MWANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Tutaonana kuzimu”
Kabla hata Rahab ajafyatua risasi ya aina yoyote ndege ikayumba gafla na kuwaangusha raisi na Rahab, kutokana na Samson kuifunga mitambo yote ya ndege, ikiwemo mashine baadhi za uendeshaji wa ndege, zimesababisha marubani kushindwa kuikwepa ndege
ya abiria ya shirika la Fly Emirates, ambayo zimekutana kwenye njia moja, marubani wa ndege ya abiria hawakuweza kuiona mapemba ndege ya Raisi wa Tanzania, kutokana na kushindwa kuiona kwenye rada zao, na wakajikuta wakiingonga, ndege ya raisi wa Tanzania kwenye ubavu wa nyuma wa ndege na kuisababisha kugeuka mara mbili na kuanza kwenda chini kwa kasi sana, huku ndege yao ya abiria ikiianza kuwaka moto
ya abiria ya shirika la Fly Emirates, ambayo zimekutana kwenye njia moja, marubani wa ndege ya abiria hawakuweza kuiona mapemba ndege ya Raisi wa Tanzania, kutokana na kushindwa kuiona kwenye rada zao, na wakajikuta wakiingonga, ndege ya raisi wa Tanzania kwenye ubavu wa nyuma wa ndege na kuisababisha kugeuka mara mbili na kuanza kwenda chini kwa kasi sana, huku ndege yao ya abiria ikiianza kuwaka moto
ENDELEA
Kelele za abiria zilizo andamwa na vilio vya uchungu, ziliendelea kusikika kwenye ndege ya raisi wa Tanzania bwana Ptraygod Makuya, kwajinsi ndege inavyozidi kwenda chini ndivyo jinsi ilivyozidi kuwaka mato mwingi na kuendelea kupasuka baadhi ya sehemu na kuzidi kulete maumivu makali kwa kila abiria aliye kubwa na kitu chochote kikali, ambacho kinaugusa mwili wake na kuzidi kumuumiza, huku wengine wakijikuta wakipoteza viungo vyao vya mwili.Hali hii inaendelea sawaswa na hali iliyopo ndani ya ndege ya abiria iliyo gonga sehemu ya nyuma ya ndege ya Raisi.Ndani ya chumba walichopo Samson, Rahab na rais Praygod, hali inazidi kuwa mbaya, kwani computer zote zinaanza kulipuka moja baada ya nyingine, kwa haraka Rahab anajitahidi kushikilia moja ya nguzo ya chuma, huku mkono wake mmoja akimshikilia Raisi ambaya anavutwa na upepo mwingi, unaoingia kwenye chumba chao, ukitokea nje kutokana na ukuta wa chumba chao kutoboka kutokana na motom mkali unaoendelea kuiteketeza ndege
“Muheshimiwa Raisi endelea kujikaza”
Rahab alizungumza kwa sauti ya juu huku mkono wake wa kulia, akiendelea kumshikilia Raisi, huku mkono wake wa kushoto pamoja na mguu wake wa kulia kwa pamoja vikiwa vimezunguka kwenye nguzo ya chuma inayo endelea kumsaidia asitoke nje ya chumba hicho.Hali kwa upande wa Samson inazidi kuwa ngumu sana kutokana na upepo mwingi kuendelea kuingia ndani ya ndege, kutokana na kipigo kikali alicho kipata kutoka kwa Rahab, ambacho kimempelekea mikono yake kukosa nguvu ya kushikilia kwenye baadhi ya vitu vilivyomo ndani ya ndege.Samson anajikuta akiachia kwenye moja ya sehemu aliyo ishikilia na upepo mkali unamtoa nje, huku akipiga kelele za kuomba msaada, Ndege nayo ikazidi kwenda chini kwa kasi kubwa huku, ikizidi kuchanguka baadhi ya maeneo yake
***
Baada ya Fetty kukata simu anawageukia manahodha wawili wanao kiendesha chombo cha kivita kijulikanacho kwa jina la ‘Sabmarine’ au Nyambizi, huku mkononi mwake akiwa ameishika bunduki yake aliyopiga risasi kadhaa pembeni
“Mutafanya kile ambacho mimi nitawaelekeza, Sawa?”
Fetty alizungumza huku bunduki yake akiwa ameielekeza kwa wanahodha hawa, ambao nao ni wanajeshi wa wajeshi la maji nchini Tanzania,
“Sa…wa”
Mmoja alijibu huku mwili wake ukimtetemeka sana, hadi haja ndogo akaanza kuihisi ikimwagika
“Kwanza hapa tulipo ni wapi?”
