwa zimeajaa lisaha za kutosha, kisha yeye mwenyewe akashika bastola mbili mkononi mwake ambazo zimefungwa viwambo vya kuzuia mlio.
“Bye muheshimiwa tumbo”

Anna alizungumza huku akifyatua risasi kadhaa zilizo tua kwenye tumbo la Mathias Reymond ambaye hadi tayari amesha fariki dunia, alipo ridhika, akashusha pumzi nyingi na kuanza kupiga hatua za haraka kuelekea ulipo mlango, akakishika taratibu kitasa cha mlango na kuanza kuuvuta polepole, akachungulia na kumkuta askari mmoja mwenye mwili mkubwa akiwa amesimama nje ya mlango huku mikono yake akiwa aimeweka kwa nyuma, kama sheria mojawapo ya kijeshi.
“Huyu ndio aliye nileta humu”

Anna alijisemea kimoyo moyo, bila hata ya kupoteza muda akafyatua risasi mbili zilizo ingia kwa nyuma kwenye kichwa askari huyo, na akaanguka kama gunia la chumvi huku kichwa chake kikichanguka kwa nyuma.Anna akaanza kutembea kwa umakini akiifwata njia iliyo nyooka yenye vyumba huku na huku, akiwa katikati ya kordo ndefu gafla mlio mkali wa sauti ya king’ora cha hatari, ikaanza kulia kwa nguvu akaanza kukimbia kabla hajafika mbali. 


Gafla akakutana na askari wanne wakiwa na bunduki mikononi mwao na kumuamrisha Anna kunyoosha mikono juu, wazo la haraka likamjia Anna kichwani mwake, akapandishia shati lake juu, na kuziacha sehemu zake za siri wazi na kuwafanya askari hao kubaki wakishangaa, huku baadhi wakimeza mafumba ya mate kwa uchu mkali wa kuto kukutana na mwanamke kimwili katika kipindi kirefu cha wao kushinda ndani ya maji baharini kwenye nyambizi yao.


Sauti ya king’ora cha hatari kikaanza kuwastua Fetty na wezake wawili ambao hadi sasa hivi wapo ndani ya chumba ambacho hawajui ni wapi, walipo
“Nini hicho?” Halima aliuliza
“King’ora cha hatari hicho”

Fetty alijibu huku akiandelea kusimama katikati ya chumba, huku kichwa chake kikiwa bado kimefunikwa na kofia jeusi, ambalo hadi muda huu wameshindwa kujivua kutokana na mikono yao kufungwa kwa nyuma na pingu.
Askari mmmoja akafungua ndani ya chumba walipo Fetty na wezake kuangalia kama wapo, 
“Wewe mpumbavu rudi ukae chini”

Askari alizungumza huku akimfwata Fetty kwenye sehemu aliyo simama, kitendo cha kumsogelea Fetty ikawa ni koso lake kubwa, kwa kutumia hisia kali Fetty aliweza kujirusha na kumtandika askari kichwa kimoja kikali cha pua na kumfanya aanguke chini, kwa hasira askari akampiga mtama Fetty na kumuangusha chini, akamkalia Fetty tumboni na kunza kumshambulia kwa kumtandika vibao mfululizo vya kichwani.


Pesi wa miguu ya Fetty, ukamsaidia katika kuipitisha miguu yake yenye nyororo ndefu shingoni mwa askari huyo na kumvuta kwa nyuma, na kuanza kumkaba kwa nguvu zake zote.Askari akajikuta akianza kufanya mawasiliano na mtoa roho, kwani kila anavyo jaribu kuitoa nyororo hiyo iliyo mpiga kabali, anashindwa na taratibu anajikuta akianza kuishiwa na nguvu, huku pumzi ikikosekana kwenye mzunguko wa mapafu yake na mwisho wa siku anakata roho taratibu

“Hei”
Fetty aliwaita wezaka baada ya kuhisi askari huyo ametulia kimya
“Tupo” Agnes alijibu
“Acheni kuzubaa sasa, njooni hapa tumpapase kama anafunguo”

Fetty alizungumza huku akiitoa mkiguu yake kwenye shingo ya askari huyo, Halima na Agnes wakaanza kutambaa chini kwa kutumi makali pamoja na mikono yao iliyo fumgwa pingu kwa nyuma, japo wanapata tabu kufika walipo lala Fetty na askari, ila wakafanikiwa kupafika.Wakaanza kumpapasa askari huyo kuanzia miguuni hadi kiunoni na Agens akafanikiwa kupata funguo nyingi 
“Nimepeta funguo sijui ndizo zenyewe”
“Jaribisha sasa” 

