Mkwasa ametoa mtazamo wake kuelekea Yanga vs Simba



Siku moja kuelekea pambano la Simba na Yanga, Charles Boniface Mkwasa mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni kocha Mkuu wa timu ya taifa ametoa mtazamo wake kuelekea mchezo huo wa Jumamosi.

“Timu hizi mbili zinapokutana inakuwa ni mechi ambayo inagusa watanzania wengi sana, lakini ukitazama sana hii mechi inakuwa na maneno mengi, presha kubwa, tension kubwa si tu kwa mashabiki lakini tension inaingia hadi kwenye timu na wachezaji wakashindwa ku-perform au timu ikashindwa kucheza kiufundi kwasababu wanataka kucheza kwa haraka kutafuta ushindi au kukamiana.”

“Ladha ya mpira ikakosekana lakini kwasababu ni mechi ya wakubwa basi kunakuwa na mpambano lakini ukiangalia standard ya namna gani mipango inatoka upande mmoja kweda mwingine, huwezi kuiona kwasababu wachezaji hawachezi kwa lengo la kuonesha standard ya mpira ila lengo ni ushindi kama unavyojua timu moja inapofungwa kizaa-zaa huwa kinaanzia hapo na migogoro inaanzia kwenye mechi kama hizi.”

“Kwahiyo ni mechi ya kawaida tu lakini inakuwa na wingi wa ushabiki.”

Ukiangalia performance ya timu zote mbili unadhani nani anaweza kupata wakati mgumu au mwepesi zaidi ya mwingine?

“Mpira huwezi kuangalia historia ya mechi iliyopita, kila mechi unayokutana nayo inakuwa na approach yake tofauti. Timu unaweza kuchezanayo leo na kesho ukachezanayo ileile lakini haiwezi kuwa vilevile kama ulivyochezanayo kwenye mchezo uliopita lazima kutakuwa na vitu vimebadilika, inakuwa ni mechi nyingine kabisa.”

“Kwa ninavyozitazama timu hizi mbili, timu moja kwa maana ya Simba, wanaingia wakijiamini pengine watakuwa wakijiamini kwakuwa wanaongoza ligi na timu yao imetulia kidogo na inaweza kucheza kupata matokeo mazuri lakini Yanga mechi yao ya ugenini ilisumbua inaweza ikawaletea shida kidogo.”

Tukirudi katika historia yako wakati bado ukiwa mchezaji, unakumbuka tukio gani nambalo wakati ukicheza mechi za Simba na Yanga?

“Wakati nachukuliwa kwenda kucheza Yanga, walikuwa na lengo la kutoa uteja wa kufungwa na Simba kwasababu kwa kipindi kirefu walikuwa wanafungwa magoli mengi, tukachukuliwa sisi ili kuweza kupunguza magoli mengi, kwahiyo ilikuwa kama ni azimio la kusajili timu itakayoleta ushindani.”

“Kipindi kile wakati tunachukuliwa sisi, Yanga ndiyo ilikuwa imefukuza karibu timu nzima kwahiyo timu ikawa inajengwa upya, katika kipindi hicho timu ikawa imepitia misukosuko mingi ikiwa ni pamoja na kufungwa na Simba mechi nyingi hadi kuonekana wateja wa Simba.”

“Kizazi chetu sisi baada ya kuongeza nguvu kidogo tukawa tumebadilisha usemi na tukawa tumeleta ushindani na ikafika kipindi tukawa tumewafunga kama miaka mitatu au minne mfululizo hivi. Mimi niliwafunga Simba goli muhimu kwenye mwaka 1983 hivi.”
 
 




Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top