Anna aliuliza kwa sauti ya ukali
“Hapa tupo bahari ya Pasifiki maharibi kwa bara la Asia, katika nchi ya Australia”
Nahodha mmoja alizungumza huku akitazama kifaa maalumu ambacho kina namba nyingi, ambazo kwa mtu wa kawaida si rahisi kuweza kugundua ni nini kinacho tazwamwa
“Mmmmmmm…..!!”
Halima aliguna huku akiwatazama wezake kwani hakuelewa kitu kinacho zungumzwa hapo ni kitu cha aina gani
“Tutarudi vipi Tanzania?” Agnes aliiuliza
“Tanzania tumeiacha mbali sana?”
“Ndio tutarudi vipi Tanzania” Fetty aliuliza kwa sauti ya ukali, na kuwafanya manahodha kuzidi kutetemeka
“Tutar….”
Kabla nahodha mmoja ajamalizia sentesi yake, akastushwa na kingora kilichopo pembezoni mwa chumba chao kikianza kulia huku kifaa kingine mbele yao chenye kioo kikukubwa mithili ya simu aina za I pad, kikianza kuonyesha vitu vilili virefu vyenye rangi nyekundu vikija kwa kasi sana
“Mungu wangu, ni mabomu haya”
Nahodha mmoja ambaye umri wake umekwenda kidogo alihamaki huku kajasho kakianza kumwagika usoni mwake akitazama kioo hicho kwa macho yake makubwa kiasi
“Mabonu……!!?”
Anna aliuliza huku naye macho yakiwa yanamemtoka
“Ndio, tumeshakamtwa kwenye rada ya nchi ya Australia”
Kila mmoja akaanza kuomba sala yake ya mwisho, kutokana na mabomu hayo kuzidi kuja kwa mwendo wa kasi huku yakionekana kukilenga chombo chao ambacho kinapita kwa siri chini ya bahari hii kubwa ya Pasific, katika eneo la jeshi la nchini Australia
***
Makamu wa Raisi wa Tanzania bwana Gift, anaendelea kujipongeza kwa kuona kifo cha raisi Praygod, kikiwa kimetokea katika wakati muafaka, kwani ni kipindi kifupi tangu waingie madarakani baada ya kushinda uchaguzi kwa kishindo kikubwa, kama chama pinzani cha YRPP(Youth Revolution Political Party), ambacho muundo wake mkubwa unaongozwa na vijana wengi akiwemo Raisi wao kijana bwana Praygod Makuya
“Vipi mume wangu mbona unashangilia?”
Mke wa makamu wa Raisi alimuuliza mume wake, baada ya kurudi nyumbani kwake akiwa na tabasamu kubwa usoni mwake akitokea ofisini kwake, alipo kaa kwa siku mbili mfululizo pasipo kurudi nyumbani kutokana na swala zima la kujaribu kuitafuta ndege ya raisi Praygod Makuya
“Nina furaha sana, mke wangu yaani leo naamini nitakupiga hata vitano”
Maneno ya Gift yakazidi kumshangaza Magnalenar ambaye ni mke wa Raisi
“Sasa, mbona unanishangaza mume wangu, nchi ipo kwenye maombolezo ya kufiwa kwa rafiki yako mkubwa, wewe unashangilia”
“Mke wangu kwangu nifuraha ndio, kwani kufa kwake ndio mafanikio yangu”
“Unashangilia kwa kuwa raisi au?”
Magnalener aliuliza huku sura yake akiwa ameikunja akimtazama mume wake ambaye ameanza kuserebuka ndani ya chumba chao, huku shati lake akiwa amelifungua vifungo vyote na mkononi mwake akiwa na chupa ya whyne
“Achilia mbali kuwa raisi, ila ninafuraha sana kwa Praygod kufariki”
“Nahisi umepagawa wewe, mtu aliye kutoa kwenye ubunge hadi kukupa umakamu wa Raisi, leo hii amefariki wewe unashangilia?”
“Haaaa wewe kinacho kuuma ni nini?”
Magnelener akaachia msunyo mkali huku akipanda kitandania na kujifunika shuka akiendelea kumtazama mume wake anaye andelea kugumumia mapafu ta whyne
“Jiandae kwa vitano”
“Nimechoka na sitaki uniguse na hizo pombe tano, mtu huna hata huruma kwa rafiki yako, sijui wewe upojee, muone na hili jitumbo lako kama…..”
