Kumbe hata Yanga imewahi kuipa Simba mkono!



Sasahivi kinachozungumzwa ni kwamba, Yanga ndiyo timu ambayo imedhalili kutokana na kichapo cha goli 5-0 na hapo ndipo Simba wanapotambia licha ya kupoteza mechi zote katika msimu uliopita.

Sports Extra ya Clouds FM imezungumza na shabiki mkongwe wa Yanga kutaka kujua katika historia ya mechi za Simba vs Yanga, hakuna kipigo kikubwa ambacho Yanga imeshawahi kutoa kwa Simba ukiachana na kipigo cha 5-0 ilichopokea hivi karibuni?

“Naitwa Said Abdallah Bangazula nimezaliwa mwaka 1935, sisi Yanga ndiyo tulikuwa wakwanza kuifunga Simba magoli matano pale uwanja wa Karume. Ilichezwa mechi ya ligi ikatokea tafrani kati ya Kitwana Manara na Emanuel wakagombana, Emanuel akafungiwa.”

“Marehemu mzee Kondo Kipwata akaenda wakamchukua Emanuel, Mzee Kitwana Kondo akaenda Dar es Salaam ligi wakati huo akawaambia wamfungulie ili ligi ichezwe, walipomfungulia ndio wakati huohuo Simba alipofungwa goli tano huku mmoja ya wafungaji akiwa ni mchezaji kutoka Tanga Farasi Mweupe Said Zimbwe.”

“Baada ya kufungwa goli tano Simba wakabaki kujinasibu kwamba wao wameifunga sana Yanga yeye alifungwa goli 5 kabla ya kujua yeye ataifunga lini Yanga magoli mengi.”

Unaamini matumizi ya nguvu za giza kwenye mpira?

“Kitu kikubwa sana kwenye mpira ni mazoezi na kujua mpira, sisi tulikuwa tunajua mpira zaidi ila wao walikuwa wanapenda vitu hivyo, sisi tulikuwa tunaamini katika Mungu.”
 
 




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top