Inawezekana kabisa unatamani kujua asili ya upinzani wa jadi kati ya Simba na Yanga unasababishwa na nini na ulianza lini hadi leo Simba vs Yanga kuwa miongoni mwa derby kubwa barani Afrika.
Maswali yako huenda yakapata majibu, Mzee Hashimu Mwika ambaye ameeleza namna timu hizi zilivyojenga upinzani tangu miaka kibao iliyopita, kwa kiasi kikubwa huenda akakufumbua macho ukajua kwanini zinapokutana timu hizi kongwe katika soka la Tanzania na Afrika Mashariki lazima panachimbika.
“Yanga na Simba ilikuwa timu moja bahati mbaya Waarabu wakaleta ubinafsi wao, unajua wanapokaa watu sehemu moja kila mmoja anakuwa na taratibu zake, Waarabu wakatamka hawa wauza samaki, wauza nazi wanatudharau wakati sisi tunatumia pesa zetu wanatuona wajinga wanataka tuwe na haki sawa, bora tuwaache Yanga sisi tuondoke”, alisimulia mzee huyo wakati akieleza namna Yanga ilivyogawanyika kuwa timu mbili.
“Wakaondoka wao na baadhi ya wachezaji, wakaenda kukaa mtaa mmoja unaitwa Kichwere kwasasa unaitwa mtaa wa Uhuru, hapo ndipo palipoanzia upinzani wa Simba na Yanga. Wale walioondoka wanasema, sisi tumeondoka wale waswahili lazima timu itawashinda, waliobaki nao wanasema sisi tumebaki na timu yetu ndogo wale tutapambana nao kwasababu sisi hapa ndio kwetu na ndio tuna asili ya hapa. Hapo ndipo upinzani wa Simba na Yanga ukaanza kushika kasi.”
“Simba wakati huo inaitwa Sunderland jina lililotolewa na mwingereza, Yanga kipindi hicho inaitwa Young Africans SC jina iliyopewa na mtoto wa kimarekani. Yanga haitaki kufungwa na Simba na Simba ikawa haitaki kufungwa na Yanga kwasababu Yanga ni watoto wadogo na masikini wakati huo Yanga ambao ndio ilikuwa timu ya masikini wanasema wale ni wageni hatuwezi kufungwa nao pamoja na ukubwa wao ndiyo kitu kilichoenea hadi leo.”
“Yanga na Simba hazikuwa na uadui, uadui wao ulikuwa ni wa dakika 90 lakini sasahivi Yanga na Simba kuna uadui sio upinzani. Kwahiyo Simba sisi hatuna uadui nao, wao ni warabu halafu sisi ni wamatumbi, wandengereko na wazaramo.”
Mpina ataka wanaosoma 'cheti' nao wapewe mikopo bofya hapa
Pato La Taifa Lakua Kwa Asilimia 7.9 bofya hapa
Maalim Seif 'Kumshitaki' Lipumba kwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) bofya hapa
UPDATED!: List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017 bofya hapa
Manispaa ya Temeke kugawanywa bofya hapa
Mapokezi ya viongozi CUF yaota mbawa bofya hapa
Wachambuzi wa uchumi watoa neno kwa ATCL bofya hapa
Wawakilishi wapitisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar bofya hapa
Simba, Yanga mwendo wa kimya kimya bofya hapa
Korti yatupa kesi dhidi ya Pierre Nkurunziza bofya hapa

Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)