Magnalener alizungumza huku akiachia msunyo mkali na kumfanya Gifti kuachia tabasamu pana na kushusha mafumba mawili ya whyne kwa haraka haraka
“Asante sana Samson, mwanangu kwa kuniondolea huyo mwehu duniani”
Gift alizungumza huku akipiga hatua kwenda kwenye kitanda alicho lala mke, taratibu akazivua nguo zake na kubaki kama alivyo zaliwa na kujirusha kitandani,
“Samson yupi huyo aliye muua raisi?”
“Hakuuhusu”
“Ahaa kumbe wewe na Samson ndio mumeshirikiana katika hili”
Magnalener alizungumza huku akikaa kitako kitandani akimtazama mume wake kwa jicho kali sana, Gift akaupeleka mkono wake wa kulia kwenye ziwa la upande wa kushoto la mke wake na kustukia akizwabwa kibao kikali cha shavu kilicho muacha mdomo wazi akishangaa
SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……24
“Gift ukiendelea kunisumbua na mapombe yako tutaonana wabaya”
Magnalener alizungumza huku akiufunika mwili wake vizuri pasipo tatizo la aina yoyote, taratibu Gift akajilaza upande wa pili wa kitanda chake kwani anamuelewa kabisa mke wake ni mkorofi, na akizungumza huwa anamaanisha na kitu amabacho anakizungumza kwa wakati huo
***
Upepo mkali na uzito wa mwili wa Raisi Praygod vikazidi kupambana na nguvu za Rahab, ambazo taratibu zikaanza kumuishia mwili mwake na kujikuta akianza kuuchia taratibu nguzo aliyo ishikilia
“Muheshimiwa Raisi, nimechoka”
Rahab alizungumza kwa sauti kubwa huku upepeo ukiendelea kumpiga usoni mwake na kujikuta akizidi kuchanganyikiwa na kujihisi vibaya.Raisi Praygod Makuya akamtazama Rahab vizuri kwa jinsi anavyo jitahidi kuyaokoa maisha yake, machozi ya uchungu yakaanza kumwagika.
“Binti ninakuomba uniachie niende”
“Hapana muheshimiwa Raisi siwezi kufanya hivyo”
“Unaweza binti tafadhali ninakuomba ufanye nilivyo kuagiza”
“Wewe ni Raisi wa nchi yenye watu si chini ya milioni thelathini na nne, huwezi kufa kirahisi, unahitaji msaada wangu.Na nitakupigania kama raisi wangu”
Rahab alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, huku hali ya rangi ya mwili wake ikianza kubadilika na kuingia uwekundu fulani, uliao changiwa na maumivu makali yanayo yapata kwa kumshikulia Raisi mwenye kilo si chini ya sabini.Maneno ya kujiamini kwa Rahab, yakaanza kumpa matumaini mapya Raisi Praygod, ya kuoko kutoka kwenye ajali hii ya ndege yake, Macho ya Rahab yakatazama kwenye shimo ambalo muda mchache ulio pita Samson alichomolewa kwa upepo mkali kiasi cha kuto julikana ni wapi alipo kwenda kuangukia
“Muheshimiwa unaona hilo shimo chini yako?”
Rahab alimuuliza Raisi Praygod Makuya kwa sauti kubwa sana, na kumfanya Raisi kutazama chini nakuona shimo kubwa likiingiza upepo mkali ukitokea nje, raisi akajibu kwa kutingisha kichwa akiashiria kwamba ameliona shimo hilo
“Sasa ninakuachia, na mimi ninafwata kwa nyuma”
Rahab alizungumza kwa kujiamini, huku akitazama baadhi ya vitu vikiendelea kuteketea kwa moto ndani ya chumba walichopo, Raisi akameza fumba la mate akarudia tena kulitazama shimo ambalo Rahab amemuomba aweze kutoka. Kisha akayarudisha macho yake upande wa Rahab, wakatazama kwa muda usoni huku kila mmoja akiwa haliamini jaribio wanalo lifanya, ila hapakuwa na jinsi nyingine zaidi ya kufanya hivyo kuliko kuteketea kwa moto mkali unaozidi kuwaka ndani ya ndege yao.