Fetty alizungumza huku jasho jingi likimwagika kutokana na shuhuli pevu aliyo ifanya, Agnes akaanza kuichunguza funguo moja baada ya nyingine, na kupata kifunguo kidogo cha pingu
“Nimepata kafunguo”
“Hembu ngoja nikusogelee”

Fetty akajiburuza hadi sehemu alipo Agnes, wakaegemeana migongo na Agnes akaanza kumfungua Fetty pingu za mikono yake, cha kushukuru MUNGU, pingu ya Fetty ikafunguka
“Yeaaahh”

Fetty alishangilia kwa haraka akaitoa pingu kwenye mikono yake, kisha akafungua mikanda nya mikofia waliyo vishwa, furaha yake yote ikaingia shubiri baada ya macho yake kukutana na mdomo wa bunduki aina ya SMG ikimtazama huku macho makali yaliyo jaa hasira na jazba ya askari aliye uliwa rafiki yake yakimtazama Fetty....

SHE IS MY WIFE (NI MKE WANGU)……22

.....Fetty hakutaka kumpa nafasi askari huyo kuchukua maamuzi yoyote katika kitendo chake cha kumnyooshea bunduki aliyo ishika, kwa haraka Fetty akaibeta bunduki ya askari huyo na kuangukia pembeni, jambo lililompa kiwewe askari huyo, Fetty akasimama huku mikono yake akiikunja ngumi akisubiria shambulizi kutoka kwa askari huyu, ambaye hadi muda huu macho yake yote aliyapeleka kwenye bunduki yake ilio anguka chini

Mshangao wa askari, wanao zishangaa sehemu za siri na Anna, ikawa ni nafasi nzuri kwake kuwafyatuli risasi zisizo na idadi askari hawa na kuwasababishia kifo tulivu kwenye maisha yao.
“Shabaha nzuri my baby”

Anna alizungumza huku akiibusu bastola zake na kuwaruka askari walio anguka chini na kwenda katika sehemu kilipo chumba walipo wezake, mwendo wake wa umakini ulimuwezesha kumuangamiza kila askari ambaya anakatiza mbele yake hadi akafanikiwa kufika kwenye chumba walichopo wezake, akamkuta Fetty amesimama huku akitazamana na askari aliye kunja ngumi
Fetty baada ya kumuona Anna akiwa amesimama nyuma ya askari anaya tazamana naye akaamua kushusha mikono yake chini na kumkonyeza Anna
“Oya broo”

Anna alizungumza huku bastola yake moja akiwa ameielekeza kwenye kichogo cha askari huyu, ambaye aligeuka haraka na kukutana na sura ya Anna akitabasamu
“Kwaheri”
Anna akafyatua risasi moja aliyoingia kwenye kichwa cha askari na kumfaya aanguke chini kama mzigo
“Poleni mashoga zangu”

Anna alizungumza huku akisaidia na Fetty kuwafungua pingu za miguuni na mikononi Halima na Agnes
“Asanteni”
Agnes alishukuru baada ya mikono yake kuwa huru, Anna akawakabidhi wezake kila mmoja bastola yake ambayo ameichukua
“Na hilo shati vibi shosti”
Halima alizungumza huku akitabasamu
“Huu ni muda wa kazi Halima, maswali mengi baadaye”

Anna alizungumza huku akimtazama Halima, Anna akasaidiana na wezake kumvua nguo, askari mmoja waliye muua kisha akazivaa pamoja na viatu vyake.
“Jamani, hapa tulipo tupo chini ya maji, hili ni manoari ambayo ndio inatumika katika kutusafirishia.Maana yangu ya kuzungumza hivyo nikwamba tuwe makini sana kwa kila hatua ambayo tunapiga”
Anna alizungumza kwa umakini huku akiwatazama wezake ambao kila mmoja alionekana kuwa makini kwa maelezo anayo yapata kutoka kwa Anna
“Tumekusoma”

