WASHAMBULIAJI WA YANGA WAMEMSIKIA MGEVEKE ANAVYOWAAMBIA?


Beki wa kati wa kikosi cha Mwadui FC Joram Mgeveke amezungumza mambo kadhaa kabla ya kupigwa kwa mtanange huo siku ya Jumamosi September 17 kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Mgeveke amesema yeye binafsi pamoja na timu nzima kwa ujumla wako tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaotazamwa kwa karibu pamoja na Dar es Salaam derby (Azam vs Simba) bila kusahau Mbeya derby.

“Kwa upande wangu mimi nipo tayari kwa mechi na pia sio mimi tu, kwa ujumla sisi kama timu tupo tayari kupambana na Yanga na sio hatu ila ni timu yoyote tukayo kutana nayo wajipange”, amesema Mgeveke

“Mshambuliaji yeyeto atakayepata nafasi kwenye kikosi chao nipo tayari kupambana naye, haijalishi ntakutana na nani kwenye mchezo dhidi ya Yanga”, Mgeveke aliji baada ya kuulizwa amejipanga vipi kukabiliana na safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Kila mchezaji navaa namba flan ya jezi kwa sababu zake binafsi, wengine inatokana na mapenzi waliyonayo kwa wachezaji wanaowazimia. Lakini nilipotaka kujua kwa nini Mgeveke anavaa jezi namba 24 mgongono, alisema mama yake na motto wake ndiyo wanaomfanya avae namba hiyo kwenye mgongo wake.

“Namba hii inamaana kubwa sana kwangu, mamaangu na mwanangu wamezaliwa tarehe 24. Naipenda sana namba hiyo.”

Beki huyo wa zamani wa Simba amesema kwa sasa yeye ni mchezaji halali wa Mwadui baada ya kumaliza mkataba wake na Simba ambao walimtoa kwa mkopo kwenda kwa wachimba madini wa Shinyanga.

“Nilikuwa nacheza Mwadui kwa mkopo nikitokea Simba, lakini mkataba wangu na Simba umemalizika, nilizungumza na Mwadui wakaamua kunipa mkataba wa mwaka mmoja.”
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top