Raisi Praygod akajiachia mikononi mwa Rahab, upepo mkali ukamvuta kwenda nje, Rahab naye, akaiachia nguzo ya chuma aliyo ishikilia na upepo mkali ukamvuta kwenda nje, wapambe wa Raisi Praygod Makuya, wakiwemo washauri wake wakuu pamoja na walinzi wake, wakajikuta wakilipuka na ndege ya raisi na kupoteza maisha yao, huku wengine wakiwa wameshasali sala zao za mwisho huku wengine wakiyaita majina ya mama zao wakiomba wasaidiwe
***
Kila mmoja ndani ya Submarine(Nyambizi) amayafumba macho yake akisubiria kulipuliwa na mabomo hayo yaliyo kilenga chombo chao, ndani ya dakika kumi nzima wakawa bado wameyafumba macho yao wakiusikilizia mlipuko huo, ila sivyo kama walivyo dhani, mtu wa kwanza kuyafumbua macho yake ni Halima, hii nibaada ya kungojea kwa muda mrefu, pasipo mabomo hayo kufika kwenye nyambizi yao, kwani kwa mwendo kasi wa mabomo hayo ilionyesha kwamba zimesalia sekunde 59 hadi mabomo hayo kuwafikia sehemu walipo
“Jamani mbona sioni chochote?”
Halima alizungumza na kuwafanya wezake wote kiyafumbua macho yao, ila kitu ambacho bado kinaendela kuwapa wasiwasi ni jinsi king’ora kilichopo ndani ya chumba chao kikiendelea kulia kwa sauti ya juu
“Kuna tatizo gani, nyinyi?”
Fetty alizungumza kwa hasira huku bastola yake akiwa amewaelekezea manahodha wa meli hii ya kivita inayo tembea chini ya maji
“Hata sisi hatujui” Nahodha mmoja alijibu huku jasho jingi likimwagika kwa wingi mwlini mwake
“Hii ni amri fanyeni haraka muturudishe Tanzania”
Agnes alizungumza huku akiwatazama manahodha hawa walio valia nguo za jeshi la maji, hapakuwa na jinsi zaidi ya wao kugeuza submarine yao na kuanza safari ya kurudi Tanzani, umbali wa kilomita zipatazo themanini na nne(84), gafla submarine yao ikatingishika
“Ni nini hicho?” Halima aliwauliza manahodha
“Tumekwama kwenye, mwamba wa barafu”
Nahodha alizungumza huku akiwaonyesha, mwamba mkubwa wa barafu, uliopo kwenye bahari waliyopo ya Atilantic, inayosifika kwa kuganda kwa barafu katika kipindi kirefu.
“Kwahiyo kama tumekwama?” Anna aliuliza
“Hatuwezi kusonga mbele, itatulazimu kukaa hapa kwa kipindi kirefu hadi hizi barafu ziyayuke”
Nahodha mmoja alizungumza huku akishusha pumzi, akiwatazama Fetty na wezake jinsi walivyo jawa ha mshangao mkubwa
“Sasa itakuwaje?”
“Hatuna jinsi, huchi nikipindi cha baridi, itatulazimu kukaa hapa si chini ya miezi mitatu hadi miinne hadi barafu zima liyanyuke, kipindi tunapita kwa mara ya kwanza ndio tulikuwa tunamalizia msimu wa barafu ila kurudi kwetu ndio, kosa tulili lifanya”
Karibia wote wakajikuta wakishusha pumzi zao, kila mmoja akihofia juu ya maisha yake, baridi kali ikaanza kupenya kwenye ngozi zao, jambo lililoanza kuzua wasiwasi mwingi sana kweye maisha yao
“Itatubidi chombo kitokeze kwenye usawa wa bahari la sivyo tutakufa humu ndani”
Nahodha mkuu alizungumza
“Kikitokeza usawa wa bahari hakutakuwa na madhara yoyote kwetu?” Agnes aliuliza huku akijikunyata
“Ndio, ila kuna makoti makubwa yapo humu ndani itatulazimu kuyatumia, kwa ajili ya kujikinga na baridi iliopo humu ndani”
Halima na Anna wakaondoka na nahodha mmoja wakaingia ndani ya chumba cha kuhifadhia makoti makubwa yanayotumika katika kipindi cha baridi kali.Wakachukua makoti yaliyo sawa na idadi yao, na kurudikatika chumba maalumu walipo Fetty na nahodha mkuu.Submarine yao ikaanza kupanda kwenda juu tataribu taratibu, hadi kikatokezea usawa wa bahari, na katika eneo zima walilopo limeganda kwa barafu kubwa.
“Itatubidi kuitoa miili ya watu walio kufa humu ndani, isije ikatuozea” Anna alitoa wazo
“Kwa baridi hii wataoza kweli?” Halima alizungumza
“Kuoza wanaweza wasioze ila ni kinyaa, unataka kusema tutakaa na maiti tukionana nazo zaidi ya mwezi humu ndani, hembu tusidanganyane hata kama sisi ni makatili ila kuishi na maiti ndani mimi wala siwezi” Fetty alizungumza
“Powa nimewaelewa, tunazitoa saa ngapi?” Halima aliuliza
“Sasa hivi?”