Agnes alizungumza, Fetty akapiga hatua hadi mlangoni na kuchungulia nje ambapo, akatazama kila kona ya nje, hakuona dalili yoyote ya kuwepo na watu zaidi ya miili ya askari walio uliwa na Anna wakiwa wamelala chini, Fetty akanyoosha kidole kimoja akiashiria kwamba mmoja atoke nje, Anna bila kusita akatoka na kwa mwendo wa umakini wakaanza kutembea kuelekea chumba cha manahodha.Kila askari ambaye wanakutana naye hawakusita kumshambulia kwa risasi, haikuwa kazi ngumu sana kwao kufika kwenye chumba cha manahodha na kuwakuta wakiwa wawili, wakijitahidi kufanya mawasiliano na makao makuu ya jeshi la maji, juu ya kuangamizwa kwa wezao wengi
Kutekwa kwa nyambizi(Submarine), ya jeshi la maji, ikawa ni pigo jengine jipya kwa wakuu wa jeshi ambao hadi muda huu wanapambana kupata kujua ni wapi wanaweza kuyapata mabaki ya ndege ya raisi wa Tanzania, sehemu ilipo anguka.
“Haoo waalifu je, wamo?”
Mkuu wa jeshi la maji bwana Lissu alimuuliza mmoja wa manahodha baada ya kuipokea simu yake,
“Ndio tupo”
Sauti ya Fetty alisikika masikiono mwa bwana Lissu, ambaye alianza kuchanganyikiwa na mwili mzima ukaanza kumtetemeka

“Mipango yenu imeoza na hatuna jinsi zaidi ya kuwarudia nyinyi, what goes around, always comes around”
Fetty alizungumza kisha, akafyatua risasi mbili zilizo zidi kumstua sana bwana Lissu na kujikuta mwili wake mzima ukimtetemeka huku akiitazama simua yake, ambayo inatoa mlio wa kukatw
“HAHAHAAAAAAAAAAA”
Samson akazidi kucheka kwa dharau huku akikitazama kioo cha computer kinacho onyesha mlipuko, ambao hadi sasa Watanzania wengi wanaamini ya kwamba raisi wao ameshafariki dunia
“Nahisi watu wako kwa sasa watakuwa wanamwagikwa na machozi, etiiii?”
Samson alizungumza huku akikinyanyua kichwa cha raisi Praygod Makuya, kwa kutumia bastola yake aliyo ishika.
“Your son of bitch”

Raisi alitukana huku akimtemea mate ya uso, Samson.Rahab akabaki akimtazama Raisi Praygod jinsi anavyo vuja damu nyingi usoni mwake kutokana na kipigo kikali alicho kipata kutoka kwa Samso ambaye muda huu anayafuta mate yaliyo tua usoni mwake kwa kutumia kiganja chake cha mkono wake wa kushoto, kisha tataribu akayalamba mate ya raisi Praygod Makuya

“Mmmmm, mate yako ni mazuri sana, ninaimani kama ungekuwa ni mwanamke ungekuwa so mwaaaaa”
Samson aliendelea kuzungumza kidhara, Samson akaka kwenye kiti cha kuzunguka na kuanza kuzunguka taratibu huku akiichezesha chezesha bastola yeka aliyo ishika mkononi mwake

“Samso ni kitu gani ambacho kitaendelea”
Rahab alizungumza huku akimtazama Samson aliye fumba macho yake huku akizunguka zunguka kwenye kiti alicho kikalia

“Wewe unahisi nini?”
“Samson hilo sio jibu”
“Unataka jibu halisi?”
Samson alimjibu Rahab kidharau jambo lililo anza kumkera Rahab, ambaye hadi muda huu ameshaanza kupoteza imani na Samson
“Ndio”

Samson akainyanyua bastola yake na kuikoki vizuri kisha akaielekezea sehemua alipo kaa Raisi Praygod,
“Moja, mbili, ta….”
“Ngoja kwanza, unataka umfanyaje huyo Raisi?”
Rahab alizungumza huku mapigo ya moyo yakimyuenda kasi, kwani moyoni mwake amesha anza kumuonea haruma muheshimiwa riasi
“Namuua”
“Huwezi kumuua raisi kiraisi hivyo”
“Ahaaaaa powa”

Samson akamuelekezea Rahab bastola, jambo lililo mstua Rahab moyo wake, kabla Rahab hajafanya chochote Samson akafyatua risasi zilizo tua kifuani mwa Rahab na kumuangusha chini, jambo lililo mstua Raisi Praygod Makuya
“Huwa sipendagi dharau nawatoto wa kike”

Samson alizungumza huku akinyanyuka kwenye kitia alicho kikalia , kwa hatua za taratibu akatembea hadi sehemu alipo lala Rahab, ambaye hajafariki dunia na wala risasi hazijaingia mwilini mwake kutokana na jaketi la kuzuia risasi alilo kivaa.Kwa haraka Rahab akarusha teke lililo ichota miguu yote miwili ya Samson na kumuangusha chini kama mzigo, muheshimiwa raisi akabaki akishangaa, Rahab akanyanyuka kwa haraka na kuipiga teke bastola ya Samson na ikaangukia miguuni mwa muheshimiwa raisi
“Waooo kumbe upo hai”

