TAMBWE, NGOMA WAFUNGA YANGA IKIENDELEZA UBABE KWA MWADUI


Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Matajiri wa Almasi timu ya Mwadui FC, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na ubabe wa hapa na pale, Yanga waliuanza mchezo kwa kasi na ndipo mnamo dakika ya sita tu, mshambuaji hatari wa timu hiyo Amissi Tambwe alipofunga bao la uongozi kufuatia mpira kuzagaa zagaa langoni mwa timu ya Mwadui kutokana na mpira wa faulo uliochingwa na Juma Abdul.



Amanusura Yanga wapate bao la pili dakika ya 12 lakini shuti la Donald Ngoma liligonga mwamba na kutoka nje.

Msuva alikaribia kufunga goli dakika ya 15 na 20 lakini umakini mdogo ulimfanya ashindwe kufunga.

Dakika ya 43, kiungo mahiri wa Yanga Thabani Kamusoko aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niyonzima.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Yanga kuwa mbele kwa bao 1-0.

Takwimu za kipindi cha kwanza



Dakika ya 81 Msuva kwa mara nyingine tena alishindwa kufunga goli la wazi baada ya shuti lake kudakwa kwa umahiri mkubwa na kipa wa Mwadui.

Yanga walipata pigo lingine baada ya mchezaji wao mwingine beki Kelvin Yondan kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’.

Mshambuliaji wa Yanga kutoka Zimbambwe Donald Dombo Ngoma aliifunga goli la pili dakika ya 90 na kuzima ndoto za Mwadui kurudisha goli walau kupata sare katika uwanja wao wa Nyumbani.

Hii ni mara ya tatu Yanga na Mwadui wanakutana. Yanga wamefanikiwa kushinda mara mbili na kutoka sare mara moja.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top