“Mmmmm” Agnes alijikuta akiguna tuu
“Sawa”
Kwa kushirikiana na manahodha wakaanza kutoa mwili mmoja baada ya mwengine wa askari wote walio waua ndani ya Submarine(Nyambizi), kutokana na wingi wa miili ya askari walio fariki ndani ya Submrine ikawalazimu kutumia masaa mengi
“Ahaaaaaa”
Agnes alishusha pumzi nyingi, huku akiutazama mwili wa maiti alio uatupa mbali kidogo na sehemu kilipo chombo chao, kutokana kwa kuganda kwa barafu wanaweza kutembea juu y barfu pasipo tatizo lolote.Agnes akaanza kuifikicha fikicha mikono yake aliyo valia gloves nyeusi, zinazo zuia kupitisha ubaridi, huku pumzi anayo itoa mdomoni mwake ikijawa na mvuke mwingi
“Mmmm, hii baridi si mchezo”
Alizungumza taratibu akipiga hatua za kurudi ilipo Submarine, kabla hajapiga hatua hata nne akastukia kuona kitu kikitua kwenye barafu kwa ngufu kikitokea juu, ikamlazimu kutazama juu na hakuona kitu cha aina yoyote zaidi ya ukungu mwingi, ulio tawala juu ya anga la bahari.Akatazama upande kilipo anguka kitu hicho na taratibu akaanza kupiga hatua za taratibu, huku basstola yake ikiwa mkononi mwake, akafika sehemu kilipo anguka kitu hicho na kukuta mwili wa mtu ukiwa unavuja damu, sehemu za tumboni mwake huku, huku akiheme kwa mbali akionekana bado yupo hai
***
Upepo mkali ukazidi kumpeleka chini Rahab, huku muda mwini akijitahidi kuvuta pumzi, ila anashindwa kutokana na hewa ya sehemu alipo kuwa ni nzito sana,
“Ohooo Mungu wangu ninakufa mimi”
Rahab alizungumza huku, akibana pumzi zake, kwa mbali akamuona Rais Praygod akizidi kwenda chini kwa kasi, Rahab akaibana mikono yake usawa wa mwili wake kuelekea nyuma, huku miguu yake akibananisha kwa pamoja, akajikuta akipata uwiano wa kuweza kwenda chini, kwa mwendo wa kasi pasipo kuyumba, kwa mtindo wa kwenda chini ali ufanya Rahab ukamsaidia kumfikia karibu muheshimiwa Raisi ambaye hadi kwa wakati huu amepoteza fahamu, Rahab akafanikiwa kumshika Raisi Praygod Makuya kiuno chake, na wote wakajikuta wakienda chini na kuingia kwenye maji mengi ya bahari.Rahab akajitoa kwenye usawa wa brahi huku akiheme kwa nguvu, hii ni kutokana na kuishiwa na pumzi, aliyokuwa ameibana kwa muda mrefu
“Raisi……!!”
Rahab alizungumza baada kwa mshangao baada ya kutokumuona Raisi Praygod kwenye usawa wa bahari jambo lililoanza kumpa wasiwasi mwngi.Ikamlazimu kurudi tena ndani ya maji, kutazama kama anaweza kumuona raisi, ila hakumuuona
“Mungu wangu!!”
Rahabu alizungumza kwa kuhamaki baada ya kuona kitu kikija kwa kasi katika upande aliopo yeye, kwa haraka haraka akagundua kwamba ni samaki mmoja hatari aina ya Papa, ndiye anaye karibia kufika katika eneo alilopo
PICHA 5: Tingatinga Lilivyofukua mamilioni yaliyokuwa Yamefichwa ardhini bofya hapa
Waziri atolea maelezo taarifa ya serikali kuhakiki watumishi wanavyotumia mishahara yao bofya hapa
Waziri atolea maelezo taarifa ya serikali kuhakiki watumishi wanavyotumia mishahara yao bofya hapa
TCRA yakipa onyo kali kituo cha runinga cha Clouds, Yakifungia kwa miezi 3 kipindi cha 'Take One' kwa kukiuka kanuni za utangazaji. bofya hapa
Polisi Aliyerekodiwa Akipokea Rushwa Kuchukuliwa Hatua bofya hapa
Jeshi La Polisi Nchini Latoa Onyo Kali Kwa Wananchi Wanaojichukulia Sheria Mkononi. bofya hapa
Polisi Aliyerekodiwa Akipokea Rushwa Kuchukuliwa Hatua bofya hapa
Jeshi La Polisi Nchini Latoa Onyo Kali Kwa Wananchi Wanaojichukulia Sheria Mkononi. bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)