Samson alizungumza huku akijinyanyua na kuanza kujipangusa pangusa kwa dharau, Rahaba akarusha ngumi kashaa kwa Samson ambazo, zote Samson aliweza kuzipangua kwa mikono yake mikakamavu, kisha akamtandika ngumi moja Rahab aliyo myumbisha mithili ya mlevi wa pombe za kienyeji.Rahab akakitingisha kichwa chake, ili kukilazimisha kizunguzungu alicho kipata gafla kukata.Samson akarusha teke ambalo Rahab aliweza kuliona likija na kuamua kulikwepa kwa kupiga msamba, Ngumi nzito ikatua sehemu za siri za Samson na kumfanya ajikunje huku akitoa mguno mkali wa maumivu.Ikawa ni zamu ya Rahab kupeleka mashambulizi ya ngumi nzito zilizo tua usoni mwa Samson
“Ulikuwa hunijui vizuri”

Rahab alizungumza huku akipeleka mashambulizi ya haraka yasiyo na idadi mwilini mwa Samson, ambya damu zilisha anza kumvuja puani. Samson akasimama na kuitunisha misuli yake ya mwili mzima, kila ngumi na teke ambalo Rahab aliyepiga, alishangaa kumuona Samson akiwa hatetereki wala kuhisi maumivu ya aina yoyote
“Hhaaaaaa, piga teke jingine la mwisho”

Samson alizungumza huku damu zikimwagika puani mwake, Rahab akajirusha hewani na kumpiga Samson teke shingo, lililo myumbisha kidogo Samson, Rahab akajaribu kujirusha hewani ila ngumi kali iliyo tua puani mwake ikamfanya aanguke chini na kuanza kuvuja damu, wakati mapambano yakiendela kati ya Samson na Rahab, muheshimiwa Raisi akawa na kazi ya kujitahidi kuifungua mikono yake, iliyo fungwa na gundi kubwa, inayotumika kufungia maboksi makubwa ya kusafirishia vitu mbalimbali kama Tv.

Samson akamkalia Rahab tumboni mwake na kuanza kumshindilia mangumi mazito yasiyo na idadi, tararibu Rahab akaanza kujitahidi kukichomoa kisu alicho kichomeka kwenye kiatu chake cha jeshi alicho kivaa, akfanikiwa kukichomoa na kwaharaka akakikita kisu kwenye mbavu za Samson aliye toa ukelele mkali wa maumivu na akamsukumiza pembeni.

Rahab akasimama huku akiyumba yumba na kwenda sehemu alipo muheshimiwa Raisi, akachimoa kishu kinginge kidogo alichokuwa anekiweka kwenye mfuko wa suruali aliyo ivaa, na kuikat gundi aliyo fungwa Raisi kwenye mikono yake na miguu yake
“Upo salama muheshimiwa raisi?”
Rahab alizunngumza huku akimsaidia muheshimiwa Raisi kunyanyuka
“Ndio, asante binti”

Rahab akamgeukia Samson na kumkuta akijitahidi kukichomoa kishu alicho mchomo kwenye mbavu, Rahab akaiokota bastola iliyokuwa chini ya miguu ya muheshimiwa raisi na kupiga hatua na kwenda sehemua alipo lala Samson
“Tutaonana kuzimu”

Kabla hata Rahab ajafyatua risasi ya aina yoyote ndege ikayumba gafla na kuwaangusha raisi na Rahab, kutokana na Samson kuifunga mitambo yote ya ndege, ikiwemo mashine baadhi za uendeshaji wa ndege, zimesababisha marubani kushindwa kuikwepa ndege ya abiria ya shirika la Fly Emirates, ambayo zimekutana kwenye njia moja, marubani wa ndege ya abiria hawakuweza kuiona mapemba ndege ya Raisi wa Tanzania, kutokana na kushindwa kuiona kwenye rada zao, na wakajikuta wakiingonga, ndege ya raisi wa Tanzania kwenye ubavu wa nyuma wa ndege na kuisababisha kugeuka mara mbili na kuanza kwenda chini kwa kasi sana, huku ndege yao ya abiria ikiianza kuwaka moto...


ITAENDELEA....





Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top