Kesi ya Mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha CHANNEL TEN Daudi Mwangosi


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali ombi la wakili wa upande wa utetezi la kumuachia huru mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha CHANNEL TEN, marehemu Daudi Mwangosi ambapo sasa mtuhumiwa huyo ana kesi ya kujibu.

Awali wakili msomi kutoka upande wa utetezi Rwezeula Kaijage aliwasilisha ombi la kuitaka mahakama kumuachilia huru mtuhumiwa kwa madai kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri hauoneshi kuhusika kwa moja kwa moja kwa mtuhumiwa huyo.

Akizungumza mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Iringa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk Paulo Kihwelo amesema Mahakama imeamua ktk shauri hilo la mauaji kuwa mtuhumiwa ana kesi ya kujibu na kwa msingi huo hatua hiyo inailipeleka shauri hilo kuingia katika hatua mpya ya utetezi.

Wakili wa kutoka upande wa utetezi Rwezaula Kaijage amesema wameridhika na uamuzi uliofikiwa na mahakama hiyo na kusema hatua iliyopo mbele yao ni utetezi ambao amesema utatolewa kwa njia ya kiapo.

Mahakama imepanga kuendelea na shauri hilo hapo kesho majira ya saa 3 za asubuhi ambapo mshitakiwa ataanza kujitetea mahakamani hapo. 
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top