Marekani kupeleka misaada ya kijeshi Israel kwa mkataba wa dola Bilioni 38

Image captionRais Obama na Netanyahu hawakutani mara kwa mara

Marekani imekubali kusambaza misaada ya kijeshi nchini Israel ndani ya miaka 10 ijayo kwa mkataba wa dola bilioni 38, mkataba huo ni mkubwa katika historia ya Marekani.

Katika mkataba huo Israel watapokea dola milioni 500 kwa mwaka kwa ajili ya mpango wa ulinzi wa makombora.

Lakini Israel wanatakiwa kufanya makubaliano kadhaa na Marekani ya kupata fedha ikiwemo makubaliano ya kutochukua fedha za ziada kutoka Congress na kuahidi kuwa hawatatumia fedha za msaada kwa ajili ya ulinzi wake mwenyewe.Image captionNetanyahu alitembelea ngome ya jeshi la anga ya Israel mwezi Agosti

Makubaliano hayo yamekuja baada ya miezi kumi ya mazungumzo.

Maofisa wanasema kuwa Rais Obama na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wanaweza kukutana kwa mazungumzo katika mkutano mkuu wa umoja wa mataifa jijini New York.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top