Na Athumani Adam
Imekuwa ni wiki ya tambo na majigambo kuelekea mchezo wa watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa. Kila upande unaamini kuibuka na ushindi kutokana na ubora wa vikosi vyao. Lakini kwenye kila mchezo kuna wachezaji hatari (Key Players) ambao mara nyingi uwezo wao umekuwa chachu ya kubadili matokeo.
Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya mchezo huo, makala hii inakupa uchambuzi kuhusu wachezaji hatari kwenye safu za ushambuliaji kwa timu zote mbili ambao wanaweza kuzisaidia timu zao kupata matokeo.
SIMBA
IBRAHIM AJIB
Ametenegeza kombineshi na Laudit Mavugo ambayo imezaa mabao matano ndani ya mechi sita. pia Ajib ana uwezo wa kumiliki mpira, kushuka eneo la katikati kusaidia viungo bila kusahahu jicho la kuliona goli.
Kama atakuwa yupo fiti siku ya mchezo bila shaka atakuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa na madhara kwa upande wa Yanga endapo asipo wekewa ulinzi wa kutosha.
SHIZA KICHUYA
Amekuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza tangu aliposajiliwa akitokea Mtibwa Sugar kwenye dirisha la usajili lililopita. Ni hatari anapocheza winga ya kulia japokuwa anatumia mguu wa kushoto. anakokota mipira kuelekea golini tofauti na mawinga wengi ambao wanalikimbia goli ili kupiga krosi.
Hadi sasa amepachika mabao manne akiongoza kwenye orodha ya wafungaji bora, kama ni Haji mwinyi au Oscar Joshua endapo mmoja wao atapata nafasi ya kuanza kwenye beki upande wa kushoto wa Yanga, wanapaswa kuwa makini vinginevyo ni mchezaji ambaye anaweza kufanya lolote ndani dakika 90 za mchezo.
YANGA
AMISSI TAMBWE
Hana mambo mengi sana anapokuwa uwanjani, wakati mwingine anaonekana wakati anashangilia bao. Mrundi huyu amethibitisha kuwa ni miongoni mwa washambuliaji hatari kwa misimu kadhaa kwenye ligi ya Vodacom msimu huu amefunga mara tatu hadi sasa.
Safu ya ulinzi ya simba hususani beki ya katikati ambayo imekuwa ikiongozwa na Lufunga pamoja na mzimbabwe Mwanjali wanapaswa kuzunguka na Tambwe muda wote. Kama watamuacha Tambwe apate nafasi ya kuruka pekee yake kwenye mipira ya Vichwa bila shaka anaweza kutikisa nyavu zao.
DONALD NGOMA
Amefanikiwa kufunga bao moja hadi sasa, lakini huyu ni mchezaji wa kuamua mechi kubwa. Anacheza kwa kasi na kutumia nguvu jambo ambalo linachangia kuweka presha kwa mabeki wengi hatimaye kufanya makosa.
Safu ya ulinzi ya simba lazima iepuke kufanya makosa kwani Ngoma ni aina ya wachezaji ambao wanaweza kukuadhibu kwa kufanya kosa moja. Nae namuweka kwenye orodha ya wachezaji ambao wanaweza kufanya makubwa na kuzipatia timu zao matokeo yaliyokuwa bora.
Mpina ataka wanaosoma 'cheti' nao wapewe mikopo bofya hapa
Pato La Taifa Lakua Kwa Asilimia 7.9 bofya hapa
Maalim Seif 'Kumshitaki' Lipumba kwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) bofya hapa
UPDATED!: List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017 bofya hapa
Manispaa ya Temeke kugawanywa bofya hapa
Mapokezi ya viongozi CUF yaota mbawa bofya hapa
Wachambuzi wa uchumi watoa neno kwa ATCL bofya hapa
Wawakilishi wapitisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar bofya hapa
Simba, Yanga mwendo wa kimya kimya bofya hapa
Korti yatupa kesi dhidi ya Pierre Nkurunziza bofya hapa
Pato La Taifa Lakua Kwa Asilimia 7.9 bofya hapa
Maalim Seif 'Kumshitaki' Lipumba kwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) bofya hapa
UPDATED!: List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017 bofya hapa
Manispaa ya Temeke kugawanywa bofya hapa
Mapokezi ya viongozi CUF yaota mbawa bofya hapa
Wachambuzi wa uchumi watoa neno kwa ATCL bofya hapa
Wawakilishi wapitisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar bofya hapa
Simba, Yanga mwendo wa kimya kimya bofya hapa
Korti yatupa kesi dhidi ya Pierre Nkurunziza bofya hapa
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)